Xabi Alonso kuwa Kocha mpya Wa Chelsea

Xabi Alonso kuwa Kocha mpya Wa Chelsea

Zirconium

Senior Member
Joined
Feb 1, 2025
Posts
185
Reaction score
236
Chelsea wamefikia makubaliano ya kumsajili Xabi Alonso kama kocha wao mpya Je ni Chaguo Sahihi!?

Xabi Alonso ni kocha bora sana kimkakati, na baadhi ya watu wanasema angepaswa kusubiri kazi bora zaidi. Lakini kivutio kikubwa kwake hapa ni kwamba pia anataka kuwa na mamlaka makubwa badala ya ule mfumo wa kisasa wa uhusiano kati ya kocha mkuu na sporting director. Anataka aina ya uhuru ambao Arteta alipewa — blank canvas — ambapo anaweza hata kupinga bodi ili kusajili wachezaji anaowataka.

Kwa bodi ya Chelsea, mfumo wao wa usajili haujafanya kazi vizuri, hivyo matakwa ya Alonso yanaonekana kuwa na matumaini zaidi kuliko kuendelea kuwaamini watu waliopo kwenye uongozi wao kujenga kikosi. Tuna sampuli ya miaka minne ya kushindwa kwao kwenye usajili. Alonso kupewa nafasi ya kuunda dira ya usajili ni kama jaribio lao la mwisho kuokoa enzi ya Clearlake, kwa sababu wameonyesha kushindwa kuunda mfumo wa uongozi unaofanya maamuzi mazuri.

Iwapo Alonso ana maono ya kutosha kustahili mamlaka haya bado haijajulikana, na hilo ndilo litakaloamua mafanikio au kushindwa kwa uteuzi huu. Usajili kule Leverkusen ulikuwa unasimamiwa kabisa na Simon Rolfes ambaye ni bora sana, na alimpatia Alonso vipaji bora vya vijana vya kuendeleza. Alonso aliishauri Real Madrid kuwasajili Huijsen, Carreras na Mastantuono, jambo ambalo linaonekana kuwa na matokeo ya mchanganyiko.

Kwa ujumla mimi huwa sipendi makocha kuwa na nguvu kubwa kwenye usajili wa wachezaji. Wana majukumu mengi sana kiasi kwamba kufanya kazi hiyo pamoja na kufundisha timu huwa ni mzigo mkubwa. Lakini kuna mifano kama Arteta ambapo faida zinazidi hasara.

Pia mvuto wa Alonso kwa wachezaji unaweza kuwa mkubwa sana, hivyo kwa ujumla mimi pia ningefanya vivyo hivyo kama ningekuwa kwenye nafasi ya Clearlake. Natazamia kuona usajili wa kwanza watakaofanya kwa sababu utaonyesha mengi kuhusu mwelekeo na mafanikio ya uteuzi huu
IMG_7023.jpeg
 
Wamarekani wanapenda sana kuwapa timu makocha ambao kwao itakuwa ni rahisi kuwaburuza. Miaka kadhaa iliyopita Louis Enrique aliwafuata mpaka London na project yake ya kuirejesha Chelsea kwenye kuoambania makombe!

Kilichotokea walimpuuza na kumpa kocha mwingine nafasi. Baada ya hapo, Enrique leo anaipa tu PSG makombe, huku Chelsea ikiendelea kuwa gunia la mazoezo. Hivyo hata Xabi Alonso hata simtabirii makubwa iwapo tu hatapewa nafasi kubwa ya maamuzi ndani ya timu!

Kwangu mimi Andon Iraola was the perfect coach for Chelsea.
 
Lakini ujue kwamba Chelsea ndio klabu bingwa ya dunia na walipata kombe wakiwa na kocha asiye Luis Enrique.
 
NI vizuri kocha aachwe achague wachezaji anaowapenda kwa sababu mwisho wa siku yeye ndiye anayetakiwa kuwajibika kwa matokeo mabaya.

Guardiola amekuwa akifanya vizuri kwenye vilabu mbalimbali anavyofundisha kwa sababu ni yeye ndiye huchagua wachezaji anaoona wanaendana na falsafa yake.

Vilabu vya kiswahili kama Simba na Yanga ni shida viongozi kukubali kumwachia kocha achague wachezaji anaowapenda kwa sababu viongozi hao wanakuwa na maslahi katika usajili.

Kuna pesa ambayo viongozi hao hupata katika zoezi hilo la usajili na wakishasajili wanalazimisha wachezaji wao wapate namba mara kwa mara timu inapocheza hata kama hafanyi vizuri na tunaona kwa wachezaji kama Dube, Nzengeli nk.
 
Alonso kuna dili la Liver alikuwa analisubiri lakini liver wameamua kubaki na Kipara ngoto ili awashushe daraja msimu ujao, Kuhusu Alonso kusubiri kazi nzuri zaidi ya Chelsea ilikuwa hakuna coz Chelsea nayo sio timu ndogo, maana ukiangalia timu kubwa zote tayari zina makocha wa msimu ujao na nyingine tayari zishaweka wazi profile za makocha wanazotaka halafu kingine Alonso hawezi kutoka kwenda ligi nyingine Kwa sasa nje ya La liga na EPL maana ni kijana na anahitaji ligi shindani na hiyo ndio mentality aliyosema kuwa anayo...Hadi Nyumbu zimebaki na Carrick.
 
Wamarekani wanapenda sana kuwapa timu makocha ambao kwao itakuwa ni rahisi kuwaburuza. Miaka kadhaa iliyopita Louis Enrique aliwafuata mpaka London na project yake ya kuirejesha Chelsea kwenye kuoambania makombe!

Kilichotokea walimpuuza na kumpa kocha mwingine nafasi. Baada ya hapo, Enrique leo anaipa tu PSG makombe, huku Chelsea ikiendelea kuwa gunia la mazoezo. Hivyo hata Xabi Alonso hata simtabirii makubwa iwapo tu hatapewa nafasi kubwa ya maamuzi ndani ya timu!

Kwangu mimi Andon Iraola was the perfect coach for Chelsea.
Tate Mkuu Andon Iraola ni kocha mzuri lakini hatufahi kwa aina ya wachezaji tulionao hawafiti mfumo wake. Andon Iraola anapenda soka la kasi anafaa zaidi kama akienda Liverpool wakati sisi tuna Enzo, Palmer, Joao Pedro ambao ni key figure hawana hiyo kasi na ndio maana wakaenda kwa Alonso ambaye soka lake halina tofauti sana na Enzo Maresca.Another factor waliozingatia ni kuwa Alonso tayari ana story ya kuchukua kombe la Bundesliga mbele ya Bayern na pia kafundisha team kama Real Madrid tayari imemtengenezea heshima kiasi ambacho itafanya wachezaji wetu wamuheshimu tofauti na tungeleta kocha mwingine ambaye Hana story ya kafundisha team kubwa au kuchukua kikombe na ndio iliyosababisha Rosenior afeli Chelsea.
 
Kwangu mimi makocha bora wa Chelsea ni Antonio Conte na Thomas Tuchel.
 
Lazima tukubali Abramovic hayupo tena namatumaini makubwa na Alonso viongozi wameshajifunza kwa matokeo mabaya tuliopata ndio maana wamempa role ya Manager badala ya kuwa kocha pekee kwahiyo atahusika na sajili zote
Binafsi sioni quality players Chelsea kwa sasa.
 
Binafsi sioni quality players Chelsea kwa sasa.
Mbona wapo Enzo fernandez huyu kachukua kombe la Dunia na alikuwa ni mchezaji kijana Bora kwenye michuano lakini pamoja na kwamba msimu tulikuwa ovyo lakini Enzo fernandez ana namba nzuri, Palmer huu msimu wake watatu japo alikuwa majeruhi muda mwingi lakini ndio best player wetu, Jaoa Pedro ana contribution ya magoal na assist 20+ bila penalty msimu wake huu Tena ni wa Kwanza, James captain unajua ubora wake, Caicedo mkataba umeme hodari, Pedro Neto, Estevao, Levi Colwil, Cucurella, Joel Hato yupo vizuri na Gusto.Hao wote niliyokutajia ni wachezaji Bora ila wameathirika na msimu mbaya tulionao lakini individual ni wachezaji wazuri sisi tunawachezaji ila Kuna baadhi ya maeneo yalihitaji yaongezewe nguvu ila viongozi wetu wakatuua hiyo ndio iliyopelekea msimu huu uwe si mzuri na mnapokuwa na msimu mbaya hata wale wazuri wataonekana wabaya ngoja nikupe mfano Arsenal Wana wachezaji wakawaida mfano Madueke, Zubimend, Tossard, Gabriel Jesus, Kai havertz, Ben White, Martinell lakini team yao inaonekana ni nzuri ni kwasababu ya wachezaji wao wanajituma na mfumo mzuri wa uchezaji ambao unaoeleweka kwa kila mchezaji inaficha mapungufu ya mchezaji mmoja mmoja ndio maana wanaonekana ni team tishio kitu ambacho sisi tunakosa ndio unaona wachezaji ni wabaya lakini kiuhalisia haiko hivyo
 
Wamarekani wanapenda sana kuwapa timu makocha ambao kwao itakuwa ni rahisi kuwaburuza. Miaka kadhaa iliyopita Louis Enrique aliwafuata mpaka London na project yake ya kuirejesha Chelsea kwenye kuoambania makombe!

Kilichotokea walimpuuza na kumpa kocha mwingine nafasi. Baada ya hapo, Enrique leo anaipa tu PSG makombe, huku Chelsea ikiendelea kuwa gunia la mazoezo. Hivyo hata Xabi Alonso hata simtabirii makubwa iwapo tu hatapewa nafasi kubwa ya maamuzi ndani ya timu!

Kwangu mimi Andon Iraola was the perfect coach for Chelsea.
Uko sahihi Lakini hata mimi nasubiri kuona kama atafanya majukumu kama Manager na sio head Coach hasa kwenye usajili …. Nguvu kubwa zaidi katika kikosi cha Chelsea ni kiwango chao cha kiufundi. Reece, Hato, Colwill, Caicedo, Enzo, Palmer — hawa wote ni wachezaji wanaofaa mfumo wa mchezo wa kumiliki mpira, kutawala umiliki wa mchezo na kujenga mashambulizi kwa utaratibu. Huwezi kuomba kocha bora zaidi ya Alonso ili kuimarisha uwezo wa aina hii ya wachezaji
 
Conte alichukua ubingwa wa Epl kupitia kikosi cha Mourinho na Conte hajawahi kuchukua ligi ya mabingwa ulaya kwanini umemtaja hapo?

kikosi cha mourinho ambacho kilashapoteza dira, msimu wa nyuma yake kabla ya conte killishia karibu nafasi ya 10
 
kikosi cha mourinho ambacho kilashapoteza dira, msimu wa nyuma yake kabla ya conte killishia karibu nafasi ya 10
Lakini kumbuka yote yalitokea kwasababu ya bifu la Mourinho na baadhi ya key figures wa team mpaka akawaita panya ambao ni Hazard, Diego Costa na Fabregas hao hao wachezaji wakawa muhimu kwenye kikosi cha Conte
 
Mourinho hakumaliza msimu, hata aliekuja baada yake pia hakufanya vizuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom