Kaka hapa umedanganya umma. Ingawa ni kweli kwamba Zantel hawatumii 3G kama Voda na Zain, bado ni kweli kwamba Zantel na Ttcl wanatumia system moja. Kwa kuwaengua TTCL hapo hujawatendea haki. Fuatilia kama nasema uongo!
Namuunga mkono thinkpad 100% Ukiangalia kwa umakini ni hivi Zantel 10GB ni Tsh 270,000/= yaani hiyo ni 27sh kwa 1MB
alafu speed ni kubwa kuliko ya mitandao yoote iliyo TZ yaani vodacom, TTCL, Sasatel, Zain, tiGO, Tritel, BOL hili halina ubishi.
Kingine kuhusu 3G kuwa expensive duniani zantel sio 3G voda na zain ndio 3G zantel wana system ambayo mitandao yoote nchini hawana hivyo Zantel wako vyema na hawaitaji faida kubwa kulinganisha na mitandao mingine nyonyaji ambayo tulipaswa kuisusia kwa umoja mpaka pale watakapoona kuwa sivyema kutengeneza faida kubwa.
Ni kweli kabisa mkuu... nataka sana kuchukua Zantel, tatizo linakuja kwenye coverage... kule kimanzichana, kibwegere, amani beach, kisota nk. ntapata reception?? Nilijaribu kuuliza wale jamaa wakasema ngoja wacheki lakini naona kimya
ila nimeumia sana mkuu na Voda, namshukuru sana ThinkPad maana huwa anatukumbusha sana kuhusu haya mambo
Nyie manazi wa Zantel acheni kupotosha watu. Zantel ni kama Clouds FM. Huwezi kulinganisha na redio inayosikika nchi nzima.
With holistic approach, TTCL is the only internet provider that is cheap.
Nakushangaa sana mkuu maana mimi napata ttcl broadband package ya 1GB kwa 30,000= sasa who is cheaper?zantel its 120Tsh per MB so its cheap, TTCL they should be a little bit smart, to take a customer from its current supplier you need to come with a package a bit lower and with zantel that 120Tsh per MB is if your not on special package, the special package you get 200MB for 10,000Tshs or 1GB for 40,000Tshs! i think TTCL had their work cut out themselves, i wont leave my zantel until i get cheaper than that!
Nakushangaa sana mkuu maana mimi napata ttcl broadband package ya 1GB kwa 30,000= sasa who is cheaper?
Kuna watu humu kazi yao ni kuleta ubishi tu!! haya fungua hiyo link ya TTCL kisha ndio uongee nasiokuongea tu ilimradi unaweza kuongea
click hapa: http://www.ttcl.co.tz/EVDO.asp
kisha fungua hii ya Zantel hapa:http://www.zantel.co.tz/cdma.html
maana watu wengine huwa ni wagumu kuelewa na kwa hili usipo nielewa basi hautaelewa kamwe.
Sasa mkuu tuamini maneno yako au tuamini kilekinachosemwa na TTCL wenyewe? Link hizo hapo chini Fungua uone kisha ubishe maana hauwezi kusema ttcl cheaper wakati gharama zao ziko juu na ushaahidi ni ktk website yao kwanini utetee TTCL wakati wao wanaweza kujitetea kwakushusha bei?
Fungua hizo link kisha linganisha bei zao zote tukiacha speed maana speed ya Zantel iko juu linganisha bei tu!
Mkuu MTM, si bora ukachukua hata Zantel 3GB kwa Tshs 86,000/= kuliko hiyo 2GB kwa 100,000/=? Anyway, isijekuwa nawaharibia watu biashara. Kupanga ni kuchagua! Zantel 10GB ni 270,000/= (Post paid) na hapo maanake unakuwa unalipia 27/= per MB.
Think of it bro!
nikweli!, lakini speed yao ni kichef-chef, jaribu Zantel mkuu utafurahi.Asanteni kwa kuhabarishana kuhusu hizo gharama za data charges za TTCL na Zantel. Hongereni mnaoishi mijini lakini kwetu tunaoishi vijijini tuandike maumivu. Mimi nafanya kazi kwenye mashirika ya UN yanayohudumia wakimbizi huku Kigoma yaani Kambi ya Nyarugusu ambako Tigo ni ya manati, Voda ya kubabaisha, Zantel ni kama Voda ila kwa sababu wanatumia portal ya Vodacom hawatoi huduma za mtandao kwa mkoa huu. Ila nina bahati moja kubwa hapa ninapofanyiakazi na kuishi ni karibu na mnara wa Zain uliopo kijiji cha Makere kwa hiyo ndiyo tandao wenye nguvu. Ninazomodem mbili yaani ya Voda na Zain ila nimeshindwa kabisa kuiumia ya Voda kutokana na signals kuwa very weak.
Kwangu mimi the cheapest network as far as data packages are concerned is Zain. Wao wana package ya MB 400 kwa Tsh 2,500/= kwa mwezi ambayo unaweza kui- "refresh" kila inapoisha. Je hamwoni hiyo ndiyo the cheapest of all. Kuhusu speed mi naona haina shida maana naitumia kubrowse kila siku na muda wote, kusikiliza Radio Maria, BBC, VOA bila shida na hata ku "chat" . Ila nimevutiwa sana na experience ya wenzangu juu ya speed ya Zantel na TTCL. nawasihi Zantel waukumbuke pia mkoa huu wa Kigoma unaoonekana kusahaulika katika kila nyanja. Kuhusu gharama za data za Vodacom ziko juu mno tofauti kabisa na wenzao Zain. Nawashauri wafikirie kupunguza data charges zilingane na za wenzao wa Zain maana hata jamaa zangu wanaoishi Kasulu na Kibondo mjini (Wilayani) na maeneo yaliyo karibu na minara yao lakini wameamua kubadilisha na sasa wanatumia hii ya Zain.