Wizi mpya kwa "spray ya kichina" Dar

Wizi mpya kwa "spray ya kichina" Dar

Ha ha ha !
Du hapa Mkuu ulilamba dume.
Na mimi hasira yangu ingeisha.
Nitapata wapi hiyo felcos?

naitafuts nipe muda as long uko humu kuna washikaji wanaendaga jnb ntakujuza ...uwakamatishe si nyingi kama randi 200 enzi hizo 2009 hope kama imepanda sana 250..ni swadakta nakwambia majuzi ilibidi nimpe kamoja jiran yangu maana ninapoficha anajua mama didy tu si unajua wakizijua wanakugeuzia kibao hawa basi naficha kama ile sehemu ya shemeji yako
 
Wiki iliyopita jamaa yangu alikuwa mwananyamala, akaingia kwa dadake kumsalimia. Ile anatoka tu akakutana na jamaa wameshavunja kioo kidogo mlango wa nyuma, washafungua mlango wanahangaika na power window. Dah! Ilikuwa almanusura aliwawahi, ikabidi aingie gharama ya kununua kale kakioo kengine! Katika kuzuga, wale jamaa wakampiga mzinga eti wa shilingi mia tano!!
 
mimi binafsi nikimkamata nitamchinja ka kuku
nina hasira nao sana.
nimechunguza nasikia kuna baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya
wanamtandao wao.naendelea na uchunguzi ila ole wake atakaeingia mikononi mwangu!!
huyo mwanamziki na genge lake wanajulikana sana..shida ukiwavunja miguu polisi wanakusumbua wewe instead mpaka utajuta...very embarrasing! yaani uibiwe halafu uuziwe tena kwa bei maradufu!
 
Hawa wachina yaani wao ubunifu wao ni wa madhara tu..kuna jamaa alitoka huko kaja na kalamu ambayo akiandika baada ya dakika kadhaa wino unatoweka kabisaa nikajiuliza walibuni hii kalamu kwa nia gani ?
 
POle sana Majoja...<br />
<br />
we should just kill those dudes who steal, inauma sana aisee
<br />
<br />
wananchi wakiwaua mnalalamika wanajichukulia sheria mkononi.
 
nliibiwa bahati nzuri nliweka madaftari kwene begi la laptop wakajua laptop wakachukua na kadi za benki nikaenda oyssterbay police chaajabu police wa pale wananipa namba ya simu ya mwalifu nimwambie anipe vitu vyangu sasa tukimbilie wapi hawa police wanashirikiana nao moja kwamoja,now nimeingia gharama nimeweka alarm at least itasaidia akiligusa tu kelele mtindo mmoja
 
Back
Top Bottom