Wosia wa baba - John Pombe Magufuli

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Hii nchi ni tajiri, Tanzania ni Tajiri sana ndugu zangu

Mungu aendelee kukupumzisha kwa amani



Hata wasiompenda kwa kuwabana kwa maslahi ya taifa wanakubali kazi zake




Tunakumiss ila tunakushukuru kwa kutuachia chuma kingine Samia Suluhu Hassan, Mama wa taifa.
Mama anasema KAZI IENDELEE 💪
 
Huyu mzee katuamsha usingizini, watanzania wengi ni watu wa kuchukulia poa kila jambo na wafuata mkumbo.

Endeleeni na upuuzi wenu wa kuabudu wazungu mtakula makombo ya nchi yenu viuno nyie.

Huyu mzee alikuwa na uthubutu, Namuomba Mungu atuletee mwingine kama huyu anyooshe wajinga wachache waliosalia.

Hatuwezi kuishi kipuuzi puuzi bila msimamo na kuamini mawazo yetu.
 
Huyu mzee katuamsha usingizini, watanzania wengi ni watu wa kuchukulia poa kila jambo na wafuata mkumbo.

Endeleeni na upuuzi wenu wa kuabudu wazungu mtakula makombo ya nchi yenu viuno nyie.

Huyu mzee alikuwa na uthubutu, Namuomba Mungu atuletee mwingine kama huyu anyooshe wajinga wachache waliosalia.

Hatuwezi kuishi kipuuzi puuzi bila msimamo na kuamini mawazo yetu.
Goodguy😍😍
 
Tutamkumbuka kwa mengi sana aliyotutendea Hayati JPM

Biashara ya dawa za kulevya ilishamiri sana nchini, alipoingia Jpm biashara ikakomeshwa haswa.

Wimbi la ujambazi na uvamizi wa vituo vya polisi na kupora silaha aliukomesha mara moja ikiwemo hata ugaidi wa kule Kibiti

Reports za CAG enzi hizo ilikuwa kila mwaka lazima ioneshe Serikali inavyopoteza mapato kwa kulipa watumishi hewa, alipoingia JPM alishughulika na hilo ipasavyo

Ameanzisha mifumo ya ukusanyaji kodi kwa kupitia ulipaji wa control number ambayo imeimarisha sana namna nzuri ya kukusanya na kudhibiti uvujaji wa mapato.

Alijitoa muhanga kudhibiti utoroshaji wa madini yetu, ambapo makampuni yalikuwa yakitorosha na hvyo Serikali kukosa kodi

Sekta ya miundombinu imeimarika sana ktk awamu yake, tumeshuhudia ujenzi wa barabara kiwango cha lami mitaani na barabara kuu za kuonganisha mikoa, Wilaya na vijiji

Sekta ya Afya nako tumeshuhudia ujenzi wa vituo vingi vya afya na kuimarisha usambazaji wa madawa na vifaa tiba

Enzi zile za miaka nyuma tulishuhudia mpaka Twiga wakitoroshwa kwenye ndege, tembo wakiuawa, ikafikia hatua mpaka ujio wa Rais wa China nchini ukiingia kwenye kashfa ya kuondoka na pembe za ndovu.
Ila alipoingia jembe Magufuli haya yote yalibaki historia

Pamoja na madhaifu yake machache lakini kiukweli MAGUFULI amepiga kazi, ameonesha ujasiri wa hali ya juu ktk kushughulikia changamoto ambazo tuliona ni ndoto kutatuliwa, ameonesha nia na uzalendo wa kupambania kulinda rasilimali za nchi ili ziifaidishe nchi

RIP JPM
 
Back
Top Bottom