WORLD VISION ni shirika la wachaga??

WORLD VISION ni shirika la wachaga??

Status
Not open for further replies.

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
6,557
Reaction score
25,749
Nimeishi sana arusha na huku ndiko makao makuu yao na wana Projects nyingi sana wenyewe wanaziita ADP's cha ajabu kila ADP ofisini wote ni wachaga!

Nilishtuka kidogo lakini nikapotezea nikajipa moyo labda 'mcheza kwao utunzwa' (wachaga>>arusha) baadae nikahamia tanga nako wana ADP nyingi sana wilaya tofauti tofauti nako pia hali ni ileile kila ofisi ya ADP unayoenda wachaga wamejaa!!! Ikaniuma kiduchu nikajipa moyo labda kwasababu tuko nao karibu (tanga na arusha)..

Sasa last week nimekuja Morogoro nikaenda pale ofisi yao kuu ya mkoa (MOROGORO CLUSTER OFISI) nikakuta ofisi wachaga 90%!!! Kesho yake nikaenda kwenye moja ya projects zao inaitwa MLALI ADP iko ndani ndani kabisa vijijini huko nako project manager mchaga, project accountant mchaga, zagazaga nyingine nao 80% wachaga!!

Nikafadhaika sana ikabidi nimuulize swali mmoja ni Staff wa hapo mlali adp (sio mchaga) akanijibu kuwa hata yeye aelewi ila hali ni hiyo hiyo karibia tanzania nzima, yeye binafsi kabla ya kuja mlali alikuwa ofisi ya kigoma nako hali ni hiyo hiyo, wachaga wachaga wachaga!!!!

Nikachoka
 
world vision ni shirika la kibaguzi sana.. kwenye interview unaulizwa vifungu vya biblia,, yani kama wewe sio mchaga na mkristo hupati kazi hapo
 
sikatai kuwa kuna weza kuwa na kaupendeleo. lakini niweke wazi maeneo mengi tz yanatofautiana itikadi. moja ya itikadi ya wenzetu huko moshi ni kusomesha watoto.

kuna familia nyingi unakuta kipaumbele ni mme kuowa na mke kudai talaka na watoto kulelewa bila muelekeo. sisemi kuwa hawawezi toka wasomi lakini mazingira sio user friend. mbona wahaya ndio wanaongoza kufundisha vyuoni hujasema?
 
---- wee utabakia hivyo hivyo soma upate fursa utakuta wewe Muha
 
Kaombe kazi Muslim aid utapata fursa mumiani wee
 
Acha umbeya hata director wa WVT si mchagga mbona husemi wazungu? Msaidizi wake ni mhaya na wengineo ni mchanganyiko. Isitoshe kila sehemu ya kazi watu huingia kwa merits and mojawapo ni kuwa informed and to take the chance. If you will not be ready to take chances then utabaki kujisemea watengeneza ndege wote why ni wazungu? Think big hapa jamvini sio mahala pa kujadili umbeya na unafiki uzandiki. Jadili sense. Hata kama ni wachagga inakupa tabu gani? Chukua kabila lako pia wakaombe kazi hapo. Usitupotezee muda hapa jamvini kwa mada zako mbofu mbofu
 
ni kweli mkuu.n wachaga tu ndyo wamejaa hapo.kuna post 9 walizitanganza hapa cha ajabu wote n wachaga walichukuliwa.
 
Tunawakaribisha sana,lakini madai yako mtoatmada sidhani kama yanaukweli coz tupo wasukuma pia wengi tu,njoo lake zone wachaga ni wawili tu,kitu hujajua ni kwamba wakati wa nyuma kidogo shilika lilikua likiajili staff kutoka sehemu husika za miradi,kwa maana ya kwamba jamii ya eneo husika wanalijua eneo lao na wanaweza kufanya kazi na jamii hiyo ambayo ni ya kwake mwenyewe muajiliwa,ndo maana katika maeneo hayo umeona wachaga wengi kwa sababu ni maeneo yao,pole kwa kutokutuamini na ubarikiwe sana!
 
Ungechunguza endapo wana sifa za kazi wanazofanya na utaratibu wa kupata ajira,kamq vigezo na masharti vimezingatiwa na.watu wanasifa zonazotakiwa.
 
wachaga ni wabaguzi sana,, tatizo hr wao ni mchaga anaweka wachaga wenzake tu..

World vision ni shirika kikristo. Ni kama Islamic foundation au Muslim propagtion. Imesajiliwa hivyo na ina operate hivyo. Asubuhi kabla ya kuanza kazi ni mapambio ya sifa na kumwabudu Mungu. Baada ya hapo mnakula neno kisha mnaanza kazi. Ni mazingira magumu kwa asiye mkristo.
 
Tunawakaribisha sana,lakini madai yako mtoatmada sidhani kama yanaukweli coz tupo wasukuma pia wengi tu,njoo lake zone wachaga ni wawili tu,kitu hujajua ni kwamba wakati wa nyuma kidogo shilika lilikua likiajili staff kutoka sehemu husika za miradi,kwa maana ya kwamba jamii ya eneo husika wanalijua eneo lao na wanaweza kufanya kazi na jamii hiyo ambayo ni ya kwake mwenyewe muajiliwa,ndo maana katika maeneo hayo umeona wachaga wengi kwa sababu ni maeneo yao,pole kwa kutokutuamini na ubarikiwe sana!

kwanini world vision wafanyakazi wake wote ni wakristo?
 
mbona wamasai wengi wafugaji lakini huulizi? ndio kipaumbele cha jamii ile. mbona wahaya wengi huenda kusoma kupitiliza mpaka kubak vyuoni jamii yao imeifluencey. mbona wasukuma wakulima ndio jamii hiyo.mbona waznz hawapendi kufanya kazi ngumu ndio mazingira yao hayo mbona wachaga wanaenda shule sana ndio jamii yao hiyo kipaumbele.

sasa wewe ukitaka nafasi sijui za uchief accountanct na umenager soma upate cpa au masters utapata ajira tu sio usome kidegree cha juu juu.kuna wakenya hapa wameajiriwa kwa weledi tu. ukitaka kuwa mkulima kama sisi wamasai wenye ngo'mbe elfu 2 unatutaman kuwa mfugaji njoo umasaini au ugogoni tuanze kukaa porini na kufuga, usikimbilie dar kwenda kulalamka eti mbona wenye makundi makubwa ya mifungo ni wamasai na wasukuma angali wewe hutaki kutoka hapo town. tumia fursa.

NYIE NDIO MNATULETEA UKABILA. BADALA YA KUONGELEA UWEZO MNAANGALIA UKABILA. LABDA UNGEJENGA HOJA KUWA HAWAWEZI KAZI LAKINI WAMEPEWA NAFASI,ELIMU ZAO MBOVU ALAFU NI WA KABILA MOJA HAPO TUNGEKUELEWA KIDOGO.
 
Tunawakaribisha sana,lakini madai yako mtoatmada sidhani kama yanaukweli coz tupo wasukuma pia wengi tu,njoo lake zone wachaga ni wawili tu,kitu hujajua ni kwamba wakati wa nyuma kidogo shilika lilikua likiajili staff kutoka sehemu husika za miradi,kwa maana ya kwamba jamii ya eneo husika wanalijua eneo lao na wanaweza kufanya kazi na jamii hiyo ambayo ni ya kwake mwenyewe muajiliwa,ndo maana katika maeneo hayo umeona wachaga wengi kwa sababu ni maeneo yao,pole kwa kutokutuamini na ubarikiwe sana!

kwanini world vision wafanyakazi wake wote ni wakristo?
 
world vision ni shirika la kibaguzi sana.. kwenye interview unaulizwa vifungu vya biblia,, yani kama wewe sio mchaga na mkristo hupati kazi hapo

Huna tofauti na yule mnyama anaezaa na kula watoto nimesahau jina lake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom