Wizi mpya BOT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi mpya BOT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lusambara, Apr 18, 2011.

 1. L

  Lusambara Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI MWAKA ULIOISHIA TAREHE 30 JUNI, 2010 inasema

  5.9 Kukosekana kwa orodha ya waliolipwa kiasi cha Sh.48,000,270,000 kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi
  Serikali ililipa kiasi cha Sh. 48,000,270,000 katika Benki Kuu ya Tanzania kama sehemu ya mchango wake wa kuchochea ukuaji wa uchumi ili kukabiliana na msukosuko wa uchumi ulioikumba dunia. Hata hivyo, hatukupatiwa orodha ya walionufaika na fedha hizo za kufidia hasara na kulipia mikopo wala utaratibu utakaotumika kwa wafanyabiashara husika kurejesha fedha hizo pindi hali ya uchumi itakapoimarika. Kwa hali hiyo, nimeshindwa kujiridhisha kuhusu uhalali wa malipo hayo na urejeshwaji wake
  utakavyokuwa. CAG – L.S Utouh


  Hii si EPA ya pili?
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  watu walifungua makampuni asubuhi na jioni wakachukua pesa hizi toka benki............
   
 3. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
   
 4. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii ripoti imetoka juzi tu na wewe unasema hizi ni habari za zamani.. tukueleweje?
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  We vipi, ufumbuzi upi tuliupata, ufumbuzi wa pesa kutumika visivyo ni kurejeshwa kwa pesa husika sasa hilo limefanyika lini? Halafu kurudia kulizungumza ni sawa kabisa si unajua hatuna madawati, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu nk. fedha hizi zingetumika kwa mambo mengi tu kama serikali ingekuwa makini, unachojaribu kufanya wewe ni kuzima moto wa petrol kwa mafuta ya taa.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo magamba ambayo ccm inabidi ijiue ili yatoke!
   
 7. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Anayetetea au kulazimisha tusiseme dhambi, ni MWIZI. Gamba Jipya sawa na CCM without old gamba, ni sawa na genge la mafisadi.

  Gamba jipya kama jina lako, tupe matokeo ya hizo habari za zamani, tunazitaka sasa kwa ajiri ya kupambana na mafisadi wa sasa.   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu anayetaka utata uliozunguka malipo haya ya mabilioni ya fedha za wananchi uwekwe chini ya zuria ana lake, lakini kwa wengi wetu tunataka vyombo husika vifuatilie tuhuma hii na wananchi wapewa taarifa juu ya jambo hilo mapema iwezekanavyo.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Gamba Jipya nalo linatakiwa kuvuliwa tu, amejadili lini na ni mgeni humu au alibadilisha I'd ndio kajivua gamba?
   
 10. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unauhusiano na Chama cha Gamba nini? Umetumwa kuja kuvuruga? Umejiunga juzi tu (16th April, 2011), umezisoma lini hizi taarifa? Gamba lako jipya halibadili mawazo na sumu yako. Tumekushitukia.
   
 11. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nina wasiwasi na JK na familia yake walichukua fedha hizo na kufanyia kampeni. Kama sivyo, basi JK achukue hatua kali dhidi ya waliotumia viabaya pesa hizo.
   
 12. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii report tumeshaizungumzia sana hata kabla ya kutoka ofisini kwa CAG na baadae Zuberi aliipeleka bungeni tukaizungumzia tena, na waziri mkubwa akatoa majibu mazuri tuu na wabunge wakamwelewa, naombeni tuongelee mambo mapya yenye kuleta maendeleo wakuu.

  Mleta mada inaonekana siyo mfuatiliaji wa wanayojiri Tanzania.
   
 13. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mmezizungumza na nani? Ufumbuzi wake ni upi? tunataka utuambia mmechukua hatua gani kwa hao mafisadi wenu waliozitafuna pesa hizo maana najua zimeliwa na watu wanaojichubua magamba.
   
 14. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo siyo mtoa mada, tatizo lipo kwako wewe unayechanganya madesa. Ripoti iliyopelekwa Rais mwishoni mwa mwezi Machi 2011 na kisha kupelekwa bungeni wiki mbili tu zilizopita wewe unasema mlishaizungumzia zamani. Wapi mlizungumza, UV-CCM, NEC au kwenye CC magamba? Majibu ya kueleweka ni yapi sasa maana wengine hatujapata taarifa hizo?
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  We mwanaGAMBA wewe!
  Nani aliyesema hizi ni habari za zamani?
  Ebu retrieve thread iliyoongelea suala hili siku za nyuma!
  Nyie WAPURUZI tushawastukia, acha watu waweke hadharani sehemu ya magamba ambayo hamjayavua bado!
  SUBIRI ZIWEKWE NA PAYMENT VOCHA HAPA ndiyo utajua kuwa TUNAMAANISHA TUNACHOSEMA!
   
 16. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mkuu hapa JF hauna hata siku 3, uliizungumzia jukwaa gani?
  maendeleo gani yatapatikana ikiwa fedha zinapotea bila maelezo ya kuridhisha..
   
 17. M

  Maimai Senior Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .... Pesa iliingizwa kwenye benki moja kubwa ina nembo yake ya rangi ya ccm baadaye ikachomolewa. Magumashi ya kampeni. Tufunge mjadala please. said mwema amchunguze shemeji????
   
 18. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Haya ni maajabu sana Ed, inauma sana pale mjasiriamali anapokwenda benki kuomba hata 'overdraft' akamatimize order yake na kunyimwa.
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Sijui tufanyeje na hawa wezi!
   
 20. N

  Ngo JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
Loading...