Wosia wa Mwl. Nyerere - Mimi ninang'atuka na siasa ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wosia wa Mwl. Nyerere - Mimi ninang'atuka na siasa ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNgumu, Nov 24, 2011.

 1. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukijaribu kufikiria upya maneno ya Mwl Nyerere 'Mmi ninang'atuka lakin bila CCM madhubuti nchi itayumba' Maswali mengi yanajitokeza.

  Kwa mfano nini alikusudia Mwl kwa neno CCM madhubuti? Ndio hii CCM tulionayo au nyingine? Je alikusudia chama chochote madhubuti au lazima CCM. Je manono yake bado yanafanya kazi ktk wakati tulionao na maswali mengine mengi.

  Tujaribu kuchukua wakati kidogo kuyatathmini maneno ya Mwl upya na tutoe maoni yetu kwa maslahi ya taifa letu.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa, unajuwa maana ya Kung'atuka? fikiri uje na jibu sahihi na si la kubabaisha.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwalimu pia aliwaachia CCM angalizo: kama CCM itashindwa kutoa uongozi bora wananchi watautafuta kwingineko.
   
 4. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Siku nyingine subiri kwanza umalize menstruation period ndio uanze kutoa comments zako jamvini. Yaani katika text yote umeona neno kung'atuka tu?

   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nadhani Faiza kapata jibu linalompasa.
   
 6. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,056
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Oh wow!
   
 7. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kung'atuka kwa uelewa wangu mdogo kunachukua muelekeo wa mtu kulazimika kuacha kitu fulani bila ya hiari yake pengine mazingira yamemfanya achukue uamuzi huo. Sina uhakika kwa asilimia 100 kua Mwl alitumia neno hilo kwa mantiki hiyo possibly.
  Ambacho nilikikusudia sana ni kutathmini maneno ya Mwl kwa ujumla na ukweli wake ktk wakati tulionao na sio neno mojamoja na ninadhani kua maneno ya Mwl kwa ujumla yanaeleweka no matter kung'tuka itakua na maana gani.

  Naomba mchango wako sister au kama ni brother please. Thanks.
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi nashangaa hawa wanaohangaika na kile kibabu. nchi ilimshinda karibu kila nyanja, afya, elimu, etc. kaliweza kudhibiti rushwa tu na kulinda rasilimali zetu. The rest was zero.
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wengi hawaelewi maana ya kung'atuka. aka ni vilaza wa neno hili
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Kung'atuka=kuachia ngazi kwa hiyari yako mwenyewe pasipo kuwa na external forces(pressure) kutoka nje

  Kujiuzulu=Ni kama alivyofanya EL kunakua na pressure kutoka nje

  Kustaafu=Kuachia ngazi kisheria mda umetimia
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Tafadhali fanya heshima, hiyo si kauli njema, mama yako kamaliza? au wewe hukuzaliwa na mwanamke?
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kujuwa maana ya kung'atuka ni rahisi sana, kwanza ujuwe "kung'ata" kama umesha juwa kung'ata ni nini basi ujuwe Nyerere alitung'ata na baada ya kuona hii mijitu hata unapoing'ata yenyewe bado tu ipo "ndiyo baaaba" akachoka kung'ata, unaing'ata mijitu kwa miaka zaidi ya ishirini yenyewe ipo tu, inakenuwa meno kama vile hawana hisia za kung'atwa, baada ya taya kumuuma aka "ng'atuka". Alikuwa hana jipya jingine taabani kwa kun'gata.

  Kung'ata = Kuuma kwa kutumia meno.
  Kung'atuka = Kuwachia kuuma kwa kutumia meno.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Nini maana yake? Ninachojua mimi Nyerere angeweza kuwa kama Mobutu, Moi, au viongozi wengi wa west africa ambao kwao madaraka ilikuwa ni haki yao ya kuzaliwa. Aliamua kukaa pembeni kwa hoja, sio viroja. Kwa hilo ninamsifu sana.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hii nayo kali,lol!!
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kitu ninachoweza kukubaliana na wewe FF ni kuwa, wakati tunasheherekea miaka hamsini ya uhuru, lazima waswahili tujisifu kwa kuweza kucheza na maneno ya kiswahili jinsi tunavyotaka. Na tusiishie hapo tu...tujipongeze kwa kuendelea kujenga kwa kasi zaidi taifa la kiswahili linaloitwa Tanzania, lol!!
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana. Chimbuko la neno kung'atuka si kung'ata. Neno kung'ata halimo katika lugha ya Kizanaki. Hicho ni Kiswahili cha Gerezani.
  Neno kung'atuka asili yake ni Uzanakini maana yake ikiwa ni kuondoka kwenye kiti. Nakumbuka tulipokuwa wadogo wageni wakija nyumbani kama bado umekalia hicho kiti badala ya kumpisha mgeni unaambiwa na mzazi wako "ng'atuka". Torokyo mufwano.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Jasusi,
  Kuna watu wanajua kila kitu hata yale wasioyajua....we are on the road to create powerful swahili nation kwa mtiririko huu wa mambo.
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Mlikuwa mnaving'ata viti kwa mananihii?

  Hilo neno ukitaka usitake asili ya maana yake ndio hiyo, linatokana na kung'ata, halafu huko kwa kina Nyerere si unajuwa meno wanayafanya nini? wee kwa kung'ata yale aking'atuka lazima ubaki na majeraha sio ya kawaida.

  Ng'ata, ng'atana, ng'atuka, ng'ang'ania. Huwezi kung'atuka ikiwa hujang'ang'ania. Na ndio maana hao wazee walikuwa wanawaambia "ng'atuka" kwa kuwa hata mnapoona watu wazima nyie bado mmeng'ang'ania kung'ata kwa mananihii hivyo viti, wazee hawajakosea walipokuwa wakiwaambia hivyo.
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Hakuna lugha duniani inayokuwa bila kuongezea maneno mapya yanayotokana na misemo na matamshi ya lugha zingine. Kiswahili kimejumuisha maneno mengi sana kutoka lugha tofauti duniani na nchini kwa wingi wake au kwa uchache wake. Usishangae kuona Wazanaki wana maneno au matamshi yaliyoingia katika kiswahili na usishangae ukakuta maneno au matamshi ya lugha zingine yapo kwenye Kizanaki. Funguka.

  Nasikia wahaya wanaongoza kwa kuingiza maneno au matamshi ya Kiingereza kwenye lugha zao mpaka sasa yamekuwa ni kihaya, sina uhakika kama ni "joke" tu kwa Wahaya au ni ukweli, nimesikia tu siku hizi Kagera watu wanaongea sana Hanglish. Kama vile masharobaro wa Dar wanavyoongea Swanglish.

  Hilo nililokuwekea nyekundu, hapana, si hivyo bali kuna watu wana uelewa mpana sana na wanayajuwa mengi kuliko wengine. Hizo ni rehma zake Mwenyeezi Mungu.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bibie,
  Nakwambiaje? Katika lugha yetu hatuna neno ng'ata kwa maana ya kuuma. Kuuma ni kuuma tu. Ukishaelewa hivyo ndipo utaweza kuelewa kwamba hakuna uhusiano baina ya maneno hayo mawili. Ng'ata ni kuuma kwa meno. Lakini kung'atuka ni neno la Kizanaki ambalo maana yake ni kuondoka kwenye kiti (specific). Kwa mfano huwezi kulitumia neno hilo kwa mtu anayetoka kitandani. Ni mahususi tu juu ya kiti. Na ndiyo maana limeingizwa katika kamusi ya Kiswahili likiwa na maana ya kuondoka kwa hiari kutoka nafasi ya uongozi ( Kamusi ya Kiswahili Sanifu, toleo la pili, ukurasa wa 306)
   
Loading...