Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

witzone2

JF-Expert Member
Jan 14, 2022
780
1,636
Serikali ya CCM imeamua kufanyia tangazo la jirani zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kuwa ni mkubwa mno.

Mimi ni mdau wa elimu, hii sababu sio kweli hata siku moja.. SEMA kwa sababu Serikali yetu haifanyi tafiti za kujua tatizo wao huja maamuzi yao bila kufanya utafiti wa kina.
===

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne, isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi rasmi kutoka kwa mdau husika.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa imeeleza kuwa shule zote ambazo zinatoa huduma ya bweni kwa madarasa yasiyoruhusiwa zinatakiwa kusitisha huduma hiyo ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza mwaka 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji na usajili wa shule uliotolewa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwezi Novemba mwaka 2020.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watoto wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi la nne, huku huduma zinazotolewa kwa wanafunzi hao zikiwanyima fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia zao.

Kulingana na tafiti zilizopo, madhara ya muda mrefu yatokanayo na tabia ya kulaza watoto bweni katika umri mdogo ni watoto kukosa mapenzi kwa wazazi ama walezi na jamii zao na hivyo kushindwa kuwa sehemu ya familia na jamii husika.

Taarifa hiyo ya Kamishna wa Elimu pia imesema kuwa hairuhusiwi kwa shule yeyote kuwa na makambi ya kitaaluma na kuzielekeza shule kuweka mikakati thabiti ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia kalenda za mihula zinazotolewa mara kwa mara na Kamishna wa Elimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi ama walezi wa watoto.

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539134

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539135

waraka-wa-elimu-na-2-mwaka-2023-kuhusu-utoaji-huduma-ya-kulaza-wanafunzi-bweni-kwa-ngazi-ya-el-jpg.2539136
 
Serikali ya ccm imeamua kufanyia tangazo la jiran zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kua ni mkubwa mno...
Kujishusha na kujidharau namna hiyo dhidi ya jirani ni upuuzi. Wakenya ndiyo wameiga kwetu. Sisi tulipiga marufuku mambo hayo kitambo tu.
 
Serikali ya ccm imeamua kufanyia tangazo la jiran zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kua ni mkubwa mno...
Kinachofuata kila mwanaume atalazimika kuoa mwanamke wa kabila lake ili kulinda maadili na lugha kwa watoto.
 
Hii ni shule ya day ya serikali hapo unasemajeView attachment 2533916
Witzone2 hapo umefunga kazi. Suala siyo shule za bweni, ni mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Serikali inatakiwa kufuta mitaala yote inyohusu elimu ya uzazi kwa shule za msingi. maana huko watoto ni wadogo sana. Kwenye mitaala niyo ndiko wanakofundishwa mimba inaigiaje, inaweza kuzuiwa vipi na kama ikiingia inaweza kutolewa vipi (tena bila ridhaa ya mzazi).

Hako ka mchezo ni sehemu ya kuzuia mimba isiingie na hivyo watoto wa kiume nao wanona kumbe hata huko nyuma inawezekana.

Nyimbo za mastaa wetu na video zao zinafundisha nini kwenye jamii?? Halafu tunawapongeza na kuwaita waburudishe kwenye majukwaa!
 
Utampelekaje mtoto wa miaka miwili boarding? Kama upo busy ajiri msichana wa kazi akusaidie kulea hapo hapo nyumbani na awe anamuandaa kwenda shule.
Shida kubwa ya mmomonyoko wa maadili ya watoto ni umasikini sehemu kubwa. Wazazi wako busy sana kuhangaika na kutafuta hela.

Kama ni swala la watoto kulawitiana nitaani ndo kunaongoza kwa sababu watoto wako huru mno.

Kwenye familia zenye uwezo, ulawiti wa watoto hufanyikia majumbani mwao walio wengi eidha kwa kufundishwa na wasichana wa kazi au house boy. Kujifunza kuangalia move za mapenzi muda mwingi wawapo majumbani.
 
Serikali ya ccm imeamua kufanyia tangazo la jiran zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kua ni mkubwa mno...
Huo waraka upo toka zamani ungekuwa unamiliki shule mara nyingi huwa uko kwenye barua ya usajili mkuu
 
Serikali ya ccm imeamua kufanyia tangazo la jiran zetu wakenya kupiga marufuku watoto kuishi shuleni kuanzia darasa la nne. Sababu kuu wanayodai ni mmomonyoko wa maadili shule za bweni kua ni mkubwa mno.

Mimi ni mdau wa elimu hii sababu sio kweli hata siku moja.. SEMA kwa sababu serikali yetu haifanyi tafiti za kujua tatizo wao huja maamuzi yao bila kufanya utafiti wa kina.
Barua iko wapi?
 
Back
Top Bottom