Wosia wa babu kwa mjukuu wake juu ya wanawake

SumadaVinci

Senior Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
161
Reaction score
328
Babu akiwa na mjukuu wake akamuusia yafutayo juu ya mwanamke/wanawake

1. Mwanamke yoyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa mama yako

2. Wanawake wote huonesha UPENDO wao wazi wazi isipokuwa wale waliotendwa kabla

3. Mwanaume kumuacha MWANAMKE anayempenda ni kama simba kuacha kula swala,,, lakini mwanamke kuamuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia simba mzee

4 Jihadhari na maneno ya VIJIWENI ,kwamba wanawake wote wako sawa kitabia la hasha!.... lakini kumbuka hakuna mwanamke asiye mwanamke

5. Kujaribu kumsahau mwanamke uliyewahi kumpenda ni ngumu sana ,,ni sawa sawa na kumkumbuka mtu usiyemjua

6. Ukipata mke mwema utakuwa na furaha ukipata mke mwovu, utakuwa mwanafalsafa

7. Muhimu kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa ,la usipojiandaa ama unaweza kuua au kujiua........ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyo kuwa hai

8.Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni...hapa duniani ni ngumu ......Omba mungu kuna makubaliano bila pesa

9.Wahenga wanasema Ukweli unauma ....na mimi nakuambia UONGO UNAUA

10 . Ili ubaki salama katika kupenda sharti UJIPENDE kwanza mwenyewe
 
Hawa watu(wanawake) hawa daaah aisee ni hatari sana, ndio maana Kuna jamaa alisema Mungu alianza kumuumba Adam pengine hakutaka kushauriwa na Hawa namna ya kumuumba Adam.

Hawajawahi kutuacha tukakaa kwa amani duniani!
 
kabisaaa
 
Pale tamu na chungu vinapowekwa kwenye kikombe kimoja halafu unatakiwa unywe tamu tuu, chungu uiache.

Ukifanikiwa hkuna mwanamke atakushinda kuishi nae. Ukijikuta tamu na chungu zote ziko mdomoni una mawili, kutema ukishindwa kuvumilia ladha ama kumeza na kukubaliana na uhalisia.
 
Babu akiwa na mjukuu wake akamuusia yafutayo juu ya mwanamke/wanawake

1. Mwanamke yoyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa mama yako

2. Wanawake wote huonesha UPENDO wao wazi wazi isipokuwa wale waliotendwa kabla

3. Mwanaume kumuacha MWANAMKE anayempenda ni kama simba kuacha kula swala,,, lakini mwanamke kuamuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia simba mzee

4 Jihadhari na maneno ya VIJIWENI ,kwamba wanawake wote wako sawa kitabia la hasha!.... lakini kumbuka hakuna mwanamke asiye mwanamke

5. Kujaribu kumsahau mwanamke uliyewahi kumpenda ni ngumu sana ,,ni sawa sawa na kumkumbuka mtu usiyemjua

6. Ukipata mke mwema utakuwa na furaha ukipata mke mwovu, utakuwa mwanafalsafa

7. Muhimu kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa ,la usipojiandaa ama unaweza kuua au kujiua........ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyo kuwa hai

8.Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni...hapa duniani ni ngumu ......Omba mungu kuna makubaliano bila pesa

9.Wahenga wanasema Ukweli unauma ....na mimi nakuambia UONGO UNAUA

10 . Ili ubaki salama katika kupenda sharti UJIPENDE kwanza mwenyewe
Amina
 
Back
Top Bottom