Steven Mwakyusa
Member
- Dec 27, 2012
- 44
- 1
Muda sasa umepita toka utoke ule unaoitwa Waraka Wa Jay Dee dhidi ya Clouds. Nilisikia pia ufafanuzi wa Ruge dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa, na hivi majuzi nimebahatika kusikia ama kusoma kile kinachoendelea baina ya Jay Dee na MwanaFa...
Sikutaka kuandika chochote, ila hili la Juzi ambalo limeshabikiwa na wengi kwa Mwana FA kuitwa MwanaFatuma limenifanya niandike kitu. Wengi wameshangilia inawezekana kwa kufuata mkumbo ama kutojua tafsiri hasa ya MwanaFA kuitwa Fatuma.
Mengi yamesemwa katika kuhalalisha ufatuma wa MwanaFa, na akaenda mbali kudai yeye ndiye alimfanyia FA chorus na alikuwa hawezi panda Fiesta bila yeye. Inawezekana ni kweli, ila lazima tujue kuwa mtu anayekaa na kuongelea kila wakati mambo yaliyopita, kuna uhakika kuwa hana lolote jipya la kufanya. Sitaki kuamini kama FA kafika alipofika kwa ajiri ya "Alikufa kwa ngoma", "msiache kuongea" na "Hawajui". Kama ni hivyo, basi Jay Dee kwanini asiukubali mchango wa FA wakati alipoimba Wanaume kama Mabinti?
Nikirudi kwenye huu unaoitwa Ufatuma wa MwanaFA nakuona kukengeuka kwa hali ya juu kwa huyu dada yetu. Kama alivyofanya kwenye "Wanaume kama Mabinti", anachokifanya hapa ni kuchukua kunakoitwa kutumika kwa FA na kuwahalalishia wanawake. Tuseme FA anafanya upuuzi pengine kama anavyodhani, lakini kwanini huu upuuzi tuwaamishie akina Fatuma? Je wanawake ni halali yao kukwamishana, kuwekeana fitina na kutumika? Anataka kutuambia anachokifanya FA kingekuwa halali endapo angefanya Linah, Recho ama Stara Thomas?
Mpaka sasa sijaona hoja ya msingi ambayo Jide ameisimamia zaidi ya kutafuta public sympathy. Haina maana ya kuendelea kulumbana tena kwa kejeli ambazo mwisho wa siku zinamshushia heshima na kuonesha jinsi alivyo upstair!!!
Kikubwa afanye kazi, hakuna namna ya kukwepa ushindani, ndiyo maana hata ukienda bar leo utakuta friji ya Pepsi na ya Coca cola ikiwa pembeni, na bado maisha yanaendelea.