X wangu kaniambia nimemroga!

X wangu kaniambia nimemroga!

Kiukweli ulimlaani japo inaweza isiwe sababu ya masahibu yake. Muambie umemsamehe kabisa kwa kukuumiza, na utubu kwa Mungu na kukiri kwa sala kuwa umemsamehe. Hii mammbo ya kuumiza nyoyo za watu can be haunting.
Umenichekesha haswaaaaa Utende dhambi ya kuzini (maana wakati ule walikuwa hawajafunga ndoa). Ulaani na baadaye utubu kwa sala kuwa umemsamehe. Mimi nadhani laana yake haiwezi kufanya kazi maana walikuwa wanatenda dhambi. Angalikuwa mme halali wa ndoa hapo sawa
 
kwani kutubu ni sh ngapi mpendwa? katikati ya kutenda dhambi huko (manake ume'-presume walifanya uzinzi. unasahau kuna watu wanakuwa na mahusiano yasiyohusisha ngono pia) huenda laana ya mmoja wao ikampata mwenzie.

Umenichekesha haswaaaaa Utende dhambi ya kuzini (maana wakati ule walikuwa hawajafunga ndoa). Ulaani na baadaye utubu kwa sala kuwa umemsamehe. Mimi nadhani laana yake haiwezi kufanya kazi maana walikuwa wanatenda dhambi. Angalikuwa mme halali wa ndoa hapo sawa
 
Huyu alikuwa mchumba wangu ambaye nilimpenda sana na tulikubaliana kuoana. Nilipatwa na matatizo njiani mwenzangu akanambia anaolewa na mtu mwingine (tulikuwa tunaishi mikoa tofauti). Niliumia sana na kutokana na hasira nikamwambia `Tutaona kama utaishi na huyo mwanaume.' Toka hapo sijawahi kuwasiliana naye tena!

Siku za karibuni alinitumia message kwamba anaomba kuongea na mimi, nikamtajia muda ambao ntakuwa free.
Muda huo akanipigia simu na kuanza kunilaumu `@nyalotsi kwanini umenifanyia hivi?'
Nikamuuliza, nimfenyaje?(huku nikiwa na mshangao)
`Umeniroga kila nikipata mimba inatoka, tafadhali sana nisamehe kama nilikukosea! Familia yangu itavurugika.'

Nilikata simu na kuanza kutafakari mambo mengi sana. Ina maana huyu dada kaniona mi mchawi? Mbona hata mizizi ya dawa za kawaida tu siifahamu? Hii laana gani tena? Baadaye nikakumbuka niliwahi kumtishia kwamba hataishi kwa amani na mumewe. Nikampigia simu na kumhakikishia kwamba siwezi kufanya kitu hiyo na wala sio muumini wa mambo hayo.
Nikamshauri pia waende na mumewe hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na wataalamu.!

Kweli duniani kuna mambo!!
Ndo mkome kutoatoa makauli yenu kwa hasira, halafu baadaye mnaanza kutamani kuyameza maneno yenu..... Muulize Nchimbi naye lazima ayaoge si kayavulia nguo...
 
Ndo mkome kutoatoa makauli yenu kwa hasira, halafu baadaye mnaanza kutamani kuyameza maneno yenu..... Muulize Nchimbi naye lazima ayaoge si kayavulia nguo...

Aisee ndugu yangu kila mtu humu akianza kutoa idadi ya aliowalaani baada ya kutendwa utagundua ni nafuu yangu! Kuna watu humu walishalaani hata zaidi ya mara mia kidogo. Hili ni suala ambalo lipo kwenye jamii yetu hii.
 
Aisee ndugu yangu kila mtu humu akianza kutoa idadi ya aliowalaani baada ya kutendwa utagundua ni nafuu yangu! Kuna watu humu walishalaani hata zaidi ya mara mia kidogo. Hili ni suala ambalo lipo kwenye jamii yetu hii.
Kwa hiyo uwingi wa watoa laana ndo unakufanya uone we ni afadhari..???

 
Hivi unajua maneno yanaumba? Hivi unajua shetani anatumia maneno ya binadamu kupitishia laana zake? Inawezekana havihusiani but inawezekana pia laana uliyoapiza kwake ndio inamuathiri...
Nakushauri tu ufanye utaratibu wa kuifuta hiyo laana kwa mwenzio. .. msaidie kwa hilo
Kauli yako ya maneno yanaumba nimeisikia leo kwenye saa 6 kipindi cha hekaheka clouds radio, mtu aliibiwa TV na computer akamleta mganga akaambiwa alieiba lazima afe na jamaa na mke wake wakawa wanapiga umbea jamaa lazima afe wakati huo huo jamaa ambae inasemekana mwizi alikuwa anaumwa TB mwisho wa siku jamaa kweli akafariki (wadau wa mtaani wamemshikia bango kwamba yeye ndio amemwondoa)
 
Kwa hiyo uwingi wa watoa laana ndo unakufanya uone we ni afadhari..???

Nyalotsi amejaribu kwa kufuata mkumbo likampata la kumpata (ni sawa na kumtishia mtu kifo alafu akafa kiutata vivyo hivyo hata kwa hili utahusishwa), Ndio maana tunaambiwa kama mwenzako alifanya kosa kama lako siku za nyuma alafu hakuchukuliwa hatua isiwe kinga ya kutaka kusamehewa, kiujumla sio vizuri kutoa laana kwa binadamu mwenzako maana hata kama huna uchawi wakati mwingine hata kisayansi unaweza ukaleta athari za kisaikolojia kwa kuufanya mwili ukashindwa kufanya baadhi ya mambo mwisho wa siku afya ya mtu inadhoofu kutokana na magonjwa ya moyo na akili ambayo umeisababisha na hofu uliyompa na mwisho wa siku akifa wananzengo watasema wewe ndio umemloga
 
Last edited by a moderator:
Siwezi kubaliana na kitu ambacho haki-make any sense to me. Ili nikubaliane na kitu make me understand, sio kunitengenezea hofu, i don't get scared easily. Sasa whether nina weak mind au vinginevyo kwa kweli sijui.
Mambo mengi ya imani haya make sense ni ama unaamini or not
 
Wewe Naomba tuheshimiane sawa? We umeelewa nilichoandika au umenivamia tu?
Mbona?Joto hasira za nini?Yamkini sio wewe 'muumini wa weak mind/strong mind' lakini watu wenye tabia hizo wapo Jf.Ujumbe huwa uwafikie hao na sio wewe.Usinielewe vibaya ndugu yangu wewe ni mjumbe tu na mjumbe hauawi.
Pole kwa kukukwaza!!
 
Back
Top Bottom