Baada ya D9 kuanza kwa kusuasua kutokana na vigingi vizito toka kwa watawala , kumeibuka kebehii za wazi wazi toka kwa machawa wa mfumo kuelekea kwa Gen z.!
Ila wasichokijua machawa fukara ambao wengi ni manyumbu katika sekta za umma. " nikwamba , athari za haya mambo hazitoangalia itikadi za vyama, wala msimamo wako juu ya serikali" .Wote tunaenda kuimba wimbo mmoja. Tusije kusikia mnatoa milio ya kero za makato ya mishahara, huduma za kifedha n.k..
Mdogomdogo acheni sasa tuonyeshane makali
Sio lazima wote kuwaamini katika maandamano na vurugugu ila inawezekana wengi wanaamni katika mabadiliko tatizo ni njia mliyochagua kuyapata hayo mabadiliko... Kwa akili zangu timamu siwezi kupambania mageuzi/mabadiliko kupitia wanaharakati kama Mange au wanasiasa kama Heche mana wote ni waganga njaa tu na wanatafuta ajira kupitia migongo yetu
Waonesheni watanzania.
1. Malengo mahususi ya wanachokipanbania (yapo na yanaoneka).
2. Onyesheni njia salama za kudai mabadiliko bila kuathiri uchumi, mali, maisha ya mtu binafsi.
3. Nani kiingozi wetu na taswira yake kwenye jamii ikoje. Hapa tumieni watu wanaoweza kujenga hoja na wanaheshimika sio kina Mange.
4. Target ni nani Samia, CCM, katiba, uchaguzi au Serikali mana serikali ni pana sanaa na sio raisi tu.
5. Hoja ya JESHI kuongoza nchi wenye akili timamu hawawezi kuikubali hata kama ni kwa mpito.
6. Kitendo cha kuanza kushitaki jumuia za kimataifa, kuchongeana kipuuzi na kususiasusia baadhi ya mambo/watu kimeosha kwamba wote ni watoto na hamjui mnachokipigania.
7. Mmewaogopesha wengi kwa kushindwa kuhimili mawazo mbadala na baadhi ya viongozi wenu kublok watu wenye mawazo mbadala. Kama unadai haki na demokrasia na huwezi kuhimili mawazo mbadala unatofauti gani na unaetaka kumtoa??? Matusi, kejeli na dharau kutoka kwenu vimewatoa wengi kwenye kundi la mapambano.
8. Kitendo cha D9 kupita bila kiongozi)muhamasiahaji yeyote kukamatwa au kutoka kinamaanisha walitaka kuwatumia watu kwa manufaa yao.
9. Hamjui manachokipambania malengo yamekua yakibalika kulingana na matukio... Mnaandamana mnaimba wimbo wa Taifa mnabariki viongozi mnaowakataa, mnadai kupewa miili ya wapendwa wenu mkishindwa mnakimbilia kwenye kuathiri uchumi, mnadai katiba mkibanwa mnakimbilia uzanzibar nk.
Tchao.