Habari zenu wana MMU,
Kuna mambo huwa yanatokea sana unakuta watu mlikuwa wapenzi then mkajaachana alafu mnawekeana uhasama mie naona ni ulimbukeni
Mie hadi leo nlishawahi kuwa na wapenzi 3 tukaachana kati ya hao wawili ni marafiki/washauri wazuri tu haipiti siku hatujawasiliana au hata kutembeleana ofisini ,wanamfahamu mchumba wangu na wanamuheshimu japo yeye hawafahamu.
Nawapenda kifrendly na katika mawasiliano yetu wote hatujawahi ongelea mapenzi toka tuachane huwa tunaongea maswala ya kikazi na maisha kwa ujumla kiufupi ni kama kaka zangu wazuri tu!
Nafikiri ukaribu wangu na hawa wakaka sidhani kama una madhara yoyote au hata kwa future yangu japo nafikiria siku mbabe akijatambua nilishawahi kuwa na mahusiano nao asijezua mengine au nimweleze?
Ushauri wenu wakuu.