Wizi mpya BOT

Hizi figures zina relation gani?
  1. KAGODA ilichukuwa 40BN
  2. Watuhumiwa wa EPA walirudisha 50bn zikapelekwa TIB. Peter Noni akateuliwa CEO hapohapo
  3. Ule mradi wa power tillers fake ulipewa 50bn
  4. CCM wakati wa kuelekea uchaguzi walidai wanahitaji 50bn za kampeni
  5. Sasa hizi 48bn
 
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
Gamba Jipya
Join Date : 16th April 2011
Posts : 31
Thanks:
0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0

Wewe ni gamba jipya au EPA mpya, na hii habari uliizungumzia wapi na kupata ufumbauzi sababu hapa umejiunga juzi tu. Tuambie Jukwaa uliloizungumzia na ufumbuzi wake.
 
Nahic sasa kuna mawakala wa mafisadi jamvini wenye mission kamili ya kuharibu mijadal inayohusu ufisadi na mmoja wao ni Gamb jua jipya aliyejiunga juzi na leo anasema walishajadili muda mrefu sana hii mada.

Naomba tuwaelewe na tuachane nao.
 
Gamba Jipya,
Labda bado hujasoma Taarifa ya CAG. Siyo hiyo tu ya Stimulus package tu. Fedha za zilizokuwa zinahojiwa ni zile tu zilizotoka kwenye Own Source, ambazo CAG ameshindwa kuziona zilienda wapi, na Serikali haikutoa ushirikiano kwa kumpa Listi ya Makampuni au atu waliopewa fedha hizo. Kumbuka Stimulus package ilitangazwa na JK siku mbili tu kabla ya Mkutano wa Bunge wa Bajet, na Serikali tulipoishaiuri utaratibi Transparent kama zilivyofanya nchi zingine ambazo tuliwapa mifano hai walikataa katakata. Hivyo fedha zote zinazohojiwa hapa ni zote 1.7 trillioni ambazo tunadai Serikali itoe listi yote ya waliopewa Fedha hizo.
Katika Ukurasa wa 127 wa Ripoti ...kwa mwaka unaoishia 30 June,2010 (Hesabu Serikali Kuu) CAG anahoji pia 70 Billioni zilizopelekwa TIB kwa ajili ya Kubadilisha TIB kutoka Taasisi ya Fedha na kuwa Benki inayoshughulikia Kilimo. Hadi anawasilisha Taarifa yake Bungeni, March 2011, CAG ameshindwa kuona fedha hizo i) Ziko Akaunti gani ndani ya TIB? ii) Hajaonyeshwa dondoo za ripoti ya fedha kuonyesha mapokezi na urari wa mfuko huo iii) Mkataba na TIB kuonyesha makubaliano ya jinsi fedha hizo zinavyotakiwa kutumika iv) Kibali cha Baraza la Mawaziri kuonzisha Benki hiyo ya Wakulima. Isitoshe inadhaniwa kuwa 70 Billioni yote au sehemu yake kubwa inatokana na Fedha zilizokuwa zikirejeshwa kutokana na EPA. Hii ni hali ya hatari sana. Tena 2010 ilikuwa mwaka wa uchaguzi. Kuna maswali mengi ya kujiuliza.

Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
 
Sijui tufanyeje na hawa wezi!

mkuu tunahitaji watu wa kujitoa mhanga tu.. au snipers! this wont stop unless we do something about it.

hizi habari zishaniharibia siku yangu, hivi hawa watu hawaridhiki? hela zote hizi wanazitumia wapi?
 
Gamba Jipya,
Labda bado hujasoma Taarifa ya CAG. Siyo hiyo tu ya Stimulus package tu. Fedha za zilizokuwa zinahojiwa ni zile tu zilizotoka kwenye Own Source, ambazo CAG ameshindwa kuziona zilienda wapi, na Serikali haikutoa ushirikiano kwa kumpa Listi ya Makampuni au atu waliopewa fedha hizo. Kumbuka Stimulus package ilitangazwa na JK siku mbili tu kabla ya Mkutano wa Bunge wa Bajet, na Serikali tulipoishaiuri utaratibi Transparent kama zilivyofanya nchi zingine ambazo tuliwapa mifano hai walikataa katakata. Hivyo fedha zote zinazohojiwa hapa ni zote 1.7 trillioni ambazo tunadai Serikali itoe listi yote ya waliopewa Fedha hizo.
Katika Ukurasa wa 127 wa Ripoti ...kwa mwaka unaoishia 30 June,2010 (Hesabu Serikali Kuu) CAG anahoji pia 70 Billioni zilizopelekwa TIB kwa ajili ya Kubadilisha TIB kutoka Taasisi ya Fedha na kuwa Benki inayoshughulikia Kilimo. Hadi anawasilisha Taarifa yake Bungeni, March 2011, CAG ameshindwa kuona fedha hizo i) Ziko Akaunti gani ndani ya TIB? ii) Hajaonyeshwa dondoo za ripoti ya fedha kuonyesha mapokezi na urari wa mfuko huo iii) Mkataba na TIB kuonyesha makubaliano ya jinsi fedha hizo zinavyotakiwa kutumika iv) Kibali cha Baraza la Mawaziri kuonzisha Benki hiyo ya Wakulima. Isitoshe inadhaniwa kuwa 70 Billioni yote au sehemu yake kubwa inatokana na Fedha zilizokuwa zikirejeshwa kutokana na EPA. Hii ni hali ya hatari sana. Tena 2010 ilikuwa mwaka wa uchaguzi. Kuna maswali mengi ya kujiuliza.

watu wengi walisema haya wakati wanatoa hizo pesa za stimulus. Mwaka wa uchaguzi + serikali inamwaga pesa bila ufuatiliaji = EPA number 2. Tumechoka na ccm, hawana uwezo wa kuongoza hii nchi! Dr Slaa tunaomba wabunge wa Chadema wachakarike zaidi kutoa hizi data kwa wananchi. Pia wapeni madiwani hizi information zisambazwe kwenye grass root levels. Na ikiwezekana, badala ya kusema ni Tri 1.7 zimeibiwa, badilisheni na kuwapa mifano hao. Kwa mfano mkiwa kwa Wamasai semeni ni sawa na ng'ombe wangapi, nk!
 
Unauhusiano na Chama cha Gamba nini? Umetumwa kuja kuvuruga? Umejiunga juzi tu (16th April, 2011), umezisoma lini hizi taarifa? Gamba lako jipya halibadili mawazo na sumu yako. Tumekushitukia.

Aha ahaha ahahah ahahaha:

Chama Cha Gamba! - CCGamba - dah
 
Dawa ni CAG kupewa meno ya kuwashtaki na kuwa-prosecute mahakamani wote anao wakuta katika ukaguzi wake kwamba wametuibia fedha.Kuendelea kutoa taarifa tu mwaka hadi mwaka bila kushtaki haina maana, na ndio maana wizi unaendelea kama kazi.

apewe na nani sasa mkuu!?hawawezi kujilipua hawa coz wanajua hawasafishiki.wakimpa hayo meno ni sawa na suicide!dah,nchi hii bwana,unaweza kuutamani uraia wa ivory coast!!
 
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.

Tukubali tusikubali huyu ni mmoja wa wanachama wa chama cha magamba alotumwa kuja kuvuruga jamvi, sasa wameanza kuvamia jamvi rasmi.... mods fukuza hawa watu wanaotaka kupotosha ukweli!!!!:alien:
 
Hii ni hoja ya msingi, tuambiwe haya mabilioni ni makampuni gani yalichukua na ni vigezo gani vilitumika na lini watazirejesha. Hapo hamna cha zamani, labda tu kama watu wanagoma kuuona ukweli, wanagoma kutumia ubongo kufikiri na badala yake wanatumia utumbo!
 
RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI MWAKA ULIOISHIA TAREHE 30 JUNI, 2010 inasema

5.9 Kukosekana kwa orodha ya waliolipwa kiasi cha Sh.48,000,270,000 kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi
Serikali ililipa kiasi cha Sh. 48,000,270,000 katika Benki Kuu ya Tanzania kama sehemu ya mchango wake wa kuchochea ukuaji wa uchumi ili kukabiliana na msukosuko wa uchumi ulioikumba dunia. Hata hivyo, hatukupatiwa orodha ya walionufaika na fedha hizo za kufidia hasara na kulipia mikopo wala utaratibu utakaotumika kwa wafanyabiashara husika kurejesha fedha hizo pindi hali ya uchumi itakapoimarika. Kwa hali hiyo, nimeshindwa kujiridhisha kuhusu uhalali wa malipo hayo na urejeshwaji wake
utakavyokuwa. CAG – L.S Utouh

Hii si EPA ya pili?

Duh kweli ww ndio nimegundua ni maimuna wa kuhusiana na masuala ya auditing. Ki utaratibu auditor (CAG) anapo rise query kinachotakiwa ni Serikali kutoa majibu yake (yaani Government Response) , baada ya hapo sasa CAG hufuatilia yale majibu yaliyotolewa yako sahihi pamoja na ushahidi wa nyaraka, sasa kama nyaraka hajapewa huwezi kusema kuna wizi, je akipewa na zikawa sahihi utasemaje ? fikirieni acheni kujibu kisiasa haya ni masuala ya weledi wa mambo ya hesabu na ukaguzi
 
Kwa maneno haya sina shaka kabisa kwamba na wewe umechotewa.Lakini kumbuka kwamba za mwizi ni arobaini.
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
 
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
Tukumbushe ufumbuzi wake ulikuwaje; ikiwezekana tutajie hayo makampuni yaliyolipwa fedha hizo.
 
sishangai kusikia kuwa hizo hela hazifahamiki zilikoenda, chini ya uangalizi wa makamanda kma rostam chini uangalizi wa ssm haya yamekuwa ni magumashi ya kawaida mno kwao, kwani yale mabillion ya kila mkoa yalienda wapi? nani anayejua yale mabilioni ya EPA yaliyosemekana yamerudishwa yalitumika vip. jamani tusijifanye cc ni wagen tz
 
Gamba Jipya
Join Date : 16th April 2011
Posts : 31
Thanks:
0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0

Wewe ni gamba jipya au EPA mpya, na hii habari uliizungumzia wapi na kupata ufumbauzi sababu hapa umejiunga juzi tu. Tuambie Jukwaa uliloizungumzia na ufumbuzi wake.
Huyu nadhani ni MS
 
Back
Top Bottom