Renegade
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 7,346
- 7,169
Hamia Airtel, Voda nilishahamaga siku nyingi sana sitaki kusikia habari zao.Hivi ukihama Voda uhamie mtandao gani labda?
Maana majanga ya Tigo ni Tsunami
Hamia Airtel, Voda nilishahamaga siku nyingi sana sitaki kusikia habari zao.Hivi ukihama Voda uhamie mtandao gani labda?
Maana majanga ya Tigo ni Tsunami
TTCL tunakuja na 4G LTE. Utahama tu!kwahinsi Neti yao ilivyo faster hunishawishi kuhamia popote
Anzisheni Tweet ya kuhama Vodacom!
Ndugu umesahau kuwa hapa ni jukwaani?Mtu ametoa kero yake msikilize kama unaweza msaidie mawazo na si kumkatisha tamaa.Hujamtendea haki.Sijutii kuwa mteja w a kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM
Hayo matatizo munayapata kwa kutokuwa makini.
Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh
Ni kweli hakuna mtandao ulio safi hata kidogo wote ni majizi tu.Mimi naona karibu mitandao yote ni wezi tu, na wanaowaendekeza ni hao TCRA. Sasa kwa ushauri wangu na nini kifanyike, ni kuwafanyia kampeni kama ya Sitti Mtemvu.
Iwe watu wote na mitandao yote, kuwashinikiza TCRA waweze kuwasikiliza watumiaji wa hii mitandao ya simu.
Tunaelewa hiyo kampuni ya voda ina hisa za watu fulani, lakini nguvu ya watumiaji nayo ikitumika ni lazima TCRA wawe na meno sasa.
Huduma zao kwa wateja ni mbovu sana na unaweza piga simu isipatikane na hata ikipatikana wanakujibu wanavojisikia wao
Sijutii kuwa mteja wa kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM
Hayo matatizo munayapata kwa kutokuwa makini.
Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh
Mi niliishalalamika kwa kuandika email TCRA baada ya vodacom kuniibia laki moja ndani ya masaa 24. Sikuwahi kujibiwa email yangu nikajua hii ni kampuni ya "wakubwa". Watakuja mwakani kuomba kura zako uwape urahisi.
Ilitakiwa fedha yoyote tunayokatwa na vodacom kwa sababu zozote lazima ije na notification au niulizwe kwanza but wao wanakata bila ridhaa ya mwenye fedha, huo ni wizi
Ni kweli hawa jamaa ni wezi sana, hata kwenye vifurush vya internet. Ukiwa na MB100 na unatumia smartphone utashangaa ndani ya dakika 5 wanakutumia msg eti kifurush kimeisha! Mbona wenzao Tigo na Airtel ukiwa na MB100 unatumia mda mrefu??
Mbona unahamasisha watu waihame kampuni kwani ukihama wewe peke yako utapungukiwa nini? Awali ya yote ni kwamba una papara,umeshawahi kufika katika ofisi za Vodacom ukauliza swali lako? Kabla hujaenda huko fanya hili: Kabla ya kuweka salio hakikisha mobile data iko OFF katika simu yako,inawezekana unapoweka hela huwa zinaanza kuliwa kama Internet Charges. Tafakari kabla ya kuchukua hatua!
Lakini angalia inaweza kuwa kuna milio ambayo imejiunga nayo bila kujua kuwa inalipiwa. Maana wengine wanapopiga simu wakisikia wimbo wa kuitia na sauti inayosema "kuupata wimbo huu bonyeza nyota" wao wanabonyeza bila kujua watakuwa wanaulipia kila siku. Mimi nina kaka yangu ambaye ana nyimbo za miito kama 5 na kila siku analalamika salio kupungua bila kujua ni yeye amejisajili kwenye nyimbo nyingi ambazo anayempigia ndiye anayesikia na si yeyeWadau poleni na majukumu ya kila siku.
Kampeni hii ni maalumu kabisa ili kuweza kumwokoa Mtanzania anayeibiwa na kampuni hii ya mawasiliano inayowaibia wananchi mchana kweupe kabisa wizi wao ni huu, ukiweka salio labda 500 kabla haujajiunga wanakata kama shilingi 20 hadi 40 , unaweza kuweka pesa ili ujiunge na Kifurushi halafu pesa ipo wanakueleza haitoshi lakini pia kukuunganisha na huduma zao za kulipia kwa lazima bila hiyari yako hivyo tuwahamasishe ndugu zetu wahame hii Kampuni hawana adabu kwa wateja wao.
Sijutii kuwa mteja wa kampuni yoyote ya simu Tanzania,HASAHASA VODACOM
Hayo matatizo munayapata kwa kutokuwa makini.
Mods futa hizi pumba muende ofisini kwao si mnapajua, mumetuchosha Arrghh