Wizara ya Elimu huku hali ni mbaya! Watoto mnawatengenezea Ulemavu

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,573
10,566
Watoto siku hizi wamekuwa kama PUNDA kwanini Waalimu wanawabebesha watoto mabegi mazito na makubwa kuliko hata kilo zao??

Je hakuna ratiba maalumu ya masomo?

Hili tatizo lipo kwa ngazi zote Msingi mpaka Sekondari.

Vitu vinavyobebwa ni kama ifuatavyo
1_ Sweta
2_Chupa la maji
3_Vitabu si chini ya nane
4_Madaftari kumi na kuendelea
5_Kompasi/Mkebe
6_Rangi boksi zima + Peni + Penseli
Na vitu vingine

Ukipiga mahesabu hapo si chini ya kilo 8 mtoto anabeba mgongoni na huyo mtoto:
  • Adandie daladala.
  • Huyo huyo atembee umbali mrefu.
  • Huyo huyo ashinde bila kula huko shule.
  • Huyo huyo awahi kuamka asubuhi (Zingatia mzigo anaozunguka nao mgongoni siku nzima)

Niulize swali: Hivi haiwezekani kukajengwa cabinets za kuhifadhi madaftari ya darasani huko huko shule?

Maswala ya Homework vitengenezwe vitabu/Daftari maalumu bila kumlazimu mtoto kutembea na midaftari mingi?

Hivi hakuna sophisticated mechanism itakayowaokoa hawa watoto?

Watoto wanatoka vibiongo wanaumwa migongo na kuchoka mno.

Ila sishangai maana hata waalimu nao wanamapochi makubwa wamejaza Kashata, ubuyu na Kababu hawawezi kuwa na huruma.

punda_ideology
 
IMG_3425.jpg
 
Nilijaribu kuwauliza wanafunzi wachache hasa wa hapa Dar kwanini wanabeba mabegi mazito ambayo yamejaa madaftari ,jibu walilonipatia ni kwamba siku zote ratiba za masomo uwa zinabadilika kutokana na walimu kuwa na udhuru nyingi.changamoto walimu hawafuati ratiba .
 
Hilo ndio changamoto kubwa. Na ujinga wa kuunganisha notes kuanzia za form one mpk four.

Sas imagine counter quire 2 liungwe mara 4 hilo ni somo moja. Ukipiga kwa masomo 10 huyo mtu anabeba kilo si chini ya 30.
 
Watoto siku hizi wamekuwa kama PUNDA kwanini Waalimu wanawabebesha watoto mabegi mazito na makubwa kuliko hata kilo zao??

Je hakuna ratiba maalumu ya masomo?

Hili tatizo lipo kwa ngazi zote Msingi mpaka Sekondari.

Vitu vinavyobebwa ni kama ifuatavyo
1_ Sweta
2_Chupa la maji
3_Vitabu si chini ya nane
4_Madaftari kumi na kuendelea
5_Kompasi/Mkebe
6_Rangi boksi zima + Peni + Penseli
Na vitu vingine

Ukipiga mahesabu hapo si chini ya kilo 8 mtoto anabeba mgongoni na huyo mtoto:
  • Adandie daladala.
  • Huyo huyo atembee umbali mrefu.
  • Huyo huyo ashinde bila kula huko shule.
  • Huyo huyo awahi kuamka asubuhi (Zingatia mzigo anaozunguka nao mgongoni siku nzima)

Niulize swali: Hivi haiwezekani kukajengwa cabinets za kuhifadhi madaftari ya darasani huko huko shule?

Maswala ya Homework vitengenezwe vitabu/Daftari maalumu bila kumlazimu mtoto kutembea na midaftari mingi?

Hivi hakuna sophisticated mechanism itakayowaokoa hawa watoto?

Watoto wanatoka vibiongo wanaumwa migongo na kuchoka mno.

Ila sishangai maana hata waalimu nao wanamapochi makubwa wamejaza Kashata, ubuyu na Kababu hawawezi kuwa na huruma.

punda_ideology
Umesahau michango kila siku na cha ajabu zaidi juzi darasa la saba Dar wamefanya Mock mkoa lakini tumechangishwa wazazi kugharimia mock hiyo mfano mzuri shule ya msingi Kizinga Mbagala wilaya ya Temeke. Wamepata mbinu mpya wanawaita wazazi wanawaeleza sababu kibao za kuhalalisha hii michango yao. Tumemjulisha Afisa Elimu mkoa kuhusu kadhia hii hakuna jibu alilotoa. Na lengo lao tumelifahamu kumuharibia mama yetu tu. Maana kiasi cha pesa kinachopelekwa mashuleni ni kilekile tena sasa hivi kuna nyongeza kidogo lakini michango kila siku. Kwanini enzi za JPM kiasi hiki kiliwezekana leo kimeongezeka kishindikane. Prof Mkenda na Waziri wa Tamisemi liangalieni hili.
 
Kuna michango yakijinga jinga.

Eti mchango wa Ulinzi! Hivi kweli serikali haijatenga bajeti ya ulinzi? Imagine Tsh 500 kwa kila mwanafunzi.

Ujinga mwingine ni huo wa kukusanya hela za mitihani wamefanya mtaji kila wiki mitihani watoto hawana muda wa kupumzika kazi kuwakalilisha tu.

Ina maana serikali haijatenga bajeti ya mitihani ya kupima uelewa kwa watoto?

Ujinga mwingine ni Mtoto aende na Bunda la RIM paper..
 
Back
Top Bottom