Ya JayDee na MwanaFa....Anachokifanya Jide ni kudhalilisha wanawake!!!


Status
Not open for further replies.
S

Steven Mwakyusa

Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
44
Likes
0
Points
0
S

Steven Mwakyusa

Member
Joined Dec 27, 2012
44 0 0
Muda sasa umepita toka utoke ule unaoitwa Waraka Wa Jay Dee dhidi ya Clouds. Nilisikia pia ufafanuzi wa Ruge dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa, na hivi majuzi nimebahatika kusikia ama kusoma kile kinachoendelea baina ya Jay Dee na MwanaFa...

Sikutaka kuandika chochote, ila hili la Juzi ambalo limeshabikiwa na wengi kwa Mwana FA kuitwa MwanaFatuma limenifanya niandike kitu. Wengi wameshangilia inawezekana kwa kufuata mkumbo ama kutojua tafsiri hasa ya MwanaFA kuitwa Fatuma.

Mengi yamesemwa katika kuhalalisha ufatuma wa MwanaFa, na akaenda mbali kudai yeye ndiye alimfanyia FA chorus na alikuwa hawezi panda Fiesta bila yeye. Inawezekana ni kweli, ila lazima tujue kuwa mtu anayekaa na kuongelea kila wakati mambo yaliyopita, kuna uhakika kuwa hana lolote jipya la kufanya. Sitaki kuamini kama FA kafika alipofika kwa ajiri ya "Alikufa kwa ngoma", "msiache kuongea" na "Hawajui". Kama ni hivyo, basi Jay Dee kwanini asiukubali mchango wa FA wakati alipoimba Wanaume kama Mabinti?

Nikirudi kwenye huu unaoitwa Ufatuma wa MwanaFA nakuona kukengeuka kwa hali ya juu kwa huyu dada yetu. Kama alivyofanya kwenye "Wanaume kama Mabinti", anachokifanya hapa ni kuchukua kunakoitwa kutumika kwa FA na kuwahalalishia wanawake. Tuseme FA anafanya upuuzi pengine kama anavyodhani, lakini kwanini huu upuuzi tuwaamishie akina Fatuma? Je wanawake ni halali yao kukwamishana, kuwekeana fitina na kutumika? Anataka kutuambia anachokifanya FA kingekuwa halali endapo angefanya Linah, Recho ama Stara Thomas?

Mpaka sasa sijaona hoja ya msingi ambayo Jide ameisimamia zaidi ya kutafuta public sympathy. Haina maana ya kuendelea kulumbana tena kwa kejeli ambazo mwisho wa siku zinamshushia heshima na kuonesha jinsi alivyo upstair!!!

Kikubwa afanye kazi, hakuna namna ya kukwepa ushindani, ndiyo maana hata ukienda bar leo utakuta friji ya Pepsi na ya Coca cola ikiwa pembeni, na bado maisha yanaendelea.
 
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Messages
23,417
Likes
11,988
Points
280
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2010
23,417 11,988 280
Mtu makini? ?
 
chinga4

chinga4

Senior Member
Joined
Mar 18, 2013
Messages
131
Likes
27
Points
45
chinga4

chinga4

Senior Member
Joined Mar 18, 2013
131 27 45
Huna jipyaaa, na wewe ni MwanaFatuma #2 ... Mwanaume wa kweli haendeshi na kuamuliwa na wanaume wenzake. Huyo MwanaFatuma ana elemnt za ulebelari. Au na wewe ndo wale wale???? Usitutafutie Ban.. Toa thread yako...
 
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
3,304
Likes
48
Points
145
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
3,304 48 145
Unatetea ufatuma kwa hamisi? Kama ni kweli asiambiwe kisa anaemwambia atadhalilisha wanawake?
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
107,263
Likes
131,756
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
107,263 131,756 280
Huna jipyaaa, na wewe ni MwanaFatuma #2 ... Mwanaume wa kweli haendeshi na kuamuliwa na wanaume wenzake. Huyo MwanaFatuma ana elemnt za ulebelari. Au na wewe ndo wale wale???? Usitutafutie Ban.. Toa thread yako...
Mmh hupendi wengine wawe na mawazoni tofauti nayakwako?
 
Neiwa

Neiwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
732
Likes
61
Points
45
Neiwa

Neiwa

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
732 61 45
Kama huna hoja kaa pembeni acha uvuvuzela. Kosa la mwanaume lake la mwanamke linagusa wanawake wote? Wewe wa wapi wewe!
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,272,655
Members 490,101
Posts 30,456,352