Wizara ya Mipango na Tume ya Mipango anzeni na hili

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Mwaka 2016/17 Serikali ikifanya maamuzi rasmi ya kuhama Dar es Salaam na kuhamia Dodoma.

Uhamaji huu umepelekea majengo mengi sana ya Jiji la Dar hasa katikati ya Jiji na maeneo ya Jirani kuwa matupu. Mengi hayana wapangaji na kiukweli ni kama yameachwa tu!

Sote tunafahamu, Dar es Salaam ni jiji letu la Kibiashara ila kusema kwelI bado hatujaliweka kuwa la kibiashara kweli. Kwa sababu hii nataka kuwapa mawazo ya namna gani ya kulifanya lile jiji kuwa kitovu cha Uchumi katika Ukanda huu wa Mashariki wa Afrika.

1. Mje na mapendekezo kwa Serikali ya namna majengo yaliyoachwa kama Ofisi yanaweza kubadilishwa kwa matumizi ya makazi ( Apartments). Sote tunajua kuna demand kubwa sana ya nyumba katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa wageni hasa wahindi, Waarabu na Wazungu wanapenda sana kukaa katikati ya jiji na maeneo ya karibu. Hivyo leo hii majengo yale yakiboreshwa na kufanywa kuwa apartments, nchi itaingiza mapato makubwa sana na ule mji utazidi kuboreka na kuwa bora zaidi. Kwetu hatutakuwa wa kwanza kufanya hivi hata Marekani linafanyika hasa kwenye miji mikubwa kama New York.

Kama wenzetu wanaanza kuwaza kufanya na kufanya basi na sisi tufanye pia

2. Mtengeneze mpango wa kufanya Watu wavunje makazi holela Dar es Salaam na kujenga majengo ya uwekezaji kama apartments na majengo ya Biashara ili sio tu kuliboresha lile jiji ila kulifanya kuwa Jiji la Utalii wa Starehe kama ilivyo Dubai.
Kwenye hili mnaweza kuja na mpango wa miaka 10-15. Kampuni au mtu aweze kupata nafuu za kikodi kwenye uwekezaji wa miondombinu atakaoufanya na awekewe utaratibu wa kununua hata mtaa mzima na kuuboresha kwa kujenga majengo ya kisasa kama malls na vitega uchumi vingine bila kusahau apartments. Hili litaliboresha sana jiji la Dar na kwa miaka ijayo litavutia watu wengi zaidi kuja kutumia hela zao na kuliingizia taifa mapato makubwa sana.

Screenshot_20230726-101224_Chrome.jpg


Uzi Utaendelea kuhusu Sekta zingine kwa siku zijazo.........
 
Kwa hiyo unataka kusema?
Kama unakumbuka Kurasini ya zamani kuanzia Shimo la Udongo hadi DSA Siku hizi TIA utanielewa vizuri

Ndio Sababu Dr Kitima alisema St Joseph Cathedral inaweza kubomolewa kupisha Bandari

Unaweza kudhani Shujaa Magufuli alipenda Sana kuhamia Dodoma lakini labda ililazimu tu😀😀

Mungu wa mbinguni akubariki!
 
Kama unakumbuka Kurasini ya zamani kuanzia Shimo la Udongo hadi DSA Siku hizi TIA utanielewa vizuri

Ndio Sababu Dr Kitima alisema St Joseph Cathedral inaweza kubomolewa kupisha Bandari

Unaweza kudhani Shujaa Magufuli alipenda Sana kuhamia Dodoma lakini labda ililazimu tu😀😀

Mungu wa mbinguni akubariki!
Bwashee. Tatizo lako unawazaga mbali sana
 
Back
Top Bottom