Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 362
- 714
Kwanini Wokovu wa zamani ulikuwa wa Moto
Wakati nikiwa kwenye kongamano la maombi la kitaifa la 18 linaloongozwa na Mwalimu Christopher Mwakasege.
Wakati ibada zikiwa ziliendelea na wakati tukiwa safarini kutoka kwenye hosteli kwenda ukumbini, kuna kitu nilijifunza
Nikamuuliza mama mmoja mtu mzima miaka 60s nikataka jua enzi zao wakati wanaokoka nini kiwasaidia wokovu wao kuwa wa moto
Kitu ambacho aliniambia na nilichokiona kwamba zamani hakukuwa na nyimbo za sifa wala kuabudu kulikuwa na nyimbo za tensi na ili mtu aonekane ameokoka lazima tenzi za rohoni ziwe moyoni
Ilikuwa ni muhimu kuimba nyimbo za tenzi kwa sababu vitabu vilikuw vichache na hivyo ukipata kitabu unajitaidi kuimba kwa bidii ili nyimbo zikae ndani yako
Nilichokiona wakati wa nyimbo mara nyingi tulikuwa tunaangaika na simu kuweza kupata kitabu husika lakini wenzetu walikuwa wanaimba kutoka moyoni.
Nyimbo za tenzi asilimia 100 ni nyimbo za ushuhuda wa matendo ya Yesu, nyimbo zote zinamjenga muhumini kuwa karibu na Yesu
Katika nyimbo za tenzi sehemu kubwa zilikuwa ni kumjenga Mkristo kuwa karibu na Yesu na sio vinginevyo
Miaka yetu hii nyimbo nyingi za kikristo nyingi ni zile za kutaka vitu kwa Yesu na sio za kujenga uhusiano wako na Mungu
Nyimbo za kuimarisha uhusiano na Mungu ni lazima zikutengezee moyo wa kumpenda Yesu, kumlingana Mungu kwa sababu nyimbo zile zilikuwa ni shuhuda za watu ambao walitembea na Yesu ndio maana zilijenga waumini kiu ya Yesu ndio maana ziliitwa tenzi ya roho au nyimbo ya Kristo nk