Mavipunda
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 6,916
- 7,522
Wakati Mhe. Rais anafungua mradi wa maji kule Kigamboni hivi karibu, Ndugu Juma Aweso alitamka mbele ya Mhe.Rais kwamba kuanzia siku ile jiji la Dar es Salaam linapata maji kwa 100%. Alitoa kauli hiyo huku akijifananisha na Kocha wa Yanga alivyopindua meza Tunis.
Wakati wa hotuba yake mama Samia nae alirudia kauli hiyo ya jiji kupata huduma ya maji kwa asilimia mia na alimpamba sana kwa sifa Ndugu Awesu.
Lakini kuanzia siku ile shida ya maji katika jiji la Dar ndio iliongezeka makali maradufu. Wakaazi wa Sinza, Kijitonyama, Mikocheni, Mbezi Beach, Tegeta n.k walikuwa wakipata maji kwa mgao kila baada ya siku tatu lakini kuanzia Ijumaa ile hadi leo hata huo mgao kwao umekata.
Kama Mhe. Rais ana mifumo yake ya kupata feedback basi afuatilie atajua ukweli wa haya tunayoongea.
Inawezekana DAWASA wanampotosha Awesu au kuna hujma za kimkakati dhidi ya Mhe. Rais.