Mimi niwapongeze sana wizara ya afya kwa mageuzi makubwa ya sekta ya afya nchini
1.Kumekua na madaktari bingwa wa kutosha pamoja na vitendea kazi vifaa tiba katika hospitali zetu za mikoa na rufaa
2.Kumekua na uboreshwaji mkubwa wa huduma kwa wagonjwa ( Customer care) siku hizi matusi, kupuuzwa na dharau kwa wagonjwa vimepungua sana kama sio kwisha kabisa
3.Kumekua na ongezeko la watendaji, maboresho ya hospitali, kujengwa kwa hospitali mpya na vituo vya afya kwenye kata zetu na vijiji, hata wale waliokua hawajui hospitali siku hizi wanazijua na wanapata huduma
4.Kumekua na uboreshwaji wa bima ya afya ya taifa. Siku hizi watu wa NHIF hatudharauliki kama awali. Nimeshuhudia mke wa ndugu yangu ambae mumewe ni mwalimu na yeye mama wa nyumbani akifanyiwa upasuaji wa moyo kwa kutumia NHIF bila kikwazo na kupona. Hongera sana MNH
5.Niseme pia kumekua na huduma bora zaidi hospitali za serikali na hospitali na mashirika ya kijamii/dini kuliko hospitali binafsi. Kwakuwa nyie ndio wasimamizi mtusaidie wananchi kujua tatizo ni nini. Kuna hospitali ambazo ukifika mjamzito kujifungua wanakushawishi kufanya upasuaji sijui hili limekaaje kiafya
Ushauri
1.Matibabu ni gharama sana na watanzania wengi hawana uwezo wa matibabu. Tunaomba nyie na NHIF muandae mpango mzuri na rahisi wa kila mtanzania kuchangia bima ya afya. Kama ilivyo Ile 50,400 kwa watoto basi angalieni watu wazima na familia wanaweza lipia kiasi gani kwa kila mwaka.
NHIF wakiweza kuweka njia rahisi na nafuu na kutengeneza mfumo ambao wananchi wengi watakua wanachangia itakua rahisi pia wananchi wachache wanaougua kutibiwa, kuliko sasa wanavyochangisha wananchi wachache na pesa nayo inakua chache kuwatibia wananchi wachache wanaougua
2.Kingine basi niwaombe mshirikiane na wizara ya elimu kuweka somo litakaloweza kubeba maadili na desturi za mtanzania na maisha yake. Vijana wetu siku hizi hawana jando na unyago, wazazi wote wawili wamekua watu wa majukumu mengi huku watoto wakiachwa wanajifunza toka kwenye t.v. na wasaidizi wa nyumbani. Ukitengenezwa mtaala mzuri wa kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne nina uhakika vijana wetu wanaweza kuwa taifa bora sana baadae. Tutaepuka hata watoto kuendelea kuharibiwa kwa kurubuniwa kwani wengi wanakua hawajui na wanafanyiwa mambo mabaya wakiwa wachanga sana hadi inapojulikana inakua basi tena
3.Wizara ya afya na elimu angalieni hizi boarding za watoto wadogo jamani na mkiweza mzifungie kabisa au pale penye ulazima kibali kitoke kwenu. Hainingii akilini mtoto wa miaka 2, 3, 4, 5, hadi 10 kuwa shule ya bweni. Malezi na matunzo ya awali toka kwa wazazi ni muhimu sana kwa mtoto. Wamama na wababa kwanini tunazaa halafu hatutaki kulea? Kweli baba na mama wanampeleka mtoto mdogo bweni, mtoto ambae hata kujifunika shuka usiku au kupiga mswaki hawezi!! Halafu wanakaa nyumbani, wanakula kwa amani kabisa na kulala?? Kuna visa vingi nimekutana navyo vya kuumiza sana toka kwa hawa watoto
Cc
Wizara ya Afya Tanzania