Ya moyoni: Msafara wa awamu hii 'unakera'!

Ya moyoni: Msafara wa awamu hii 'unakera'!

Sio popote ulimwenguni mkuu.Kuna nchi mfano South Africa misafara huwa inakuwa aidha pembeni ya high way/yellow line ama inapita barabara ya juu huku wengine wakipita barabara za chini.

Hata jambo dogo kama hilo unashindwa kulielewa? Huoni kwamba AK kuna Miuondo mbinu mingi zaidi na kuwezesha Misafara kupita kwa haraka wkt mambo mengine yakiendelea? Sasa hapa Dar Raisi anaelekea Tegeta ulitakaje, ulitaka kipi kifanyike kwamba watu wasisimamishwe wote wapite njia moja?
 
Kama unaona misafara ya viongozi Tanzania inakera hamia Somalia.Kule msafara wa viongozi ukitokea ukiwa na gari lazima ushuke ulitelekeze na utokomee porini kwa sababu kule havipigwi ving`ora ni kurusha risasi njia nzima kila upande watu wapishe misafara ya viongozi ipite

pointless
 
Ina maana Raisi hakujua kuwa Ndugai karudi? Au baada ya kumwona Maalimu
Mbowe ndo kajua yupo

Au anaenda mkanya kuhusu kusawazisha mambo
 
Duh! Sasa msipokaa muda mrefu utajuaje Mh anapita? Kuna boss mmoja alikuwa anatusisitiza sana kuwahi kazini tatizo ni kuwa yeye mwenye funguo za ofisi anachelewa, hivyo tunajikuta tuko nje tunasubiri boss afike!! Mkuu anasema HAPA KAZI TU hakuna kuangalia bunge live ili watu wafanye kazi, hakuna mikutano ya hadhara ili watu wafanye kazi. Ok issue inakuja pale tunapoambiwa watu wamesimamisha msafara wake ili wamsalimie, na yeye kusimama na kuwasalimia badala ya kuwasisitiza waache poteza muda waende fanya kazi. Mh mwenye anakuwa na mikutano ya hadhara watu wanaoendakumsikiliza huwa wanaacha fanya kazi. Then leo misafara yao ndio hiyo inasimamisha shughuli za watu. Sasa sijui Mkuu anataka nini
 
Huku nako ni kuonesha kuishiwa hoja kabisa.
 
Watanzania,tangu zamani,tunawapenda na kuwaheshimu viongozi wetu wa kitaifa hadi wale wa mitaa. Viongozi wetu tunawalinda kwa kila mmoja wetu na namna yake.

Viongozi wakuu watatu wa kitaifa: Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu huwa na misafara maalum wanapokwenda mahali fulani. Ingawa misafara ya sasa haina gari la wagonjwa na imepunguziwa idadi ya magari,kuna jambo linakera.

Watumiaji wengine husimamishwa kwa kati ya dakika 30 hadi 70 wakisubiri msafara upite. Foleni hutamalaki haswa. Inafikia wakati,madereva hutoka kwenye magari yao na abiria huamua kutembea kwa miguu. Misafara ya awamu hii inakuwa kero. Kuna mambo ya kurekebisha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Bado Miezi tu ndio ujue sababu moja wapo ya kuhamia Dodoma ili wananchi kama ninyi mfurahie maisha!
 
Dah, leo nimekaa kwa foleni zaidi ya dakika 50, sijui nani alikuwa anapita, ila alikuwa anaelekea Bagamoyo bila shaka.

Alikuwa Mh. Rais nadhani akienda kwa Mh. Ndugai nilipigwa almost two hours ya zero movement nikienda mjini. Ushauri hivyi kwa nini wasitumie Helikopta naona pia ni salama zaidi.
 
Watanzania,tangu zamani,tunawapenda na kuwaheshimu viongozi wetu wa kitaifa hadi wale wa mitaa. Viongozi wetu tunawalinda kwa kila mmoja wetu na namna yake.

Viongozi wakuu watatu wa kitaifa: Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu huwa na misafara maalum wanapokwenda mahali fulani. Ingawa misafara ya sasa haina gari la wagonjwa na imepunguziwa idadi ya magari,kuna jambo linakera.

Watumiaji wengine husimamishwa kwa kati ya dakika 30 hadi 70 wakisubiri msafara upite. Foleni hutamalaki haswa. Inafikia wakati,madereva hutoka kwenye magari yao na abiria huamua kutembea kwa miguu. Misafara ya awamu hii inakuwa kero. Kuna mambo ya kurekebisha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Usijari siku sio nyingi usumbufu huu utahamia ugogoni,huku baharini tutaendelea kutelezaaa Kwa sanaaa! Tukielekea kula bata.
 
Mfalme Juha anatamba kwenye himaya yake,nani wa kumuuliza kitu bana?
Ikulu kazi zimekwishaa?
 
Kwani wewe upo wapi na hiyo misafara imetokea wapi? Kwa kawaida kusubiri msafara ni jambo la kawaida popote ulimwenguni
Ulimwengu upi unangelea? yaani kuishi Dar kwako ndio unafikiri ulimwengu mzima!!?? unachekesha kweli kada, tembea uone
 
Mbona yanajulikana. Ukweli ni watu kubanwa na mkojo hadi basi wakati wa hii misafara Nilipata wazo la kuwa na vyoo vya umma kila baada ya mita 50.
 
Hata jambo dogo kama hilo unashindwa kulielewa? Huoni kwamba AK kuna Miuondo mbinu mingi zaidi na kuwezesha Misafara kupita kwa haraka wkt mambo mengine yakiendelea? Sasa hapa Dar Raisi anaelekea Tegeta ulitakaje, ulitaka kipi kifanyike kwamba watu wasisimamishwe wote wapite njia moja?
O.T.P
 
Back
Top Bottom