Belinda wa maisha yangu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
BELINDA WA MAISHA YANGU – SIMULIZI YA MAPENZI


Pingu za maisha ni kitu cha furaha na cha kutamaniwa na Binadamu yoyote yule.Ni siku ya furaha sana na ina kumbukumbu nyingi sana katika maisha hasa ikiwa unaemuoa au anayekuoa ni mtu wa ndoto yako.Yani mtu uliyetamani sana katika maisha yako yaliyo baki utumie nae siku hizi kwa mapenzi mazito.

Ndio siku ambayo mimi naikamilisha leo ikiwa ukingoni kabisa na sasa ni saa nane na mimi ndo naelekea chumbani na mke wangu mpya kabisa Belinda.


Baada ya shamra shamra za wiki nzima na baada ya Siku ile ambayo siku penda iishe maishani mwangu,hatimaye napata fursa ya kwenda fungate la mwezi mmoja nchini saudia na huko naandika hadithi hii ili kila mtu ajue kwanini nampenda sana huyu Belinda.


Ni utamaduni ambao ni wakigeni katika nchi zetu za Afrika,Utasikia mtu akisema familia fulani ni family friends wetu na vitu kama hivyo..Nakumbuka tuliishi katika nyumba za wafanyakazi wa shule ya sekondari Kiluka.Shule hii ilikuwa na wafanyakazi wengi sana na nyumba zao zilijengwa ndani ya eneo la shule hii.

Ndani ya jumuiya yoyote huwezi kupendwa au kuchukiwa na watu wote na hii ilitokea baada ya jirani wetu upande wa kushoto kuonyesha chuki sana kwa familia yetu na jirani wa upande wa kulia alikuwa ni family friend wetu.

Siku moja nikiwa natoka shule,shule ya msingi nikiwa nasoma darasa la kwanza,nilipata mshtuko baada ya mzazi wangu yani baba yangu kuwa na hasira sana na mimi na kuonyesha hali ya majonzi makubwa.Sikujua nini kimemsibu bali niliingia na kwenda kwenye meza ya chakula moja kwa moja maana nilikuwa na njaaa sana.

Nilipo maliza kula aliniita chumbani kwake.Kwa kawaida baba akiwa amechukia hukuita chumbani kwake na kutaka kujua ukweli ukimficha hapo ni kipigo kikali na hakuna huruma ila ukimwambia ukweli basi hupata furaha tena na huwa rafiki yako mkubwa.

Mzee Kise amesema wewe umemfanya vibaya mwanae mdogo yule anaitwa Ester..Ni kweli?alihoji baba yangu mzazi,Baba mimi nimeshinda shuleni toka asubuhi na hata home work zote nimefanya na kabla ya kuja hapa nyumbani,nimesubiri baiskeliyangu kwa dakika ishirini maana mwalimu aliiomba aende nayo mahali toka asubuhi na akachelewa kurudi na ndio maana nilishindwa hata kuja wakati wa kifungua kinywa.Nilimaliza kutoa maelezo yangu huku nikiwa sina wasiwasi kabisa.

Baba yangu aliniacha huku akisema jirani alikuja pale na matusi chungu nzima na amedai atakwenda polisi maana mtoto wake ameharibiwa vibaya sana ..nikataka kujua ukweli tu na kama ni hivyo naona mwache afanye atakalo hakuna shida wala haja ya kumfuatilia ..alimaliza mzee wangu na kuondoka zake.

Nikiwa shuleni siku ya tatu tokea uongo huo wa kusingiziwa niusikie,nilimuona jirani yule akiwa na mgambo wawili na walielekea hadi ofisi ya mwalimu mkuu.Walikaa kama dakika ishirini kisha nikaitwa ofisini kule.Ulikuwa wapi siku ya jumatatu?mbona hukuwepo shuleni?Alihoji mwalimu mkuu..Nilijieleza vizuri kisha nikamuita hata mwalimu niliyemuazima baiskeli na mwalimu wa darasa akathibitisha kwamba nilikuwepo shuleni siku nzima.

Kama haitoshi mzee yule jirani alienda tena polisi na safari hii wakaja hadi nyumbani kwetu na kunichukua na kunipeleka kituoni.Kijana sema ukweli ama tutakupiga sana fimbo..Hakuna ukweli ninaoweza kusema zaidi ya hou niliomwambia mkuu wa shule mbele ya askari na mzee huyu,kama nilisema uongo,mbona hawakunichukua pale pale hadi leo mliponifuata tena hapa?

Nilikaa pale hadi jumatatu nilipoomba mwalimu mkuu aitwe maana nilikuwa sitendewei haki na alipokuja niliachiwa na mzee yule alitakiwa anilipe fidia ya sh 200...enzi hizo ni mshahara wake kwa miezi 3.Hakuwa na ubishi ikabidi awe analipa kwa installment na nikawa huru.Ila ndo aliongeza chuki mara dufu.

Pale shuleni tunasoma na mwanae wa kwanza ambaye anaitwa Belinda.Binti huyu hunipa siri zote za kwao na apangayo baba yake dhidi ya familia yetu.Mara nyingi tumekuwa tukimchukia sana baba yake hasa kwasababu ni mlevi kupindukia na kila mara akilewa huwapiga wanawe pamoja na mkewe.Siku moja mkewe jirani huyu na watoto wake walipigwa na mzee huyu na kukimbilia kwetu..hatukuwa na hiyana tuliwapokea na kuwapa hifadhi ya usiku ule.


Kesho yake ilikuwa fujo kubwa toka kwa jirani aliyewatimua watoto na mkewe kwani alifika pale kwetu akiwa na hasira kana kwamba ni sisi tuliwaomba watoto na mkewe waje kwetu.Walikimbia kipigo..alisema mdogo wangu mmoja ambaye ni msanii sana wa maigizo.Jana ulikuwa mitungi sana kule kwetu tunasema uliweka bambuuuucha ya kushiba aliongeza mdogo wangu huyu..

BAADA YA MZEE HUYU KUONA MANENO YANAMKERA NA KUHISI AIBU ALIAMUA KUSHUSHA MATUSI KAMA MVUA...huku akiondoka na kuonya tusije wapokea tena watoto na
mke wake kwani nyumba ipo na yeye si mjinga kupiga watu bila kosa.Hii ni njia yangu ya kutoa mafunzo msiniingilie hata siku moja.alisema...mzee wetu alikaa kimya kisha akasema mwacheni aende zake na tumsamehe bure maana alikuwa ameamka na faida ya pombe kichwani.

Siku iliyofuata mzee wangu alinikalisha chini na kunipa maneno mengi yenye hekima na mafunzo ambayo nimeyaweka kichwani hadi leo.Wakati wote huu mama aliendelea kuwa mkimya sana maana nilihisi mama amechukia lakini nilisita pia kumhoji maana siku zote sikupenda kumuuliza maswali mama yangu na nilikuwa sipo karibu naye sana.

Tukiwa tunatoka shuleni mimi na Belinda bila kuwa na hofu,nilimuomba anisindikize sokoni kununua vitoweo vya jioni maana mama aliniagiza nipitie kule sokoni nikanunue vitu kadhaa.Bila hiyana alinisindikiza na njiani alinihadithia mambo mengi ya kwao na jinsi wanavyoteseka sababu ya pombe za baba yake.

Baada ya kununua kila kitu nilishangaa nashikwa bega na kupigwa kibao kikali sana,nilianguka chini na kujikusanya pale na kuangalia alikuwa ni baba yake Belinda akiwa na hasira kibao..untaka kuniharibia na huyu eeh?aliuliza akiwa na mahasira kama mbwa mwenye kichaa..sikujibu kitu nilianza kukimbia kuelekea nyumbani huku ninalia.

Nilimhadithia baba juu ya makasa ule na kama ilivyo ada alisema jitahidi sana kumuepuka Belinda na familia yote na utaepuka mengi na kuwa na amani katika maisha yako ya shuleni na nyumbani pia.Ushauri huu niliupokea kwa mikono miwili japo ulinifanya niwe mnyonge pia.Nilihisi kutenganishwa na rafiki mzuri tu asiye na hatia wala kosa.

Nilipofika shuleni siku iliyofuata nilimweleza Belinda juu ya ushauri wa baba yangu na aliupokea pia kwa shingo upande huku tukipanga mikakati ya kumkwepa baba yake na kuendeleza urafiki wetu.


Ninasoma sasa kidato cha tatu shule ya old moshi mkoani kilimanjaro na masomo yanaenda vizuri sana.Pia hapa shuleni mimi ni kiranja wa taaluma na ninasimamia pia group la watu wanaopenda midahalo ya kiingereza.Niliobwa sana kuandaa mdahalo na shule ya jirani hasa weruweru na sikubisha,baada ya ridhaa kutoka kwa walimu tulifunga safari hadi weru weru na tulipokelewa kwa shangwe na furaha kubwa.

Baada ya mdahalo ule ambao sisi tuliibuka washindi,tuliandaliwa tafrija fupi ya chai na wali,chakula ambacho tulikihusudu sana sisi wanafunzi baada ya kula ugali wa dona kwa muda wa wiki nzima,basi wali ulikuwa muafaka mzuri wa kufanya sisi tuone kama tupo nyumbani.Tukiwa tunaendelea na maakuli,nilimuona Belinda akipita nje na nilimwita akaja tkaanza kushabikiana kwa shangwe.

Naitwa Richard,ni mtoto wa kwanza wa mzee kide.nina dada wawili na mdogo mmoja wa kiume ambaye ni mtundu sana n achakaramu wa maana tu.maana toka nimeanza kuongea hapa sikuataja hata jina langu.

Nilimuomba Belinda kama ataweza kunisubiri wakati natoka tuongee zaidi na alikubali na alikaa dukani akiwa ananisubiri.Sikutamani tena kukaa pale ndani na watu wale..akili yangu ilikuwa mbali sana ikiwaza mengi juu ya Belinda.Baada ya kama nusu saa tuliaga na kuanza kuondoka mmoja mmoja.Niliongea mengi na Belinda na kuahidiana tutakuwa tunawasiliana kwa barua na kutembeleana.

Baada ya kuandikina barua kwa muda mrefu sana na Belinda na baada ya sisi kuwa marafiki wa karibu sana,niliamua kutumia muda wangu sasa kwa masomo na kujiandaa kwa weekly test.siku moja nilikuwa chumbani na rafiki zangu tukijisomea,tulikua tunajiandaa na mtihani wa chemistry,soma ambalo kwangu ni kitendawili kikubwa sana.Basi jamaa wakiwa wamemaliza kukamua nilisikia wakipiga story za wapenzi wao na kunifanya nijione kama mtu wa zama za mawe.Basi nikabaki nimetoa macho tu a sikuweza kusoma tena.

Ah nimefeli test yenyewe na sasa ni bora nifanye lile linalonikosesha amani.niliwaza huku nikiwa naenda dukani kununua stamp na karatasi nzuri sana za kuandikia barua.Kisha niliingia libraly na kuanza kuandika barua yangu kwa mwandiko mzuri na wakupendeza.....................


...............nashukuru pia kwa barua yako nzuri na nina kitu nataka kukujulisha.Nimefeli mtihani wa chemistry sababu nilishindwa kusoma kwa ajili yako,nilikuwa nakuwaza sana sababu nimetokea kuhisi mapenzi mazito sana juu yako.Ningeomba pamoja na maumivu niliyopata juu yako na misukosuko mingi maishani mwangu,basi tuwe wapenzi na tufurahi pamoja.Hii itanisaidia mimi katika masomo yangu na tunaweza kuja kuishi mimi na wewe kama mke na mume.

....kama utaridhia basi usisite kunijulisha mapema maana nina kuwa na mawazo mengi juu yao malkia wangu akupendae daima.....Rich.

Mwezi wa pili sasa sijapata jibu wala barua toka kwa Belinda,nimejaribu kumuomba msamaha kama barua yangu ya mwanzo ilimuudhi lakini sijapata jibu hata la karatasi tupu isiyo na maandishi.

Wakati wa likizo nilirudi nyumbani na kukuta familia inahama kuelekea kigoma,baba alisema nitahamishwa shule ya karibu na kigoma ili nisiwe mbali sana na wazazi na familia.Wazo hili lilikuwa mwiba mkali sana moyoni mwangu hasaukizingatia kuwa nilikuwa na marafiki wengi shuleni na ningemkosa kabisa Belinda ambaye bado nilijipa moyo wa kumpata.

Siku mbili tatu niliulizia watu juu ya Belinda,nikaambiwa walihama na sasa wapo wilaya moja inaitwa mwanga.Nikaona huu sasa ni mkosi mkubwa na ni bora nianze kumsahau Belinda taratibu.Haikuwa kazi rahisi,utadhani alinilisha limbwata kwani alikuwa kama sala yangu wakati wa kulala na kuamka.Niliteseka sana na mwishowe nikaanza kumsahau taratibu

Nilirudi shule kumalizia ngwe ya mwisho na sikukuta barua wala karatasi iliyoandikwa jina langu kutoka kwa Belinda.Nilijua ndio mwisho naona barua yangu imemuudhi na hataki tena urafiki wetu uendelee.Sina la kufanya zaidi ya kuandaa debate ya mwisho kuniaga mzee wa ngeli....maaana pale shule waliniita mzee wa ngeli sababu nilikuwa nawapeleka sana kwa shule za mabinti zaidi yawanaume na hii kama nilivyopanga ni weruweru,basi watu walifurahi sana.

Tulipofika jambo la kwanza lilikuwa ni kumuulizia Belinda na nikaambiwa yupo tu na amejaa kibao.basi nikaitiwa na alikuja akiwa na sura tofauti kabisa na nilivyomuona mwanzo....Kaka leo najisikia vibaya sana ..ongoza mjadala huu yani tumbo linauma sana..nilimuomba msadizi wangu aongoze mjadala wakati mimi nilitumia muda ule kukaa na Belinda kusikiliza anasema nini na nini kimesibu.

Kwa aliye wahi kumuona Belinda anaweza kudhani ni binti chotara,yani labda baba yake au mama yake ni mzungu,kwani ni mweupe wastani halafu ana nywele ndefu zifikazo mgongoni.na mwanya wenye kujenga mfereji unaokaribisha ulimi kupita katikati yake na midomo mibichi saa zote.

Ana umbo namba nane..wale watu wangu wakukadiria wanajua na ana curve moja inayosema usinijuejue..yani ni kanundu fulani hivi kwa nyuma na mguu ambao niliwahi kumuona nao dada mmoja pale kariakoo akiwa na mini skirt nyekundu halafu kila mtu akapiga kelele kwa nguvu huo.Anatembea kwa kujinyonganyonga kama hataki.Macho yake kama gololi yani..shingo ndefu na mikono kama malaika...

Alianza kwa kusema najua unadhani mimi ni mtu rahisi au ulinichukulia kama nakupenda sababu ya ngono..mimi sijawahi fanya hayo mauchafu na sifanyi kitu sababu nasikia watu wanasema nikizuri ila nafanya sababu naona kinamanufaa kwangu,sidhani kama ni muda muafaka wa kuanza uhusiano na mwanaume wakati kama huu....alimaliza Belinda huku akiwa na jazba na machozi kibao yakimtoka.

Sikuwa na expirience ya mapenzi ila nilipata ushujaa wa kuweza kusema chochote....Sikiliza Belinda,sina maana mbaya niliposema nakupenda na mwanzo wa kitu kizuri chochote huwa ni mgumu sana.Naamini huelewi nini au hukuelewa nilikuwa namaana gani na ndio maana umechukia.Nilipenda tuwe zaidi ya kaka na dada..yani tushee mengi zaidi ya unavyofikiri..mapenzi sio ngono tu na kudanganyana bali mapenzi si siri kubwa kati ya wapendanao.

Unapompenda mtu kwa dhati,unatarajia mtu huyo awe na wewe wakati wote wa shida na raha.sisi bado ni vijana wadogo sana na hatujui lolote,tupendane na tuheshimiane bila kujali umri na tujenge mazingira ya familia bora ya badae...inawezekana baba yako na mama yako hawakufahamiana kwa muda mrefu na ndio maana yanatokea haya katika familia yenu.Mama yako asingependa kuolewa na mume kama baba yako kama angejua tabiayake vema.

Haya maneno yaliamsha hisia kuli sana kwa Belinda na akaanza kunielewa na ghafla bila kuamini alisema

..SAMAHANI SANA RICH ..NAKUPENDA SANA NA IMEKUJA GHAFLA SANA....alimaliza hapo na akaanza kulia na kujiona ametenda kosa kubwa sana ambalo atalijutia milele.

Nilimbembeleza sana Belinda,ingekuwa ni sehemu hakuna watu wengi basi ningemkumbatia hata kwa ubavu ubavu na kumpa busu la upendo wangu wamoto sana. Nilirudindani ukumbini nakukuta mada imepamba moto,kila mtu alishangilia na kunipa pole kwa kuugua ghafla na nilishukuru na kuanza kushusha point kama mvua.Belinda nae alikuja kuona makali yangu na hakuamini kuona naongea kama chiriku na hakuna anayepinga pionti yangu na hadi walimu walinishabukia sana.

Tukawa tunaandaikiana barua za mapenzi nyingi sana na tukawa kama wapenzi waliokutana siku nyingi.Mara nyingi shule zikifungwa huwa tunachukuliwa na mabasi sisi watu wa mikoani na si lazima kupanda basi la shule ni kwa anayependa tu.Basi nilimshawishi sana Belinda tukifunga shule tukutane moshi mjini maana nina kitu nataka kumpa na mimi nitakaa siku 2 pale maana treni yangu ya kigoma inaondoka jumamosi kwenda huko na leo ni jumanne.

Alikubali na kudanganya kwao kuwa watafunga shule ijimaa na ataondoka jumamosi kwenda kwao.Nilikuwa na kama elfu hamsini nilizojibana sana pale shuleni nikiwa na lengo la kutimiza lengo langu la kila uroda kwa mara ya kwanza na binti huyu ambaye nae hajawahi kuguswa undani wake na kidume chochote.Nilijua si kama kumsukuma mlevi bali ni kama kumchinja kobe bila kupasua nyumba yake.

Tulikutana pale stand ya mabasi ya mikoani mkoa wa kilimanjaro na nikajua hapa bila kuwa mwangalifu nitapeperusha ndege wangu.Basi nikamuomba anisindikize kcmc kule kuna rafiki yangu mkubwa anaitwa Silva naye bila hiyana akakubali.

Tukiwa tunashuka kwenye basi pale kcmc...baba yake Belinda alituona,kumbe alikuwa pale hospital akimhudumia


mwanawe mdogo aliyelazwa pale.Aliamua kutufuatilia hadi aone tunapokwenda...alifuata na sisi tulienda hadi kitengo cha macho,tukamuulizia dokta Silva tukampata ..akanivuta chemba na kusema..ee bwana mbona kama nimemuona baba yake Belinda hapa isije kuwa noma kaka..duh nikaona sasa ni mkosi mkubwa na sina budi kuingia mitini na binti wa watu kabla haijawa soo.

Tukiwa tunataka kuondoka ,mara baba yake Belinda akamwita Belinda....haya nini kimekuleta huku?halafu upo na huyo kijana niliyekukataza.Baba sikia..nimekutana na huyu kaka shuleni alikuja kunipa taarifa kwamba tunamgonjwa hapa..ndugu yake ni dokta hapa na alishafika kumuona mgonjwa wetu ..sasa tumeenda na amesema hajawaone tena inawezekana mmsesha toka.Hapa nilikuwa nataka niende kupiga simu mjini na nirudi shuleni...alimaliza Belinda aliyejibu kishujaa hadi mimi nikaona huyu kweli gaidi.

Majibu mazuri ya Belinda hayakuwa sbabu ya kumfanya baba yake awe na furaha na kukubaliana naye.Aliyapokea kwa shingo upande na kumruhusu aondoke.Dear tuwe makini huyu atatutumia hata mtu ajue mimi naenda wapi saa hizi sasa panda gari jingine na mimi nipande jingine na twende nje ya moshi kabisa.

Wazo zuri sana Belinda na panda gari nenda hadi weruweru kisha ingia shleni kabisa.Mimi nitapanda gari hadi mjini kisha nitakuja na tax ambyo ni tinted halafu tutaenda nayo hadi kia kisha pale tutapanda basi twende tukatembee arusha.Wazo zuri sana basi baadae kisha akapanda basi nakuingia mitini. Tulifika Arusha na kuanza kuzunguka huku na huko tukijua wazi sasa hakuna anayetujua na ni muda wa kula raha sasa..moyoni niliwaza mengi na nikapata story ya kuwapa jamaa shuleni tutakaporudi likizo.

Mficha uchi hazai na kama huamini ngoja uone...........Tulikuwa chumbani mimi na Belinda.Alikuwa anatoka kuoga huku akiwa mbichi ..yani sijui nisemeje hapa laikini mwili wake ulikuwa na maji bado na alibaki vile kama nusu saa hadi akakauka na wakati wote huo alikuwa mwenye aibu na mimi sikujua nini nifanye ili nianze kula mavituz.

Asubuhi yake nikiwa sikufanikiwa kufanya mavitu kutokana na nguvu alizonazo Belinda,tulitoka nje na kwenda mitaani kuzurura,huku nikiwa na matumaini ya siku ya leo kufanya japo jambo ambalo litamfanya Belinda achoke sana.Nilifikiri akitembea sana atachoka na nitamshinda nguvu kunako tano kwa sita.

Kufika sehemu Sanawari pale karibu na kituo cha mafuta,tulimkuta mzee mmoja akatuita na kusema kuna mgeni wetu yupo mjini hivyo tupande gari na kumfuata.Nilishikwa na woga sana na nikaona hii sasa ni balaa.

Tulifika eneo la tukio na kukuta hakuna mtu.Tuliandaliwa chakula kisha akaja baba yake Belinda akiwa na polisi...huyu hapa kijana naona anampango wa kuniharibia mwanangu..ni mwanafunzi huyu Belinda na anasoma shule ya sekondari weruweru.Shule imefungwa toka juzi na wanafanya starehe tu huku...alimalizia baba yake Belinda kwa hasira.

Nilichukuliwa na polisi walioonyesha wazi walipewa kitu kidogo na mzee huyu,kisha nikawekwa rumande kama siku nne bila kupewa ruhusa ya kumjulisha mtu yoyote juu ya tukio hili.Baada ya siku ile ya nne ndipo alikuja mzze mmoja ambaye anaonekana kuwa na busara kisha akasema mtoeni kijana aende zake kwao.Walinionya sana na kunipiga fimbo kama tano hivi uchi kisha nikaenda zangu kituo cha basi na kupanda gari hadi dar.

Niliendelea kumuwaza sana Belinda japo mapenzi yake sukuyaonja,nilifikiri mengi na kuona kama nimemkosea Mungu kitu.kwanini namlazimisha Mungu kufanya haya yote?nilijiuliza nikiwa kwenye treni kuelekea kigoma nyumbani.

Nilifika kigoma na sikutaka kumjulisha yoyote juu ya yaliyonipata maana nilijua ningezua mambo mengine ambayo yangeleta mzozo mkubwa wakati yalikuwa ni makosa yangu.Likizo ilipoisha mzee wangu alinifungashia kila kitu na kurudi shuleni.

Sikutaka mtu pale shuleni ajue mambo yangu...Nilimuandikia barua Belinda na akajibu kuwa siku ile alipigwa sana na baba yake na akaonywa iwapo itaonekana na mimi tena,basi atafukuzwa nyumbani.Nilikaza buti sana kwenye masomo nikiwa nawasiliana na Belinda kwa barua tu.

Siku ya kumaliza shule ilifika na wazazi wengi walikuja.mimi hakuna aliyekuja hata mmoja na nilikuwa na hasira na ndugu zangu na wazazi.Haisaidii sana kuwachukia kaka wewe shukuru umemaliza shule na unaenda sasa kusubiri matokeo yako.Alisema mtoto mmoja wa kidato cha pili ambaye wakati wote alikuwa sambamba na mimi kunifariji.

Mida ya saa kumi na moja jioni alitokea Belinda akiwa na wenzake kama sita.Mkononi alikuwa na zawadi ambapo yue kijana wa kidato cha pili niliyekuwa nae,alikuwa amenipa zawadi ila sikuifungua.Kaka nlileta zawadi hii kukufichia aibu maana nilijua hakuna atakayekupa zawadi na nikafanya shauri hili la kufunga huu mzigo mkubwa utakao kufanya unikumbuke milele.

Fungua mpenzi zawadi tuone ..alisema Belinda huku yule kijana akiangua kicheko kikubwa sana..basi nikachukua lile box lake na kufungua ....hahahahahahaaaaaaaaa shabashhhhhhh...asante sana kaka yangu..lilikuwa ni jiwe dogo na majani ya mpapai..sikuwa na pesa ya kununua kitu chochote kaka na pokea hiyo kama kifuta aibu na nikumbuke sana kaka yangu mpendwa...alimaliza kijana huyo kisha akacheka tena na wote tulicheka sana.


Belinda aliniletea kamera digital na suruali ya jeans,....graduu yangu tarehe 27 Rich..sijui utakuwepo bado?aliuliza Belinda huku akiwa na haiba ya kujua nini nitasema.Mfukoni sikuwa na hata nauli yakwenda kigoma na nilikuwa nasubiri pesa toka kwa dingi maana aliahidi ningepata fedha kwaajili ya graduu pia.

Tuombe Mungu Belinda hakuna linaloshindikana mpenzi..nilimjibu kisha tukakumbatiana na kukumbushana story za Arusha na maisha yetu kwa ujumla. Baada ya kumaliza shule nilirudi Kigoma na kukaa tu nyumbani..maisha yalikuwa tofauti sana kwani nilikaa sana nyumbani bila hata kuwa na pesa ya mfukoni.Baba hakunipa pesa ya kuhongea wadada hivyo nikaanza kufanya kazi za ualimu bubu kwa kufundisha wadogo zangu wa kidato cha tatu na cha nne.Kama baada ya miezi mitano nilipata kama laki tatu hivi na kuaga nyumbani kwamba naenda Dar kutafuta shule ya kufundisha.


Nilienda hadi kwa Belinda na alikuwa anabanwa sana kwao.Japo nilifika hadi mtaani kwao lakini alipata taarifa na kusema asingeweza kufika popote maana baba yake alikuwa nyumbani muda wote kwani alikuwa mgonjwa wa maralia.

Niliona ni mkosi mkubwa sana,nikaamua kununua simu ya mkononi ili niwe angalau nawasiliana nae Belinda kupitia simu yao ya ndani.Nani wewe unaongea,?ilikuwa ni sauti ya mama yake Belinda..nikajibu hapo ni kwa mzee Rashid?..hapana naona ni wrong number..kisha nikakata.

Idadi ya wrong numba ilimshitua baba Belinda kwani kila nilipopiga ili nimwambie Belinda kwamba nina simu ya mkononi alipokea mama yake au Baba yake.Atafutae hachoki na akichoka basi ujue kapata.Ndivyo nilivyoendelea kusema huku nikiwa najipa moyo kwamba siku moja nitafanikisha azma yangu ya kumpata Belinda tena awe wangu wa milele.

Maisha yaliendelea hivyo na nikawa najaribu bila kuchoka kumpigia simu Belinda hadi siku moja akapokea ..nadhani siku hiyo alikuwa peke yake kwao..ni mimi mzee wa wrong number nilisema kisha tukacheka sana.Wangejua hawa mabedui kama ni wewe naona wangekata kabisa nyaya za simu...alisema Belinda.

Haya ni mambo ya kizamani sana Belinda maana wangejua wanakuzuia lakini bado tunawasiliana,kweli kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.We ngoja tu dawa yao ipo jikoni na inachemka..nitaipika taratibu tu na watainywa..alisema Belinda huku akionyesha hasira kwa kufugwa ndani kama mnyama.

Poa basi namba yangu ni hiyo na ukipata mwanya nitumie hata sms na nitakupigia simu ... ReWiNdddddd

Ilipita kama miezi miwili bila mimi kuonana na Belinda.Siku moja alijaribu kutoroka na alifanikiwa kuingia mitini akiwa na uhakika baba yake hamuoni.Alifika hadi mjini na kunipigia simu..upo wapi mpenzi?leo nimetoroka nyumbani yani nina hamu sana na wewe.Upo wapi nije mara moja jamani?aliuliza Belinda huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana.

Upo wapi nije mimi Belinda...nilimuuliza na aksema yupo uwanja wa sabasaba kuna restaurant inaitwa majeshi.Mimi sikungoja nini wala nini nikachukua Tax hadi sabasaba na kumkuta Belinda.Alikuwa amenenpa sana na uzuri ulizidi maradufu.Tukakumbatiana na kubusiana mara kama saba hivi.Kisha nikamwambia tuende mahali ambapo hataonekana na watu wanaomfahamu.

Tulienda hadi sehemu moja ambapo kuna nyumba ya wageni kisha nikamwambia Belinda aingie ndani ....tunaenda kuongea tu Belinda hatuta kaa muda mrefu na utarudi nyumbani.Alikubali kuingia na tukawa tunaongea hili na lile..kisha nikaanza kumshiashika hapa na pale nikaona anaanza kuomba maji ya kunywa mara analia mara anasema hili na lile.

Nilimshikashika taratiiiibu na kumgeuza huku na kule,kisha nikaanza kumtoa t-shirt yake aliyovaa na kumpendeza sana.Muda haukutusubiri kwani ulienda kama umeme vile.Mwishoni nikampa maji ya kunywa na alikuwa hajiwezi kwa kuanza kuhisi muwasho wa mapenzi mazito kwenye wake mwili wamoto sana.

Tuliendelea kushikana hadi ikafika muda akasahau kabisa ya nyumbani kwao.Ukali wa baba yake ukamtoka akilini na tukawa wote kama tuliopigwa na shoti ya mapenzi kwani woga ulimtoka nikampa dawa ya mapenzi ambayo ilimfanya alegee zaidi.(ukitaka dawa hiyo njoo kwangu ukiwa mgumu mwenyewe utalegea tu).

Taratibu nikaanza kumvua sketi yake na akawa hana ubishi sana na nikamvua na kufuli lake.Kuchaki chinimashalah alikuwa tayari hoi akisubiri tiba ya maisha yake ya kijima,nasema yakijima kwanialikuwa hamjui mwanaume hadi wakati ule.Nikaanza kuhema kama pwagu na pwaguzi.Nikahangaika hadi kufanikiwa kuingia kwenye hekalu lake alitunzalo kama lulu.Ila kuingia tu mzee nikashusha na zege kuuuubwa lililompa hamu zaidi ya mapenzi.

Alipata maumivu makali yaliyomfanya ashindwe kutembea..sasa Richard mie siwezi hata kunyanyua miguu yani.maumivu makali sana napata hapa,lakini asante sana maana sasa woga umetoka na wewe ndie ulienitoa usichana wangu.Ya nyumbani niachie mie maana huyo idi amini sasa anajua nipo kuzimu sijui?alisema Belinda huku akiwa na nusu hofu.Maadam sina tena usichana,na alieutoa ni mwanaume nimpendae,basi liwalo na liwe.

Saa 4 usiku bado nipo na Belinda na hatujuia itakuwaje,anataka kwenda kwao lakini maumivu apatayo ni makali sana na hawezi hata kutembea.Mimi naona ubaki hapa hadi utakapokuwa fresh maana ukifika home saa hizi utasema nini


sasa?na watajua tu ulikuwa na mwanaume sehemu na mama yako kama ni mjanja atajua mapema sana....nilimpa ushauri na yeye muda wote alikuwa ameinama anatunga sheria.

Ya,nitabaki hapa Rich,nitaenda home kesho kama mambo yatakuwa mazuri.Tulienda kuoga na kurudi pale chumbani,nikatoka na kwenda kutafuta kitu cha kula kisha nikaja na chips myai kuku.

Asubuhi tuliamka na Belinda akataka tufanye tena ..yaani tule tunda maana jana hakupata full raha.Tulikula tunda tena bila hata zana au mifuko ya rambo.Ikafika saa nne asubuhi huku wote tukiwa hoi.Sasa tupange inakuaje Belinda,niliuliza huku nikitamani hata aseme anabaki kwa siku nyingine.


Mimi siendi bwana nyumbani.ataniua yule mzee,na akijua nilikuwa na wewe ndio itakuwa balaa kabisaa.sijui tufanyaje?aliuliza Belinda huku nikiwa na wazo jipya kichwani.

Tumpigie simu tumwambie unaumwa ila kabla tutafute daktari pale hospitali ya wilaya akikubali tucheze deal hili.Nilienda hadi hospitali ya wilaya na kumkuta dokta mmoja kijana na nikamsomesha somo hili lakini akasema ni vigumu.Ila alinipa ushauri mzuri tu wa kufanya na kuliepuka noma hili ambalo kadiri muda unavyokwenda ndio soo linazidi kuwa kubwa.

Ok,nashukuru sana bro..nilimwambia kisha tukabadilishana namba za simu.Nilirudi hadi pale tulipolala kwenye nyumba ya wageni na kukuta mhudumu akizozana na Belinda.Muda wa kulala umepita kama mnakaa siku ya pili mnaruhusiwa kubaki kama hamkai basi ondokeni...alisema mhudumu huyu kwa jazba.

Sie hapa ni wageni mama kwahiyo hakuna ruhusa ya kutufukuza.Kwanza si ustaarabu huo unaofanya ebo..nilimjibu huku nikiwa na risiti nikamwonyesha akaona aibu sana.

Nimeenda kule mpenzi na nikampata dokta mmoja ambaye ni kijana na akasema itakuwa ngumu sana kupanga

suala la kusema wewe ni mgonjwa toka jana.Ila tunaweza kufanya hivi....

Piga simu kwa mama yako mwambie hurudi nyumbani hadi baba yakoaache tabia yake ya kunywa pombe na kuwapiga.Halafu pia aache tabia ya kukuchunga kama mnyama na akileta ubishi basi hatakuona tena kwani upo porini na unataka kujiua.

Lilikuwa wazo linalotisha lakini tukakubaliana tulitumia na likafanya kazi kwani mama Belinda alimwambia mumewe na mimi nikapiga simu kama mpita njia kule porini nakusema ..Binti yao ni mnyonge sana..inaelekea hajakula chakula kama siku tatu hivi hivyo mnatakiwa kuja kumchukua maana pia ameweka kitanzi tayari shingoni.

Ulikua ni ujumbe uliomfanya Baba yake Belinda anipigie simu mara moja na kusema kama anaweza kuongea na mwanae..yupo hapa ila mnyonge sana na amesema nikimkaribia tu anajinyonga.sasa ni vema nimpe simu uongee nae.

Belinda aliongea na baba yake na kumpa vitisho vikali kisha akakata simu..alipiga sana baba yake bila mafanikio.KIsha alipiga tena baadae nikamwambia tayari nimeenda polisi na wapo eneo la tukio na nilazima watamuweka polisi kama atakuja kwani kuna ushahidi kwamba alimfukuza mwanae akiwa amelewa pombe na kumpiga sana.

Ushindi huu si tu ulifanya Belinda awe huru,bali ulifanya pia mimi nipate mwanya wa kumtumia Belinda kila nitakapo.Alianza kuja kwangu mara nyingi na tukawa kama mke na mume.tofauti ni kuwa hakulala pale ghetto usiku mzima ila alikuja mara nyingi na tulianza kufurahia mapenzi yetu. Belinda alimaliza masomo yake na kujiunga na chuo cha usafirishaji pale dar es salaam,na akaajiriwa na kampuni ya clearing na forwardind hapo hapo dar es salaam.

Mimi ni mwajiriwa wa Freshwap .Maisha yanaenda tu na niliamua kufunga safari hadi kwa wazazi wa Belinda na kuwapa taarifa kuwa nataka kumuoa binti yao.

Haikuwa rahisi kwa baba yake Belinda kuamini kwamba ni mimi niliekuwa kama kinyesi mbele ya macho yake ndie nataka kuwa mkwe wake.


Aliomba radhi sana na kunipa ruksa ya kumuoa Belinda ambaye wakati wote huu alikuwa Dar bado kikazi.Mipango ilipangwa na mwishoni wazazi hawa waliokuwa maadui tuliwaunganisha na mzee wangu alishangaakuona siku ya harusi yetu baba Belinda hagusi pombe.

Baada ya ndoa yetu tuliwakalisha wazee wote na kuwahadithia mkasa mzima wa mapenzi yetu na siku ile tulivyocheza ile deal ya kufa mtu.Walibaki wanacheka sana na mimi nikasema kwaherini wazee mimi naondoka na BELINDA WANGU PEKE YANGU KWENDA KULA TUNDA......
 
Hivi umemwomba Bellinda hilo jina msije mkakosana na Masa hivi hivi.
 
hahahahah!....Belinda come out come out wherever you are.....alafu naona shem my wifi wangu amepotea sana umempiga beat nini asiiingie humu siku hizi?...

Yuko busy na mambo fulani shem! si unajua 2010 haiko mbali....hahahah
 
Aaaa babu, fungate unaenda Saudia????? joto lote hilo? huta enjoy tunda, unatakiwa uende mahali penye minus degree afu to keep warm hamuwashi hata heater, ni kitu juu ya kitu, mkiwa mmejifunga mataulo yenu tu, kamvinyo kwa pembeni na kamziki kwa mbaaaaaali.
 
si atunge kitabu?, maana nimeSCOLL mpaka basi, duh.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom