Ni kwanini kabla ya Bajeti kila Wizara lazima iandae Semina Elekezi kwa Wabunge?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,053
49,737
Nimepitia Wizara zote waliandaa kile wanaita seminaza kuwajengea Wabunge uelewa. Mfano Afya waliandaa kuhusu Elimu ya Bima ya Afya kwa wote, Madini Wiki ya Stamico, Ardhi Waliandaa kile wanaita Elimu ya Ubia kati ya NHC na sekta binafsi na siku za karibuni Nishati wao Wametia fora Kwa kuwa na wiki ya Nishati iliyoambatana na kugawa mitungi ya gas.

Sasa ni zamu ya Wizara ya Michezo na Sanaa, wao kupitia COSOTA wameandaa semina ya Elimu ya kazi za COSOTA🤣🤣🤣🤣
---

Ofisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA), imetoa Semina kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu na fursa zilizopo katika ofisi hiyo ikiwemo kulinda hakimiliki za Wabunifu.

Semina hiyo imefanyika Mei 30, 2023 katika ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma ambapo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua semina hiyo na kueleza kuwa, semina hiyo ina lengo la kueleza fursa za kibiashara zilizopo katika Hakimiliki pamoja na kuongeza uelewa kuhusu taasisi hiyo.

"Sekta ya Ubunifu nchini inakua siku hadi siku, sisi upande wa Serikali tunandelea kuhakikisha Wabunifu wananufaika na kazi zao pamoja na kuwaelemisha kuhusu umuhimu wa kusajili kazi zao katika ofisi yetu ya COSOTA", amesema Chana."

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa ofisi hiyo, Doreen Sinare amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha Wasanii wananufaika na kazi zao ikiwemo kupata mirabaha kutokana na matumizi mbalimbali ya kazi hizo ambapo amefafanua kuwa mwaka jana Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki ambapo jukumu la kukusanya limeondoka na linakwenda kufanywa na Wabunifu wenyewe kupitia kampuni watakazozianzisha.

Nae, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Kitila Mkumbo alisisitiza kuwa Serikali inakamilisha mchakato wa kusaini Itifaki ya Arusha kwani imechukua muda mrefu na jambo hilo ni la msingi kwani litasaidia kuitangaza nchi na kukuza ubunifu katika eneo la kilimo.

Kwa upande wa wadau wa uzalishaji wa maudhui ya Televisheni Azam Media na DSTV, waliwaomba Wabunge hao kusaidia kukemea vitendo vya wizi wa maudhui sababu kunapoteza mapato ya Serikali na kunadhoofisha uwekezaji uliyofanywa na makampuni hayo.

Mwenye kufahamu hizi ninsemina kweli au ni vilainishi yaani lubricants?
 
Nimepitia Wizara zote waliandaa kile wanaita seminaza kuwajengea Wabunge uelewa eg Afya waliandaa kuhusu Elimu ya Bima ya Afya kwa wote, Madini Wiki ya Stamico,Ardhi Waliandaa kile wanaita Elimu ya ubia kati ya NHC na sekta binafsi na siku za karibuni Nishati wao Wametia fora Kwa kuwa na wiki ya Nishati iliyoambatana na kugawa mitungi ya gas..

Sasa ni zamu ya Wizara ya Michezo na Sanaa,wao Kupitia Cosota wameandaa semina ya Elimu ya kazi za Cosota 🤣🤣🤣🤣

Mwenye kufahamu hizi ninsemina kweli au ni vilainishi yaani lubricants?

Ulishawahi kusoma kitabu cha bajet?
 
Kwenye mawizara Kuna madudu mengi lazima wawaweke wabunge sawa,

Umemskia hata Jana mbunge wa ukerewe akiwasemea wafanyakazi wa Tanesco kuwa wanaenda likizo bila malipo na wafanyakazi wapo kimya tu!
 
Back
Top Bottom