Wizi wa pesa za Umma sababu ya Raia kukosa elimu husika

lugano GTB

Member
Oct 23, 2020
90
144
Jana tarehe 14-12-2020 nilisafari kwa basi dogo maarufu kama Coaster kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma muda ukiwa umeenda kidogo kwa sababu nilikuwa na ratiba ngumu iliyopelekea kusafiri usiku.

Tulisfiri kwa tabu kidogo kwa sababu coaster tuliyopanda Mbezi mwisho ilipofika Morogoro ilitufaulisha kwenye coaster nyingine kwa sababu wanazozijua wenyewe.

Kuna umuhimu wa kila mtu kujisomea sheria mbalimbali zinatumika nchini angalau kuwa na uelewa kidogo wa kuweza kupambana na changamoto mbalimbali zinazoweza kukutokea bila kutarajia katika maisha kama nitavyoeleza hapo chini.

Coaster ya kwanza iliyotuchukua Dar - Mbezi mwisho saa kama saa kumi na mmoja na dakika 08 (11:10)chache jioni ilitufikisha Morogoro Msamvu saa tatu na nusu usiku(03:30 usiku) baada ya kugombana nao kutuchelewesha saa nzima wakidai kuwasubiri abiria wengine.

Coaster ya pili iliyotuchukua Morogoro Msamvu iliondoka saa nne na nusu (10:33) kwa baada ya wasafiri kuamua kwa pamoja kushuka na kuomba dereva na kondakta wake waondoe gari mara moja lasivyo waturudishie nauli zetu; tuliondoka saa nne na nusu usiku na kufika Dumila ambapo sekeseke la story ndipo ilipojikita.

Ofisa wa LATRA wakishirikiana na Trafiki walisimamisha coaster tuliyopanda na baada ya ukaguzi walikutwa na makosa ambayo yalipelekea kuadhibiwa faini ya shs 500,000/= na sisi kucheleweshwa kuondoka hadi saa nane na dakika thelathini na saba (8:37 usiku ).

Baada ya abiria kujadiliana wenyewe kwa umoja wetu tuliamua kushuka kuwakabili hao maofisa kujua tatizo na suluhisho lake na majibizano yalikuwa haya

ABIRIA:Ofisa tumekaa hapa muda wa saa nne bila maelezo ya msingi tatizo nini na unatusaidiaje?

OFISA POLISI: Yeye hakutujibu kabisa aliondoka kimyakimya na kutupuuzia

ABIRIA: Tuliamua kumfuata Ofisa wa LATRA na kumuuliza swali lile lile la mwanzo

OFISA LATRA: Kwani hamjui dereva hajawaambia kosa lenu

ABIRIA: Hapana

OFISA LATRA: (i)Gari halina kibali cha safari (ii) Hakuna mkataba kati yenu abiria na mwenye basi kwa sababu hamna tiketi (iii) Mwenye gari hana EFD receipt ya kukodishwa gari hivyo ameikosesha Serikali mapato ya kodi ya VAT.... kwa maana hiyo dereva na kondakta wanatakiwa kulipa faini ya tshs 500,000/= ili gari lipate ruhusa ya safari.

ABIRIA: Je, kama dereva na kondakta hawana hizo pesa ? je sisi tutaendelea kukaa hapa kama mateka? kwa sababu hata sisi ni waajiliwa kama wewe na kesho tunatakiwa ofisini asubuhi na mapema?

OFISA LATRA: Nimewapa njia mbadala walipe nusu ya pesa sasa hivi ili muondoke

ABIRIA: Je, kama hawana pia hiyo nusu ya pesa inakuwaje?

Baada ya majadiliano na maswali mengi kati ya pande tatu Abiria wakiuliza Ofisa anatumia vifungu gani amabvyo vinamtaka mwenye gari alipe papo hapo badala ya uataribu wa Serikali kulipia kwa CONTROL NUMBER ndani ya siku saba OFISA akalegeza msimamo na kusema wajidhamini kwa leseni ya udereva au sticker ya SMATRA nadhani walifanya hivyo na tuliruhusiwa ambapo tumefika Dodoma saa kumi na moja asubuhi (11:00)

MASWALI
1. Sheria ya faini kwa baadhi ya makosa inataka pesa ilipwe taslimu kwa ofisa sababu tu amatoa notification au ilipiwe kwa Control Number ? Je nusu ya faini inaweza lipwa kwenye tukio na nyingine baadaye?

2.Ofisa LATRA anaruhusiwa kutoa notification bila taarifa ya agari husika kwenye hiyo notification. Kulikuwa na sababu gani ya kuomba leseni ye udereva au stikcker ya SMATRA kwa ajili kuwadhamini dereva na kondakta? AU hivi ndio vile vitabu vya mfukoni visivyojulikana na serikali

3. Sheria inasemaje kuhusu kumkalisha abiria kwa makosa ya mwenye gari? Tumekalishwa saa 4 mbele ya kituo cha polisi na tulipoomba kwenda kumuona Mkuu wa kituo Polisi walizima taa za kituo kukawa giza totolo.
 
Back
Top Bottom