Wizi unaofanywa na makampuni ya kusafirisha watu kwa ajili ya kazi nje ya Tanzania

Azniv Protingas

JF-Expert Member
Oct 29, 2020
299
457
Habari wana JF, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, sasa hivi kutokana na uhaba wa ajira ndani ya nchi yetu ya Tanzania, kuna makampuni ambayo yanatangaza yanatoa ajira nje ya nchi, hasa nchi za uarabuni.

IMG-20240303-WA0001.jpg

IMG-20240311-WA0113.jpg

Makampuni hayo yameanzisha mchezo wa kutangaza kuwa kuna kazi fulani, lakini inahitajika kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kujiandikisha. Watu wanaenda kujiandikisha lakini hakuna interview inayofanyika na pesa hazirudishwi.

Mwezi wa tatu kuna kampuni zilitangaza kuwa kuna nafasi za kazi Saudi Arabia na kujiandikisha kwa ajili ya hizo kazi ni 50,000/- hiyo pesa ni kwa ajili ya interview Tu. Kwa hiyo ukifeli au ukifeli hairudi hiyo pesa. Kuna watu walitoka sehemu mbalimbali za Tanzania lakini mpaka leo hakuna interview iliyofanyika na haijulikani ni lini hao wanaohusika na Interview kutoka kwenye kampuni ya Saudi Arabia watakuja lini.

IMG_20240510_211658.jpg

Na pia hakuna mrejesho wowote kutoka kwa makampuni kwamba labda vumilieni tumewasiliana na hiyo kampuni na tumefikia wapi lakini hakuna. Na wahanga wakubwa wa huu utapeli ni wanaume.

Pia juzi kampuni mojawapo kati ya hizo walitangaza kuwa kuna kazi za Canada, pesa walizokula kwa ajili ya interview ya Saudia hazijawatosha wamekuja na kazi nyingine. Wanajificha kwenye kivuli cha kuwa tumesajiliwa na serikali kwa hiyo tunafanya kazi kihalali, tumepewa ruhusa na serikali.

IMG_20240510_212827.jpg

IMG_20240510_212722.jpg

IMG_20240510_212746.jpg

N.b Sio kwamba hakuna ambaye amesafirishwa na hizo kampuni wapo waliobahatika kupata ajira. Lakini hii ya Saudi Arabia inaonekana kama imetengenezwa ili watu watoe pesa za usajili kwa ajili ya kunufaisha matumbo yao. Watu wakilalamika kuwa pesa ya usajili ni kubwa wanajibu kwa jeuri kuwa, tutapata wapi pesa ya kodi na mishahara ya wafanyakazi.

IMG_20240510_212213.jpg

IMG_20240510_212350.jpg

Hizi kampuni ni mfano tu lakini zipo nyingi na kuna watu wametapeliwa zaidi ya hiyo 50000/-. Na hizi kampuni sio mara ya kwanza kushtakiwa, Kuna moja ilifungiwa lakini baadae ikafunguliwa tena.
IMG_20240510_212858.jpg
 
kuna thread humu ya kupeleka watu poland
kam sijakosea sijawahi jua kam kuna watu walifikishwa huko poland😂
 
Ajira ni ngumu sana mimi mwaka jana nimelia sana, nilikopa kiasi cha laki moja nikaongeza na laki yangu niliyoipata kwa kuuza tofali zangu nikaenda kwenye usaili ,nikafaulu vema ,ila cha ajabu kuna mkufunzi aliniliza laki 2 na mpk wa leo sina kazi na waliofanya hivi ni mmoja ya wakufunzi wa kampuni ya ulinzi ya SGA .

Nilichoambiwa niwe nasubira ajira nitapata lakini mpaka waleo naelekea kutimiza mwaka sijapatiwa kazi ,kiujumla kazi ni ngumu sana yatupasa tusiwe na wepesi wakutoa pesa kwa ajili yakutafuta kazi maana kuna kutoa pesa na bado ukapoteza pesa yako , mimi naishi kwa kunung'unika mpaka waleo.
Inasikitisha sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kuwalaumu watanzania kwa ujinga na kutapeliwa, lazima tufahamu kuwa watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutatua changamoto zinazotukabili.
Serikali inabidi izifuatilie hizo kampuni zinazolalamikiwa kwa utapeli!!
 
Ngoja nikisanue mwanangu, hao nao ni graduates kama nyie wamekosa kazi wametafuta namna ya kuishi wakaona ni wajinga wengine wenye tamaa, si ajanu hata kenya hawapajui... jiongezeni😀😀😀
 
Ajira ni ngumu sana mimi mwaka jana nimelia sana, nilikopa kiasi cha laki moja nikaongeza na laki yangu niliyoipata kwa kuuza tofali zangu nikaenda kwenye usaili ,nikafaulu vema ,ila cha ajabu kuna mkufunzi aliniliza laki 2 na mpk wa leo sina kazi na waliofanya hivi ni mmoja ya wakufunzi wa kampuni ya ulinzi ya SGA .

Nilichoambiwa niwe nasubira ajira nitapata lakini mpaka waleo naelekea kutimiza mwaka sijapatiwa kazi ,kiujumla kazi ni ngumu sana yatupasa tusiwe na wepesi wakutoa pesa kwa ajili yakutafuta kazi maana kuna kutoa pesa na bado ukapoteza pesa yako , mimi naishi kwa kunung'unika mpaka waleo.
Pole sana
 
Huwezi kuwalaumu watanzania kwa ujinga na kutapeliwa, lazima tufahamu kuwa watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutatua changamoto zinazotukabili.
Serikali inabidi izifuatilie hizo kampuni zinazolalamikiwa kwa utapeli!!
Itakuwa vizuri Lkn hata zikifuatiliwa wataachiwa wataendelea kupiga watu wengine.
 
Back
Top Bottom