Katuni gani hiyo itakuburudisha zaidi ya hii soka..T&J? au Dora?!..uwe unachungulia na soka wakati uko na katuni!
Haya wapenda kandanda, kipyenga ndo karibu kinapulizwa. Mimi niko na Chile leo
BJ, naona unazifagilia timu za EURO baada ya zile za Afrika.
Ni bora nimwangalie Popeye the sailor man na The Flintstones kuliko hawa Chile.....wameshaniboa
Na kesho ifike haraka tumpige (USA) mtu bao....nawaonea huruma wapenzi wa Ghana kesho
Kisije kibao kugeuka tu na ikawa vice versa.
Amini usiamini kesho niko upande mmoja na Obama.....sports can also make strange bedfellows....lol
Nasikia Slick Willy naye atakuwa ndani ya nyumba kesho....Go USA go....wafunge hayo Maafrika magharibi
Haya endelea tu na hizo katuni mana ni 2-0 sasa Spain wakiwa juu!..Na kesho Ghana wanaweza kufungwa na US,sishangilii timu yoyote kesho ntamshangilia mshindi tu!!
USA hawawezi kuwafunga Ghana poleni washabiki wa Obama and co. mwambieni tu Bill Clinton arudi nyumbani aendelee kula tende.
Hilo neno mkuu timu zetu zimeharibu sana hope Ghana watafanya vyema kwenye hii round ya pili.yani umesubiri goli la kwanza ndio ujitambulishe unawashangilia ha ha ha .haya kila la kheri mie nipo nipo tu nsubiri kesho sitaki stress za ajabu saa hizi nimebeba za kutosha na timu zangu za africa.
Italy wamenyolewa kwa chupa na kuachia kombe mapema sana katika duru za awali sana. Nadhani wamejisikia kufedheheka sana.
Wanna put a wager?
Ghana tu imebaki saa hizi ndio raha ya World cup inaanza mwanzo timu za nyumbani zilikuwa zinachanganya habari au kama vipi shangilia magoli ya timu zote lol.siangalii mechi zijazo nahisi kuumwa maana uzalendo umeniponza!!
niwe napitia-pitia umu jamvini basi
!!!!!!
Mkuu Ghana anamfunga USA leo vizuri tu.
hivi tukishakumfungisha virago OBAMA leo, tunakutana na mshindi wa mechi gani? hehehe kweli WC imeanza sasa ,acha nifute TV mavumbi kidogo
Uruguay au mkorea.World ndio inaanza na leo usiwe na wasi wasi mkuu Ghana hawatuangushi kabisa.