KERO Wizi unaofanywa na makampuni ya parking!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hivi unafahamu unapigwa katika parking?, Hawa jamaa wanapiga sana unapo egesha gari hata kama ukiondoka wao wanatunza kumbukumbu lisaa likiisha wanaongeza muda hata kama wewe upo kwako umelala utakutana nazo bills!

Hiyo ndiyo hali halisi ya wizi huu unaofanywa na kampuni ya parking na wafanyakazi wao! unawanufaisha wafanyakazi maana mapato yako ndiyo insensitive yako hivyo wanaiba sana!

Mbaya zaidi hata akikaa pembeni gari zinajipitia barabarani anaingiza Namba ya gari anaongeza mapato hata kama aujasimama umepita tu Maeneo hayo! Hatuwezi kuendelea na wizi wa namba hii lazima Serikali ifanyie kazi hili swala!

SULUHISHO NA MWAROBAINI NI HUU HAPA!
Kampuni itoe stickers zenye barcodes zibadindwe katika windscreen, mfanyakazi akija ana scan nakuacha lisiti kila muda ukiongezeka anascan tena, hii itatuondolea huu wizi unaofanywa na makampuni ya parking!
 
Back
Top Bottom