Kuna fununu kuwa Balali alifanya mahojiano na Tanzania Daima mwaka jana huko US.Tanzania Daima walikuwa tayari kuyaprint,wakaingiliwa na UWT...wakachimbwa mkwara mzito sana na matokeo yake it has gone mum till today.Lakini inasemekana ipo na kuna siku itaibuka tu.
Wanaendelea kutuzingua tu, si watoe huo waraka?
Kama waraka huo upo kweli naamini Mbowe ni mmoja kati ya watu walio nao.
CHADEMA mna kazi kweli na huyu mheshimiwa maana ni ngumu sana kwake kutofautisha mambo ya chama na familia. Mimi naamini hiyo ndio weakness kubwa ya Mbowe.
Hii mambo ya EPA na Ballali angewaachia CCM wajimalize wenyewe na Dr. Slaa akiwa upande wa sisi wanyonge.
Najiuliza hivi spinning yote hii ya nini? Kama waraka upo, basi utoeni vinginevyo kaeni kimya kama mlivyokaa kimya wakati Ballali alipokuwepo.
Story nzima hii haimweki Ballali vizuri maana kukaa miezi tisa na siri nzito na kusubiri mpaka afe ndio itoke ni cowardice ya hali ya juu mno.
Laiti angewakabili mafisadi, Ballali angelikufa kama shujaa wa Watanzania, lakini sasa kazidiwa hata na vijana kama akina Zitto wakati yeye alikuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutusaidia kuitengeneza Tanzania yetu.
Kibaya eti anawaachia siri watu kama akina Mkono, hivi kweli Ballali alikuwa anasoma alama za nyakati?
Mimi ninashindwa kushangaa maana hii imezidi kiasi!
Hatimaye sasa imethibitishwa kuwa ni kweli Mkono, alikuwepo US katika kipindi fulani mwezi wa April, kwa sababu kuna mpaka interview ninayo sasa aliyoitoa kwa gazeti moja nchini kuhusu malipo yake aliyolipwa na BOT ya shillingi Billioni 7.9, aliifanya hiyo interview akiwa US, hii ni kubainisha habari kuwa alikwenda na kukutana na Marehemu kwa masaa karibu 24, ambako inasadikiwa alimkabidhi mikoba yote muhimu ya uporaji wa mapesa yetu wananchi, pole pole tutawafikia tu wote watinge kwenye sheria ya wananchi!
Huu mchezo ndio kwanza umeanza!
Waraka huo ambao kwa sasa unatafutwa kwa udi na uvumba unadhihirisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Serikali
Mtanzania,
sidhani kama ni sahihi kusema Balali alikuwa coward,tukumbuke kuwa yeye hakuwa na moyo wa chuma,na ikizingatiwa kuwa alikuwa amezungukwa na mbwa mwitu kila kona waliotaka nyama hapo BoT na mabo baada ya kula nyama wasingekubali kuona akiwa huru.Hata ingekuwa wewe sidhani ungekuwa na ujasiri wa kupambana,kwangu mimi ni nafuu ameacha maandishi ambayo angalau yatatupatia...tusimfanye Balali kuwa exceptional human being ambaye hatishiki na umafia na ujambazi wa mafisadi jamani,kuna wangapi ambao wameshindwa kuacha hata maandishi tu?Cha muhimu tusubiri hizo documents...
that said I can guess nani anaweza kuwa miongoni mwa wanasiasa wawili wenye ushawishi waliomlazimisha Balali kutoa hizo pesa ambao hawatajwi katika EPA,Kingunge Ngombale Mwiru lazima yumo tu maana anajulikana kwa umafia wake.
Kuna fununu kuwa Balali alifanya mahojiano na Tanzania Daima mwaka jana huko US.Tanzania Daima walikuwa tayari kuyaprint,wakaingiliwa na UWT...wakachimbwa mkwara mzito sana na matokeo yake it has gone mum till today.Lakini inasemekana ipo na kuna siku itaibuka tu.
Ilikuwaje Tanzania Daima wakaenda UWT kuomba ruhusa ya ku print mahojiano na Ballali?
Tunaomba maelezo ya uhusiano wa Ballali, UWT, Tanzania Daima na mpangilio mzima wa gazeti kukiambia chombo kingine nje ya chumba cha habari: tuko na news story hapa tunataka kuichapisha!