Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wapo hawa? Au Wizara ilianzisha hapa Uzi wa maswali ikautelekeza?...Swali: Wale tuliochanja kabla vyeti vya kielectroniki havijaanza tunapataje vyeti vyetu?
 
Mkiweza futeni gharama ya kupima covid wakati hiyo chanjo ni bure hiyo rapid test mbona Nchi zingine bure tuu kama Botswana hapo tupunguzieni gharama wasafiri...na ukiingia Tanzania lazima ulipie na kupima wakati Nchi nyingi kama mtu katoka kapima na masaa bado yanasoma unapita tuu hapa shida nini au ndio mnakusanya mapato kupitia wagonjwa...
Vv a
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Huu Muongozoo(Program) ya Kujitolea ambao meutoa Kwa wataalum wa afya Utekelezaji Wake Utakuwa Lini ?

Au Mtatoa Tangazoo la Watu Waendee Kujitoleaa au Utapelekeka Barua za Maombi katika Hospitali &Kituo Husika ambacho Ungependa Kujitolea Hapo ,Wizara ya afya au .Baadhi Ya Hospital zitatangaza nafasi chache watu waende zenye Uhaba
 
Manesi muhimbili wana gubu na majibu ya jeuri kwa wagonjwa....
Chunguzeni hilo jambo
 
Watumishi waliopambana dhidi ya UVIKO 19 waliahidiww kulipwa stahiki zako na Naibu Waziri baada ya wiki mbili zitakuwa zimeingia kwenye account zao.

Cha kushangaza ni karibu mwezi Sasa unakatika hakuna chochote. Vipi hapo mnalizungumziaje HILO JAMBO?

Mnataka watumishi hao wawaeleweje?
 
Wakati jpm akiwepo nidhamu mahospitalini ilikuwa ya kiwango cha juu. Sasa hivyo nyodo kibao.huduma hakuna unauliza mtu yuko busy na simu.

Kweli ni maumivu makubwa kumpoteza jpm.
 
Wizara ya afya muwe munatembelea baadhi hospital/ zahanati binafsi mulizowapa leseni kwa lengo la kusaidiana majukumu.

Njooni Hospital ya NDANDA mufanye mdahalo na wagonjwa mutagundua kitu then mutakuja kunishukuru.
 
Kwa unyenyekevu mkubwa nawashukuru Wizara kwa kutoa ajira kwa vijana wenu,vijana wameripot katika vituo vyao vizur kabisa cha kushangaza tangu walipoti had sasa hawajapata hela za kujikimu na mshahara pia hawajapata.
 
Habari waungwana.

Naomba msaada juu ya tatizo Hilo linalonikumba.

Tatizo nikama linavyoonekana katika picha.

Mikono huchubuka na ngoz hutoka Tena bila maumivu.

 
Kuna taarifa za ukweli kuwa watumishi wa huduma za afya hawana imani na chanjo za UVIKO-19 ndio maana wengi wao hawajachanjwa. Hata baadhi wanaotoa chanjo wao wenyewe hawajachanjwa.

Katika hali hiyo ni dhahiri watu wanakuwa na mashaka na hiuo chanjo
 
Wizara ya afya upokeaji wa matibabu wa watoto chini ya miaka 5 bado ni.changamoto watoto wa umri wa chini ya miaka 5 bado upokeaji wa matibabu ni changamoto kwao hata mama mja mzito bado kuna changamoto.namna.ya upokeaji wa matibabu
 
Kuzidi kwa tatizo la ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali (zahanati/vituo vya afya/hospitali) ni wazi kwamba bajeti inayotengengwa kwa ajili hiyo haiendani na upatikanaji wa dawa katika vituo hivyo. Je bajeti hiyo ni halisia au vinginevyo !?

Ukizingatia bajeti hiyo kusemekana kuongezwa kutoka Bilioni 31-275 (787%).
 
Kuzidi kwa tatizo la ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali (zahanati/vituo vya afya/hospitali) ni wazi kwamba bajeti inayotengengwa kwa ajili hiyo haiendani na upatikanaji wa dawa katika vituo hivyo. Je bajeti hiyo ni halisia au vinginevyo !?.....Ukizingatia bajeti hiyo kusemekana kuongezwa kutoka Bilioni 31-275 (787%).
Hakuna mwaka bajeti Tz ikajitosheleza..hua ni njanja janja tu kuwaongopea watz...ilihali ukweli unajulikana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wizara ya Afya angazieni Hospitali ya wagonjwa wa Akili Mirembe Dodoma inaihujumu Serikali vibaya sana. Unakuta Mtumishi wa Serikali aliachakazi kwa Maksudi akatoweka kwenda Sekta Binafsi let say mwaka 2011 hukooo.

Baada ya kutoweka bila taarifa Serikali ilimlipa malipo hewa labda miezi 6 au hata mwaka mzima ndipo akabainika kuwa ametoweka na hatimae anafutwa kwenye Kitabu cha Mshahara. Sasa Mambo yakienda kombo huko sekta binafsi baada ya miaka 10 au zaidi.

Mtumishi huyu kwa kushirikiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Mirembe wanatengeneza Vyeti na Nyaraka kuwa kwa Kipindi chooote hicho Mtumishi huyo alikuwa Kichaaa kafungiwa Hospitalini hapo akiwa Mgonjwa wa akili na sasa amepona.

Huu uhuni Unaendelea mpaka leo na kesho na Utaendelea kuitafuna Serikali. Mwisho wa siku Huyo mtumishi magumashi atarejeshwa kazini na kulipwa Mishahara ya miaka 10 au zaidi ambayo alikuwa Mirembe hewa.

Wizara ya Afya hili liko wazi, wasilianeni na Ofisi ya Rais Utumishi wawape uhalisia wa huu Uhuni na Uhalifu wa Mchana wa Watumishi wenu suala hili linaichafua Wizara na kuiingizia Hasara Serikali. Over
 
Back
Top Bottom