Ya moyoni: Msafara wa awamu hii 'unakera'!

Ya moyoni: Msafara wa awamu hii 'unakera'!

wabongo bwana as if hii kero imeanza leo wakati toka kipindi kilichopita hii kero ilikuwepo au tunajifanyaga hatuoni yaliyokwisha pita??
 
Kuwasimamisha wananchi dakika zaidi ya 60 bila sababu ya msingi,kwani wanafikiri sisi wananchi hatunaga haraka sijui? Wanakera sana.
Juzi kati hapa sijui msafara wa nani ulikuwa unatoka njia ya mtwara huko;tulisimamishwa njiani kama masaa mawaili hivi.
 
Huko Dodoma ndio hakuna watu? (Japo sio wengi sana)
Unafikiri yanayofanyika huku huko hayatafanyika?
Kamanda vipi aiseee...
Mkuu Nifah Dodoma mpaka wafikie karaha utapita muda kidogo. Dodoma sio kubwa wakitoka Area C ushabiki mjini so kutakuwa na unafuu kidogo. Darisalama ni kero kwa kweli!
 
JPM alipokuja Mwanza ilikuwa ni kero kubwa. Tena nikilinganisha hna Dar na Mwanza huwa ovyo zaidi. Huku mnaweza kusimamishwa wakati hata anayekusimamisha hajui huyo kiongozi yupo wapi. Kuna wakati mwakajana tulisimamishwa kwa sababu ya ujio wa Pinda alipokuwa akitokea Shinyanga, tulikaa masaa 4 ndiyo akatokezea.

Haya mambo yapo Afrika tu ambapo kiongozi huonekana ni mfalme, na muda wa mwananchi wa kawaida huonekana hauna thamani. Very disqusting!
 
Umenikumbusha ile siku ya kufungua maonyesho ya 7/7!
Nilikaa kwenye foleni hadi mipango yangu yote ikaharibika! [emoji34]
Hivi nawe huwa na mipango ha ha haaa, kwa hiyo Jamaa alichoka kusubiri?
 
Huko Dodoma ndio hakuna watu? (Japo sio wengi sana)
Unafikiri yanayofanyika huku huko hayatafanyika?
Kamanda vipi aiseee...

Kuvuja pakacha nafuu ya mchukuzi. Dar tumebeba mpaka biashara zetu zinakwama. Dodoma, itakuwa mji wa bureaucrats / warasimu zaidi hivyo hata wakisimama kupisha misafara hakuna madhara makubwa. Watuachie Dar yetu tupige mzigo bila bughudha.
 
mwanza walifunga barabara zote kuanzia SAA 10 mpaka 12yaan haijawai kutokea in kero kubwa sana wahusika waliangalie, tena wanafunga barabara hata ambazo hazipiti msafara
 
Duh isije kuwa anaenda kwa Ndugai kumzuia asiweke suluhu na ukawa, maana Tulia atakuwa kashachombeza huko makao kuwa jamaa anataka kufuta maamuzi yake ya kimzuka!!
Job atamwambia arudi magogoni akakae apitie katiba vizuri ndio arudi..
 
Huko Dodoma ndio hakuna watu? (Japo sio wengi sana)
Unafikiri yanayofanyika huku huko hayatafanyika?
Kamanda vipi aiseee...
Nifah, ondoa shaka watu wa Dodoma wanawapenda sana hao jamaa. Mimi naombea Magu afanye haraka kwenda huko ili tuwatwisha wagogo zigo lao la misumari limetuumiza vya kutosha hapa Dar Lol
 
Nifah, ondoa shaka watu wa Dodoma wanawapenda sana hao jamaa. Mimi naombea Magu afanye haraka kwenda huko ili tuwatwisha wagogo zigo lao la misumari limetuumiza vya kutosha hapa Dar Lol
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
You made my evening
Thanks [emoji9]
 
Watanzania,tangu zamani,tunawapenda na kuwaheshimu viongozi wetu wa kitaifa hadi wale wa mitaa. Viongozi wetu tunawalinda kwa kila mmoja wetu na namna yake.

Viongozi wakuu watatu wa kitaifa: Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu huwa na misafara maalum wanapokwenda mahali fulani. Ingawa misafara ya sasa haina gari la wagonjwa na imepunguziwa idadi ya magari,kuna jambo linakera.

Watumiaji wengine husimamishwa kwa kati ya dakika 30 hadi 70 wakisubiri msafara upite. Foleni hutamalaki haswa. Inafikia wakati,madereva hutoka kwenye magari yao na abiria huamua kutembea kwa miguu. Misafara ya awamu hii inakuwa kero. Kuna mambo ya kurekebisha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kwanini mnapinga wanavyotaka kuhamia Dodoma.?
 
Back
Top Bottom