Halima Mdee Aishukia Wizara ya Ardhi Kwa Kutenga Posho Bil.47 Huku Tume ya Ardhi Ikipewa Bilioni 10 Pekee Kushughulikia Migogoro

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,405
49,052
Kwa hili natoa kongole nyingi kwa Halima Mdee..

Ni aibu Nchi imejaa Migogoro ya Ardhi na Ujenzi holela harafu Tume ya Ardhi inatengewa pesa kiduchu na Wanasiasa wanatengeana mabilioni ya posho kwenye Wizara hiyo hiyo..
Huyu Waziri wa hii Wizara hatoshi..
===

1685045739050.png

Hali Mdee akichangia hoja bungeni amesema:

"Migogoro ya ardhi nchi hii Mawaziri na watendaji wa serikali kwenu nyie mnaitumia kama dili la kuzunguka kufanya ziara. Hamna dhamira hata kidogo ya kuhakikisha kuna mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi ili kuhakikisha tunaondokana na migogoro ya ardhi

Leo kamati inatuambia Bilioni 47 ni ya posho na uratibu na kuzurura zurura huko halafu Tume ya mipango ya matumizi bora ya ardhi wanapewa chini ya bilioni 10. This is nonsense, this is lack of seriousness.- Halima Mdee, Bungeni Dodoma.

My Take
Serikali Undeni Wakala wa Mipango Miji na Land administration Tanzania au badilisheni Muundo na majukumu ya tume ya Ardhi Ili ndio washughulike na issues za Ardhi..

Mbona Tarura,Ruwasa nk mumeunda ,huku kwenye Ardhi Kuna kigugumizi gani?
 
Kwa hili natoa kongole nyingi kwa Halima Mdee..

Ni aibu Nchi imejaa Migogoro ya Ardhi na Ujenzi holela harafu Tume ya Ardhi inatengewa pesa kiduchu na Wanasiasa wanatengeana mabilioni ya posho kwenye Wizara hiyo hiyo..
Huyu Waziri wa hii Wizara hatoshi..

My Take
Serikali Undeni Wakala wa Mipango Miji na Land administration Tanzania au badilisheni Muundo na majukumu ya tume ya Ardhi Ili ndio washughulike na issues za Ardhi..

Mbona Tarura,Ruwasa nk mumeunda ,huku kwenye Ardhi Kuna kigugumizi gani?

DONDA NDUGU Ardhi wanauziwa Raia wa kigeni na hakuna monitoring.
MAAFISA wapo ofisini KAZI Yao kuombaomba Rushwa.
wamrudishe lukuvi hiyo wizara huyo anjelina haiwezi.ni wizara inayonuka rushwa kila kona.hakuna msafi kwenye wizara hiyo.raisi amefuta adhabu kwenye kodi ya ardhi lkn ukienda ardhi bado wanakuwekea maadhabu ya miaka ya nyuma kiasi kwamba walipaji wameamua kugoma kulipa na wanasema liwalo liwe.ni ajabu sana inaonekana rais pia hana nguvu ya maamuzi.
 
Njia yeyote iliyotumika,tunangalia content yake..

Bila Nyerere kuwakatalia Wananchi kwenye matokeo ya maoni ya Vyama vingi au hapana hata wewe ungekuwa mwana ccm saizi..
Nyerere hakukubali mfumo wa vyama vingi kwa wema, bali aliujua ukweli kuwa watu walioongozwa na CCM kwa shuruti. Hilo bunge kibogoyo la majizi ya kura halina ubavu wowote wa kusema na serikali ikatii. Yote ni kwasababu serikali inajua ina bunge kiini macho, kutokana na ule uhayawani wa 2020.
 
Kwani wewe umeona Halima Yuko Bungeni Kwa ubaya?
 
William Lukuvi aliiweza sana hii wizara.
Hawa wengine ni shida tu.
Wote ndio walewale hakuweza chochote kama angeweza si migogoro ingeisha,binafsi familia yetu iliporwa kiwanja eneo maarufu na kila tulipoomba kuonana naye alikuwa akitusukumizia kwa kamishna wakati huyo kamishna ni miongoni mwa walioshiriki mchezo mchafu,sema alikuwa mtu wa maigizo kama bosi wake.
 
Back
Top Bottom