Habari wadau..!
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la 9 September kwamba muda si mrefu lile eneo lote la Kurasini-Temeke lilitwaliwa miaka kibao ya nyuma enzi za JK sasa litaanza kufanyiwa kazi kwa kugeuzwa kituo cha biashara.
Pia maeneo ya karibu yote na hapo kama Machungwa na Mivinjeni kumekuwa na migogoro kati ya wawekezaji wao kwa wao wakigombea maeneo mfano pale Mivinjeni kitu ambacho kimepekekea ugomvi mkubwa sana wa watu kutishiana mapanga ,na baadaye wazee wakaamua kufanya kikao cha kusoma albadili ili kuwaloga wote wanao muhujumu muwekezaji wao wanaomtaka wampatie eneo la kuwekeza baada ya kukidhi vigezo vyote vya utwaaji wa eneo.
Inasemekana kwamba mwekezaji mmoja alifuata taratibu zote za kutwaa eneo,wananchi wakajaza fomu zote wanachongoja ni malipo tu ila sasa kuna watu ndani ya serikali wakishirikiana na mwekezaji mwingine mwenye interest ndio wanaleta figisu figisu baada ya njia za kisheria kugonga mwamba sasa wazee wameamua kutumia majini ,maluani na mashetani kwa yeyote anayewahujumu.