Albosignathus
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 4,898
- 1,051
Unaweza kueleza kidogo jinsi gani hiyo inakuwa? kisayansi.
Wewe acha mikwara mbuzi,Sayansi huijui wala nini,wewe mwenyewe ni mchawi.
Unaweza kueleza kidogo jinsi gani hiyo inakuwa? kisayansi.
Mkuu Nyalotsi,Huyu alikuwa mchumba wangu ambaye nilimpenda sana na tulikubaliana kuoana. Nilipatwa na matatizo njiani mwenzangu akanambia anaolewa na mtu mwingine (tulikuwa tunaishi mikoa tofauti). Niliumia sana na kutokana na hasira nikamwambia `Tutaona kama utaishi na huyo mwanaume.' Toka hapo sijawahi kuwasiliana naye tena!
Siku za karibuni alinitumia message kwamba anaomba kuongea na mimi, nikamtajia muda ambao ntakuwa free.
Muda huo akanipigia simu na kuanza kunilaumu `@nyalotsi kwanini umenifanyia hivi?'
Nikamuuliza, nimfenyaje?(huku nikiwa na mshangao)
`Umeniroga kila nikipata mimba inatoka, tafadhali sana nisamehe kama nilikukosea! Familia yangu itavurugika.'
Nilikata simu na kuanza kutafakari mambo mengi sana. Ina maana huyu dada kaniona mi mchawi? Mbona hata mizizi ya dawa za kawaida tu siifahamu? Hii laana gani tena? Baadaye nikakumbuka niliwahi kumtishia kwamba hataishi kwa amani na mumewe. Nikampigia simu na kumhakikishia kwamba siwezi kufanya kitu hiyo na wala sio muumini wa mambo hayo.
Nikamshauri pia waende na mumewe hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na wataalamu.!
Kweli duniani kuna mambo!!
Maneno uliyoyasema mazito ati!
Kwenye ulimwengu wa mwili, ndiko kwenye coincidence!, kwenye ulimwengu wa roho, hakuna coincidence!, kila kinachotokea, kilikuwa kitokee hivyo hivyo kitavyotokea!, every move, every action, every occorunce its all a pre meditated moves, kilikuwa kitokee!.coincidence! it happens.
Mmm ngoja nikauze nyumba yangu ya gongolamboto kisha nije nipate hiyo ya mgando na pembeni.Lakini 7 utahimili? Naona msiba unautaka wewe maana nina guu la mtoto utaliweza???
Mkuu Cyberteq!, you have the powers!.hamna lolote ni coincidence tu! Siku moja nilikuwa ofisini kwangu nafanya kazi, nakumbuka siku hiyo nilikuwa busy kupita maelezo, mpaka mchana wa saa8 sijatia kitu mdomoni wala kukaa. Akaja bwana mmoja kuchukua pesa, zile pesa nilkuwa nimeshazipanga kabisa ziko pembeni kwenye bahasha ndani ya draw, nina uhakika wa asilimia mia kuwa zilikuwa zimetimia, basi yule jamaa alipoingia tu akakuta nina purukushani vibaya mno akabaki amesimama kama dk kadhaa maana hata viti vilikuwa vimejaa, baadaye akanigutusha tu akasema "mkuu"..nilivoinua macho nikasema "daah, sorry kaka nimekuweka" nikachukua bahasha na kumpa, hakuhesabu pale akaondoka, dk kadhaa akarudi mbiao "samahani kaka hazijatimia"...what?.."kweli kaka"...hiyo pesa nimehesabu kwa umakini sana haiwezekani ipingue (nadhani yeye alivonikuta busy vile alijua nitajichanganya, kumbe ile pesa mimi nimeiweka kitambo kabla hata kazi hazijanitinga), nikamuuliza sh ngapi, akataja....mo way, thats too much siwezi kuchanganya kiasi hicho! akakomaa, nikajikuta kitu kimenipanda kwenye nafsi kimenikaba, nikafungua droo nikachomoa pesa nikampa huku nasema kwa mzuka wa hali juu "KAMA HII PESA NAYOKUPA SIYO HAKI YAKO UTAPOTEZA PESA NYINGI NDUGU YANGU NAKWAMBIA", Jamaa akachukua pesa akaondoka. Baada ya siku kadhaa nikaambiwa na jamaa yangu mwingine, "mbona yule jamaa anakusema vibaya, umechukua pesa yake kimazingara"...dafuq!!!!!? coincidence
siku nyingine tena niko ugenini nikakodi taxi, nikazunguka kidogo nikaingia kwenye ofisi fulani nikamwambia aningoje, muda kama wa saa moja hivi, nilivotoka nikamwambia aniache sehem, karibu tu, nauliza bili akaniambia elfu50...khaaa! bei ya kukodi siku nzima mkoa ule naijua vizuri ni elfu 80 mizunguko ya kawaida na mafuta kwake, huyu nikihesabu haizidi kilometa tano, na muda tuliotumia ni kama saa moja na nusu kuwa naye (mostly waiting), kwa mzunguko ule nisingekuwa na mzigo ningekuwa nimefanya kwa miguu tu! Akakomaa, hasira zikanipanda, nikamwesabia 50 nikawa nimeropoka..."UNAFIKIRI UTATAJIRIKA NA HIYO 50, ITAKUTIA UMASKINI, NDIYO NIMEKWAMBIA HIVYO"!....Loh, kama sjui nini, kesho yake napita mitaa fulani nikamkuta yuko garage, nikamsalimia akaanza kulalamika "KWELI KAKA NDIYO TUNAFANYIANA HIVI KWA AJILI YA VITU VIDOGO TU".....LOH! coincidence.
kuna vitu vinaweza kukutia kwenye mazingira magumu sana bila kukusudia, na watu inakuwa ngumu sana kukuelewa, lakini basi tu inatokea kama bahati mbaya!
Hivi unajua maneno yanaumba? Hivi unajua shetani anatumia maneno ya binadamu kupitishia laana zake? Inawezekana havihusiani but inawezekana pia laana uliyoapiza kwake ndio inamuathiri...
Nakushauri tu ufanye utaratibu wa kuifuta hiyo laana kwa mwenzio. .. msaidie kwa hilo
CYBERTEQ;9360206 siku nyingine tena niko ugenini nikakodi taxi said:Kweli mkuu faida ya dhuruma Mungu huipiga kofi ogopa dhuruma na udanganyifu imewacost wengi.".......apandacho mtu ndicho atakachovuna"
Ndio umemloga kweli kwani maneno huumba.Mkuu acha uchawi kwa jina la YESU! Vipi na kuruka na ungo unaweza? kwa maana nataka niende London.
Kiukweli ulimlaani japo inaweza isiwe sababu ya masahibu yake. Muambie umemsamehe kabisa kwa kukuumiza, na utubu kwa Mungu na kukiri kwa sala kuwa umemsamehe. Hii mammbo ya kuumiza nyoyo za watu can be haunting.
una "natural anciety witches in your body" "mtaje jina then zungumza kwa mkazo "fulani" sasa umepona"ninakuachia na sasa upo huru zaa watoto salama
Hahahah, kwamba ulikuwa unanijibu mimi eeh.
Duh hata kama ni usanii siwezi kumiliki personality tofauti hivi nisichemshe
Mmh pole umenikumbusha mbali Sana.
Nakumbuka nilikuwa na bf those years back. Nilimpenda kuliko hata nafsi yangu. Basi imeendaa akawa na mtu pembeni bila mi kujua. Kuna siku ikatokea huyo dada ajanitumia sms ya kunikashfu sana. Nikamwambia jamaa akabisha kuwa na uhusiano nae na hapo relationship ilikuwa imeshakuwa official kwao na kwetu.. nilikuwa nalia day and night. Nimejibembelezesha kwa jamaa wapi... baada ya miezi kibao ya kuumia nikasema enough is enough nikakata mawasiliano but kwa kumwambia maneno mabaya Sana like you will never be happy...hutafanikiwa etc etc.
Mmmmh baada ya two years nikasikia jamaa yupo vibaya mno kiuchumi...pia hana relationship stable kabisa.
Kuna siku bahati mbaya Sana si nikakutana nae bhana mahali....mmh nilichoka kabisa maana akaniambia kila anachofanya hajafanikiwa.La ajabu eti anasema eti ooh naomba ukubali nikuoe siwezi pata mtu kama ww.
I was like are you a nut case!!!
Sijaeleza yote asije akawa yupo humu akajua buure but no mengi na mabaya alinifanyia....