Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,959
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA WATU 32 KWA TUHUMA ZA MABILIONI YA BENKI YA NMB JIJINI DSM.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu 32 kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha Tsh Tsh Bil 2.082.00

Mnamo tarehe 08/06/2020 majira ya saa tisa mchana huko katika Benki ya NMB tawi la Mbezi

Beach wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi ya SECURITY GROUP OF AFRICA @ SGASecurity Tanzania Limited wakiwa na gari namba T 853 DPX MITSUBISH CANTER walikabidhiwa kiasi cha fedha Tsh Tsh 2 /= kwa maelekezo ya kuzisafirisha kutoka NMB tawi la Mbezi Beach ili wazipeleke tawi la NMB Benki House - CASH CENTRE iliyopo maeneo ya Posta Mpya.

Mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo wafanyakazi hao badala ya kuzipeleka walipoelekezwa, walitoweka na fedha hizo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM siku hiyo ya tarehe 08/06/2020 majira ya saa 12 jioni lilibaini kutelekezwa kwa gari hilo maeneo ya Mbagala rangi tatu jirani na Shule ya SAINT MARY.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na ujambazi lilianza ufuatiliaji mara moja ikiwa ni pamoja na kufika eneo lilipoonekana gari hilo na kubaini kuwa wafanyakazi hao watano wamekula njama na kuiba kiasi cha fedha Tsh kutoka kwenye sanduku moja la chuma kati ya masanduku manne waliyokabidhiwa.

Aidha, masanduku matatu yaliyokutwa katika gari hilo yalifunguliwa na kukutwa na kiasi cha fedha Tsh 1,302,000,000 /= pia katika gari hilo zilikutwa silaha mbili aina ya Short gun Pump Action yenye risasi 12 na Short gun Protector yenye risasi 05, pamoja na sare za kampuni hiyo.

Watuhumiwa hao walikamatwa Mkoa wa Mbeya na Kigoma wakiwa wamenunua vitu vifuatavyo:-

(i).Trckta Power Tiller aina ya TRA-Change Model 7C/15 lenye thamani ya Tsh 20,000,000/=

(ii),Pikipiki moja aina ya SANLG

(iii).TV flat screen moja aina SUNDA na vitu mbalimbali vya matumizi ya ndani kama kitanda, godoro,jiko la gesi,rnakochi n.k

Mpaka sasa katika shauri hili Jumla ya Tsh 1,497,680,000/= zimeokolewa, mbali na thamani ya vitu vilixyonunuliwa kutoka sehemu ya fedha zilizoibiwa.

Jumla ya "'atillnuniwa 32 wamekamatwa na kuendelea kuhojiwa juu ya ushiriki wao kuhusiana na tukio hili

Aidha Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika na tukio hili.

ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 07/07/2020 kwa madai ya kudai Tume huru ya uchaguzi waaache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
1594029083600.png
1594029179853.png

1594027089066.png
1594027226822.png
1594027242726.png
 

Attachments

  • Wizi Polisi.pdf
    960.8 KB · Views: 20
Mbwa kabisa hawa. Tanzania haina wezi ina matahira wa kiwango cha lami..

Wangepata master mind kama mimi wao ndio wangekamatwa mimi muda huu ningekuwa kisiwa cha mauritius nafanya yangu..
Mkuu ungekuwa unakunywa juisi ya Madagascar...:D
Hao wamekimbilia vijijini kwao hopeless case...
Ifikie mahali magari ya pesa yawe na secret escort za pikipiki au isiwe gari 1 yawe mawili au matatu...

Everyday is Saturday.........................:cool:
 
Tarehe 8 mwezi wa 6 bado hatujafika,huo uandishi JAMHURI ndio inaandikwaga hivyo
 
Hapo Suma jkt ndo inapigiwa chspuo ichukue kaz za ulinxi Mali za Benki.

Ila hawa majamaa kwanini hawanitafutagi tupige mpango bila kuacha alama

Walivyo wajinga wamepewa 2bln eti wamechukua mamilion kiasi na kuacha Zaid ya 1.3bln yan kweli wajinga hawaishi duniani
 
Kuna usemi unasema "hatua zote tisa"

Umeamua kutenda kitu hiyo ni hatua ya kwanza, kwanini usimalizie tisa?

Ushaamua kuiba kiasi kama hicho, unachotakiwa umalizie hatua za kukata mawasiliano na ndugu, kupotea nchini, kuacha ujinga, kuacha kuwaza nini kitatokea usipowaona ndugu zako...

Sasa umefanya hatua ya kwanza, zinazofuata ni kununua power tiller, sanlg na flat screen ya Sunda? Upo sawa kweli?
 
Kuna usemi unasema "hatua zote tisa"

Umeamua kutenda kitu hiyo ni hatua ya kwanza, kwanini usimalizie tisa?

Ushaamua kuiba kiasi kama hicho, unachotakiwa umalizie hatua za kukata mawasiliano na ndugu, kupotea nchini, kuacha ujinga, kuacha kuwaza nini kitatokea usipowaona ndugu zako...

Sasa umefanya hatua ya kwanza, zinazofuata ni kununua power tiller, sanlg na flat screen ya Sunda? Upo sawa kweli?
Jamaa wapumbavu sana.
 
Back
Top Bottom