Wosia wa Ballali kuwaumbua wengi!

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
157
Dk. Ballali kuumbua vigogo

  • Wosia wake wataja walioshinikiza EPA
  • Wanasiasa, wanasheria wauhifadhi
Mwandishi Wetu Mei 21, 2008

KIFO cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Timoth Said Ballali (65) kinazidi kuibua mambo mengi, sasa waliokuwa karibu naye wanataka undani wa wosia aliouandika kwa mkono wake na maelezo aliyoandika alipohojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuondoka nchini kwenda Marekani, uanikwe.

Watu mbalimbali walio karibu na familia ya Ballali, wakiwamo wanasiasa na wanasheria, waliozungumza na Raia Mwema wiki hii, wamesema ni wakati mwafaka kwa sasa mambo yote aliyoyaacha gavana huyo wa zamani yawekwe wazi ili kuondoa utata kwamba kuna jambo linalofichwa.

Wakati hayo yakiendelea, habari zinasema kwamba kuna mkakati maalumu wa kuhakikisha kwamba siri ya waraka huo haitolewi hadharani na baadhi ya watu mashuhuri wamethubutu kusafiri hadi nchini Marekani kufanikisha mkakati huo bila kujua mengi zaidi yapo nyumbani Tanzania.

Akizungumza na Raia Mwema wiki hii, mwanasheria mmoja mashuhuri amesema anafahamu na ameuona waraka aliouandika Ballali kwa mkono wake akielezea mambo mengi ya msingi aliyotuhumiwa nayo ikiwamo lile sakata la fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) uliokuwa ukisimamiwa na BoT, ambako zaidi ya Sh. bilioni 133 zinadaiwa kupotea.

“Ballali aliandika kwa mkono bila kupigwa chapa mambo yote yaliyotokea ambayo anatuhumiwa kuyafanya kama mhalifu na amewataja watu wote kwa majina na muda bila kuacha katika waraka wake huo ambao ameweka saini na kuhitimisha kwa alama za vidole,” anasema mwanasheria huyo ambaye hajawahi kutajwa popote kuwa na mahusiano na Ballali wala BoT.

Maelezo ya mwanasheria huyo yameshabihiana karibu kwa kila kitu na Mbunge mmoja wa Upinzani ambaye pia ni mmoja wa viongozi muhimu katika kambi ya upinzani ambaye naye amekiri kuuona waraka. Mwanasiasa huyo hakukiri wala kukanusha kuwa na nakala ya waraka huo wa Ballali.

Wote wawili wanasema kwamba waraka huo unaweza ama uko mikononi mwa watu zaidi ya watano wakiwamo wanasheria, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa sasa na wa zamani, wanasiasa wawili wa kambi ya upinzani na baadhi ya wanafamilia na hivyo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kuubadili ama kuuficha “milele”..

Kwa mujibu wa habari hizo, sehemu ya waraka huo inaelezwa kuelezea kwa kina kuhusu nini hasa kilichofanyika hadi BoT ikaidhinisha kutolewa kwa kiasi cha Sh bilioni 133/- na Ballali anaeleza kwa uwazi wahusika wote wakuu wakiwamo viongozi wa juu wa Serikali na wanasiasa walioshinikiza na waliochukua sehemu kubwa ya fedha za EPA pamoja na watendaji wa BoT walioshiriki katika zoezi hilo.

Waraka huo ambao kwa sasa unatafutwa kwa udi na uvumba unadhihirisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Serikali kutokana na baadhi ya wahusika muhimu wanaotajwa na Ballali kutozungumzwa popote linapozungumzwa suala la EPA na hata katika vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa waliouona waraka huo wa wosia, Ballali, kwa mfano, anaeleza jinsi alivyosita kuidhinisha malipo ya Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ambayo pekee ilikabidhiwa kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh. bilioni 40/-) kwa kutumia nyaraka za kughushi.

“Ballali ameeleza katika waraka ule kwamba alikataa kuidhinisha malipo hayo akielezea jinsi isivyo sahihi kutumia nyaraka za kughushi lakini aliitwa na mwanasiasa mmoja akiwa na mwanasiasa mwingine mkongwe mwenye ushawishi hadi sasa ambako aliamrishwa kuidhinisha malipo hayo mara moja.

“Unajua alivyoitwa aliwaeleza athari za kutumia nyaraka za kughushi wakamlazimisha na baada ya kuona wanamlazimisha akawaambia kama BoT itaidhinisha basi mtu anayatakiwa kukabidhiwa fedha hizo hastahili kwa kuwa kuna fedha nyingine zaidi ya Dola za milioni 60 alizotakiwa kurejesha kwanza kabla ya kukabidhiwa fedha zozote, lakini akalazimishwa kumlipa huyo huyo,” anasema mwanasheria aliyezungumza na Raia Mwema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara huyo ambaye ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania alikuwa akiwasiliana na wanasiasa waliomshinikiza Ballali amlipe kiasi cha kumpigia simu Ballali kabla hata ya kuondoka viwanja vya majengo alikokutana nao.

“Unajua inatisha kwani Ballali anasema katika waraka wake huo kwamba alipotoka tu kuzungumza na wazee wale kabla hata ya kuondoka akapigiwa simu na mfanyabiashara huyo akimuuliza kama alikwisha kupata maelekezo na yeye kumtaka aende ofisini ambako atakutana na msaidizi wake ambaye ndiye anayeshughulikia fedha za EPA,” anasema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara aliyekabidhiwa fedha hizo ana uhusiano wa karibu sana kibiashara na kijamii na ofisa wa BoT aliyehusika pia na sehemu ya mchakato wa EPA, jambo ambalo limeelezwa kwamba linazidi kuibua utata baada ya wote wawili kutotajwa popote katika sakata hilo.

“Sijasikia popote huyo ofisa wa BoT akitajwa maana hata nafasi ya ugavana alikuwa akitajwa kuwa anaweza kupewa lakini bahati ndiyo akateuliwa Profesa Benno Ndulu, maana angeteuliwa (anamtaja jina) mambo yangeendelea kuwa mabaya zaidi na siri nyingi zingefichwa lakini sasa najua mambo yatajulikana tu,” anasema.

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inatajwa kuchota zaidi ya Sh. bilioni 40/- hadi sasa haijulikani ilipo pamoja na kuwapo madai kwamba ilikabidhiwa kwa mfanyabiashara mmoja mwenye kashfa nyingi nchini ili ionekane kuwa ni ya kwake lakini hadi sasa haijaelezwa bayana hasa ni mali ya nani.

Kampuni hiyo kwa kumbukumbu za Msajili wa Makampuni (BRELA) inaonyeshwa kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina kampuni tofauti jirani lakini namba hiyo haionekani na kinachoonekana ni viwanja kuanzia Plot 77 na hata Plot 86 na Plot 88 katika eneo hilo maarufu la viwanda lakini plot ilipo Kagoda haionekani popote.

Aliyesimamia na kufuatilia BoT na hatimaye chukua fedha za kampuni hiyo katika Benki ya CRDB Limited tawi la Azikiwe anajulikana waziwazi na wafanyakazi wa maeneo hayo, lakini kumbukumbu zake zinaelezwa kupotea ama kufichwa na wahusika kwa nia ya kuwasaidia watuhumiwa ama kwa sababu za kichunguzi.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba wapelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwisha kuchukua nyaraka zote muhimu ikiwa ni pamoja na kadi ya benki iliyotumika kufungulia akaunti tawi la Azikiwe, ikiwa na picha na saini za wahusika wote muhimu kwa uhakika zaidi.

Sakata la BoT na zaidi akaunti ya EPA lilichukua sura mpya baada ya kuelezwa kwamba sasa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha fedha zote kiasi cha Sh. bilioni 133 zinarejeshwa kabla ya kuchukuliwa hatua kwa wale waliofanya makosa ya kijinai katika kupata fedha hizo.

Imeelezwa katika hali ya kutatanisha tayari hata fedha kutoka kwa wamiliki wa Kagoda nazo zimekwishakuanza kurejeshwa japo kwa awamu, jambo linalodhihirisha kwamba Serikali inawafahamu kwa hakika kabisa wamiliki wa Kagoda na inawaficha ama inataka kuwalinda kwa sababu za kisiasa zaidi.

Katika uchunguzi wa awali wa mkaguzi wa nje, Samuel Sithole wa kampuni ya kimataifa ya Deloitte & Touche tawi la Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo “nyeti” ya kiusalama.

Hata hivyo, siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na Gavana Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo ambaye sasa ameachwa nje ya Baraza la Mawaziri.

Baada ya kifo cha Ballali sasa inaelezwa kwamba uchunguzi unaoendelea dhidi ya wanaotajwa kuchukua fedha za EPA unaweza kufungwa kwa kuwa shahidi muhimu atakuwa hawezi kutoa maelezo yake mahakamani jambo ambalo linaelezwa kuweza kuichafua zaidi serikali.

Ballali ambaye amefariki dunia akiwa nchini Marekani na kuzikwa huko huko anaelezwa kuondoka na siri nzito ikiwa ni pamoja na mazingira ya kuondoka kwake, kuugua na hata kifo kumkuta huku serikali ikiendelea ‘kuweweseka’ na ‘kutapatapa’ kutokana mkanganyiko mkubwa wa yaliyomsibu gavana huyo wa zamani.

Hata mahali na siku aliyofariki Ballali ni mambo yaliyoelezwa kuwa na utata hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba alifia Boston, huku wengine wakisema alifia nyumbani kwake Washington DC Ijumaa ya Mei 16, 2008 na baadaye taarifa zake kutangazwa Jumanne usiku ikiwa ni siku tano baadaye, huku baadhi wakianza kudai kwamba alifariki Jumapili ya Mei 18, 2008. Hata mazishi yake yalifanywa kuwa siri na ni wanafamilia wachache tu waliobahatika kuuona mwili wake Jumanne Mei 20, 2008.


KANISA la Mt. Stephen Shahidi

Mwili wa marehemu Ballali ulihifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko Washington DC, kabla ya ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC. Kanisa hilo lipo 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037 na baadaye kuzikwa kwa faragha katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, Maryland.

Pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali, hasa magazeti na kutangazwa majukwaani, Ballali hakuwahi kushtakiwa rasmi pamoja na kuwapo taarifa kwamba aliwahi kuhojiwa na TAKUKURU.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.

“Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti,” alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.

Aliongeza Warioba: “Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.

“Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.

“Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.

“Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.

“ Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika.”

Ballali ambaye ameacha mke na familia, amekuwa akitamka wazi kwamba hajawahi kuiba hata senti moja ya umma katika kipindi chote akiwa BoT na kuwashutumu watu ‘aliowakwamisha’ kuwa chanzo cha kuandamwa kwake na tuhuma mbalimbali kabla ya kukataliwa kujiuzulu na hatimaye uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Marehemu Ballali alijiunga na Benki kama Gavana Julai 14, 1998 hadi Januari 8, 2008.

Ballali alikwenda ghafla nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana akiwa na nia ya kurejea nchini, alikwama huko baada ya kubainika na matatizo makubwa tumboni kabla ya kulazwa hospitali na kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Kwa mujibu wa habari za awali, Ballali aliieleza familia yake kwamba alikuwa akihofia kula kitu chenye madhara makubwa hasa baada ya madaktari wa Marekani kumfanyia uchunguzi mara tu alipowasili nchini humo, madhara ambayo alionyesha kuhisi kuyapata alipokuwa nyumbani hasa kati ya miji ya Dar es Salaan na Dodoma.

Wakati akiendelea na matibabu, Ballali aliandika barua kuelezea nia yake ya kuomba kujiuzulu kutokana na kuendelea kuzorota kwa afya yake huku akiwa bado na majukumu mazito ya kusimamia uchumi wa Taifa.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za upande wa Serikali kuthibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Ballali siku kadhaa kabla ya serikali kutangaza matokeo ya ukaguzi wa kampuni ya nje iliyopewa kazi ya kukagua hesabu za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kupitia ripoti ya wakaguzi hao, ndipo alipotamka kumfuta kazi Ballali bila kuzungumzia lolote kuhusu kujiuzulu kwake.
 
Inasemekana mtu mashuhuri aliyesafiri hivi karibuni ni fisadi Mkapa.

Wakati hayo yakiendelea, habari zinasema kwamba kuna mkakati maalumu wa kuhakikisha kwamba siri ya waraka huo haitolewi hadharani na baadhi ya watu mashuhuri wamethubutu kusafiri hadi nchini Marekani kufanikisha mkakati huo bila kujua mengi zaidi yapo nyumbani Tanzania.
 
ni kina nani hao hebu tuwaanike mapema wajue kwamba tuko macho......ebwana tusisubiri hadi wapate sababu..hebu tuwataje mara moja najua kuna watu wana data za kutosha na nina imani na Jf kwamba muda si mrefu tutauona wosia wa Balali
 
ukilazimishwa kufanya jambo ambalo unaamini kuwa siyo sahihi katika kazi ya kuteuliwa unajiuzulu.

Kwa vile pesa zilianza kupotea miaka mingi kabla ya kugunduliwa na kampuni ya nje, excuses za kulazishwa haziwezi kupokelewa sasa hivi.

Aliyelazimisha na aliyelazimishwa wote wako responsible.

kama kuna waraka uliodhamiriwa kwa wananchi njia sahihi ingekuwa ni kuutuma kwa vyombo vya habari.Kuukabidhi kwa wanasiasa ni kuendelea kuficha ufisadi na hakutaleta utatuzi wowote katika hili.
 
Hatimaye sasa imethibitishwa kuwa ni kweli Mkono, alikuwepo US katika kipindi fulani mwezi wa April, kwa sababu kuna mpaka interview ninayo sasa aliyoitoa kwa gazeti moja nchini kuhusu malipo yake aliyolipwa na BOT ya shillingi Billioni 7.9, aliifanya hiyo interview akiwa US, hii ni kubainisha habari kuwa alikwenda na kukutana na Marehemu kwa masaa karibu 24, ambako inasadikiwa alimkabidhi mikoba yote muhimu ya uporaji wa mapesa yetu wananchi, pole pole tutawafikia tu wote watinge kwenye sheria ya wananchi!

Huu mchezo ndio kwanza umeanza!
 
ukilazimishwa kufanya jambo ambalo unaamini kuwa siyo sahihi katika kazi ya kuteuliwa unajiuzulu.

Kwa vile pesa zilianza kupotea miaka mingi kabla ya kugunduliwa na kampuni ya nje, excuses za kulazishwa haziwezi kupokelewa sasa hivi.

Aliyelazimisha na aliyelazimishwa wote wako responsible.

kama kuna waraka uliodhamiriwa kwa wananchi njia sahihi ingekuwa ni kuutuma kwa vyombo vya habari.Kuukabidhi kwa wanasiasa ni kuendelea kuficha ufisadi na hakutaleta utatuzi wowote katika hili.

assumptions zako ziko sawa lakini kwa siasa na mazingira ya Nchi yetu ni hatari zaidi kukabidhi kwenye vyombo vya habari.. Angalia hata magazeti yanayounga mkono vita dhidi ya ufisadi na udhalim serikalini yote hayako wazi kwa mfano huyo mwandishi wa hiyo habari ameelezea story lakini hajataja jina la hao wanaotajwa katika hadithi hiyo...Hiyo yote inatokana na uoga, ubabe na jeuri ya pesa waliyonayo mafisadi....hivyo kuwakabidhi watu kama hao ni hasara zaidi..Njia nzuri zilikua ni;

(i) Kumkabidhi wosia huo Dr Slaa alieibua kashfa hizo
(ii) Kupost huo wosia JF.

Ni mtazamo tu...!
 
assumptions zako ziko sawa lakini kwa siasa na mazingira ya Nchi yetu ni hatari zaidi kukabidhi kwenye vyombo vya habari.. Angalia hata magazeti yanayounga mkono vita dhidi ya ufisadi na udhalim serikalini yote hayako wazi kwa mfano huyo mwandishi wa hiyo habari ameelezea story lakini hajataja jina la hao wanaotajwa katika hadithi hiyo...Hiyo yote inatokana na uoga, ubabe na jeuri ya pesa waliyonayo mafisadi....hivyo kuwakabidhi watu kama hao ni hasara zaidi..Njia nzuri zilikua ni;

(i) Kumkabidhi wosia huo Dr Slaa alieibua kashfa hizo
(ii) Kupost huo wosia JF.

Ni mtazamo tu...!

mtazamo wako mzuri sana na uko sahihi.
Kwa nyongeza tu, JF pia ni chombo cha habari.
 
Duh...hivi mkono ataponea mlango upi??? kila kitu yupo kinachomhusu Balali yupo.... ni wakati wa kumuomba nakala ya wosia
 
Hatimaye sasa imethibitishwa kuwa ni kweli Mkono, alikuwepo US katika kipindi fulani mwezi wa April, kwa sababu kuna mpaka interview ninayo sasa aliyoitoa kwa gazeti moja nchini kuhusu malipo yake aliyolipwa na BOT ya shillingi Billioni 7.9, aliifanya hiyo interview akiwa US, hii ni kubainisha habari kuwa alikwenda na kukutana na Marehemu kwa masaa karibu 24, ambako inasadikiwa alimkabidhi mikoba yote muhimu ya uporaji wa mapesa yetu wananchi, pole pole tutawafikia tu wote watinge kwenye sheria ya wananchi!

Huu mchezo ndio kwanza umeanza!

Mkuu narudia tena, huyu Mkono wengi wetu tumemweka kwenye kundi la mafisadi kutokana na malipo makubwa aliyoyapata toka BoT ambayo hadi hii leo ameshindwa kuyatetea. Hivyo kama yeye ndiye aliyeachiwa ushahidi kuhusiana na mafisadi wa EPA, basi sidhani kama kitatoka chochote kitakachotusaidia Watanzania kujua mengi kuhusiana na ufisadi na ujambazi mkubwa uliofanyika BoT
 
  • Thanks
Reactions: SDG
mtazamo wako mzuri sana ny uko sahihi,
kwa nyongeza tu. JF pia ni chombo cha habari.

yah JF ni chombo cha habari pekee Tanzania kinachomkoma nyani giladi kweupe....sema ni kitu gani humu kinafichwafichwa au kuonewa aibu???!!! na ndio maana nakuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba viongozi wakubwa wote wanatembelea jamvi hili kuliko hata member wa kawaida..

1
 
Mkuu narudia tena, huyu Mkono wengi wetu tumemweka kwenye kundi la mafisadi kutokana na malipo makubwa aliyoyapata toka BoT ambayo hadi hii leo ameshindwa kuyatetea.

Mkuu Heshima Mbele,

Unajua huwa ninakusanya magazeti yote ya bongo ya mwezi mzima na kuyasoma kama siku mbili mfululizo kila mwezi, Ushahidi wa Mkono, kuwepo US nimeupata kwenye gazeti la,



The Citizen la Wednesday, 16 April 2008, akitetea malipo yake ya shillingi Billioni 7.9 form Central Bank alifanya akiwa US.
 
yah JF ni chombo cha habari pekee Tanzania kinachomkoma nyani giladi kweupe....sema ni kitu gani humu kinafichwafichwa au kuonewa aibu???!!! na ndio maana nakuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba viongozi wakubwa wote wanatembelea jamvi hili kuliko hata member wa kawaida..

1

nilipoandika kuwa JF pia ni chombo cha habari nilimaanisha kuwa kwenye response yangu ya kwanza nilipoandika kuwa njia sahihi ingekuwa ni kuutoa waraka huo kwenye vyomo vya habari ilijumuisha JF pia.
 
GT angesema hivi

33csysn.jpg


huwa napenda sometimes GT anpojibu hoja kwa image....
 
Inawezekana hata huyo Mkono mwenyewe hajaachiwa chochote

Kwa maoni yangu ni kuwa tunatakiwa tuwabane watupe ripoti halafu kila kitu kitajipa.

Maelezo yatakayotolewa ambayo inasemekana Ballali alimpa Nimrod Mkono yatadhibitika kuwa na nia nzuri ya ukweli mbele za wananchi na yenye haki zenye uwezo wa kusafishana endapo tu tutayalinganisha na ripoti ya uchunguzi kuona kama yana ukweli ama la.

Haya mambo ya nyaraka wakati alikataa kusema akiwa hai yanazidisha vuguvugu la changa zito la macho.
Kama ripoti itabaini nafasi ya Ballali either kama shahidi ama mtuhumiwa then tutajua kama huo waraka wake utasaidia ama kama ni mbinu nyingine tu ya kiusanii.
 
wosia kuachiwa mkono ni biashara ya kesi ya nyani kupewa ngedere...mkono mwenyewe naye si mmoja wao tu hao haoo halafu tutegemee kitatoka kitu??mayb de one tutayopewa ni ile edited one kuwa marehemu alikua na shillingi elfu kumi bank kamwachia mkewe Ana etc ( as if kweli amekufa! )
 
Hivi mmesoma habari hii vizuri?
Kuna watu zaidi ya watano wanao huo Wosia.Hata kama mkono anao si hoja.

"Wote wawili wanasema kwamba waraka huo unaweza ama uko mikononi mwa watu zaidi ya watano wakiwamo wanasheria, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa sasa na wa zamani, wanasiasa wawili wa kambi ya upinzani na baadhi ya wanafamilia na hivyo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kuubadili ama kuuficha “milele”..

Tena ametia sahihi ya dole gumba na kaandika kwa hati ya maandishi yake(yaani kwa mkono).
Serikali wanajifunika shuka wakati kumeshapambazuka tayari
 
Back
Top Bottom