Wizara ya Afya msimwangushe Rais Samia

Mpingamkoloni

Member
Feb 14, 2021
13
32
Baada ya Rais Mhe. Samia Suluhu na Waziri wa Fedha Mwigulu kutoa pesa za IMF kwa manunuzi ya vifaa mbalimbali hospitali za mikoa kwa nia ya kuboresha Afya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya alikasimu mamlaka ya kununua vifaa hivyo kwa baadhi ya taasisi zilizopo chini yake. Lilikuwa wazo jema kabisa.

Inadaiwa jambo hili toka kwa katibu mkuu wizara ya afya halikupokelewa kwa mikono miwili na watumishi wa Wizara ya Afya ambao walitegemea kutumia mwanya huu wa manunuzi kula kwa urefu wa kamba yao. Mfano awali wataalamu wa radiolojia wa Wizara ya Afya walitenga pesa kubwa kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya radiolojia. Ingawa hawa wataalamu wa radiolojia wa Wizara ya Afya ndio waliandaa bajeti ya manunuzi ya vifaa hivi, kwa nyakati tofauti Wizara ya Afya ilikuja kutoa miongozo kwa bodi za uzabuni za taasisi zilizokasimishwa manunuzi haya, zikiwa na makadirio ya bei za chini zaidi ya kile walichokitenga awali, ikidai uchunguzi unaonesha bei ya vifaa kuwa chini saana ya bajeti waliyotenga awali. Sasa unajiuliza bajeti waliyotenga awali walitoa wapi? Je, walijua bei ila waliweka pesa yao juu?

Hadi sasa taasisi zote zilizokasimishwa manunuzi zimemaliza taratibu za manunuzi (baada ya kulazimishwa kurudia mara kadhaa na Wizara ya Afya), na wazabuni walioshinda wanasubiri mikataba. Ajabu sana waradiolojia wa wizara ambao wana elimu ndogo, wamekuwa wakichelewesha michakato kwani kampuni waliyotaka ipate kazi, haikufanikiwa kwa kiwango walichotaka.

Hivi hao waradiolojia wana elimu gani na uzoefu gani wa kuweza kuyachezea maamuzi ya bodi za manunuzi ya taasisi mbalimbali? Halafu kwanini hawataki kuwasiliana na wenyeviti wa bodi za manunuzi au wakurugenzi wa taasisi ila wanawasiliana kwa siri na wakuu wa manunuzi? Hivi Wizara ya Afya kama wanaona waliowakasimisha manunuzi wamekosea si wangesitisha hili zoezi na kufanya manunuzi wenyewe? Mbona wanaingilia sana taratibu huku wakionesha wazi upendeleo kwa kampuni inayosambaza ile brand ya ujerumani na yule dada anayepaka rangi nywele?

Kumekuwa na mahusiano yenye shaka kati ya wasimamizi wa radiolojia wa wizara, na wakuu wa idara za manunuzi wa taasisi, wakitengeneza mapungufu ya kufikirika ya mashine za wazabuni zilizoshinda kusambaza scanner huku wakikwepa kutoa au kuomba taarifa toka kwa wakurugenzi wa taasisi zilizokasimishwa manunuzi na au hata wenyeviti wa zabuni. Nia kubwa ni kuhakikisha huu mchakato ulipofikia sasa haufanikiwi kwa maeneo ambayo wameshinda watu wasio wao. Wengine wanahisi labda wanatengeneza mazingira walioshinda zabuni wajiongeze.

Mheshimiwa Rais, nikuthibitishie kwamba kufikia Mei scanner zitakuwa hazijafungwa hospitali za mikoa, na watakaokuangusha ni viongozi wote wa wizara ya afya ukianzia na katibu mkuu afya, idara ya fedha, wasimamizi wa mradi wa imf wizarani, wasimamizi wa manunuzi wa wizara na waradiolojia wa wizara.

Tunajua nguvu zote zinazotumika ili kumpa kazi yule mhindi wa siemens.
 
Asante kwa whistleblowing. Mamlaka husika watafanya uchunguzi wa unachokisema na kulifanyia kazi.
 
Nilifuatilia ile taarifa ya mwalimu wangu - Katibu Mkuu Prof. Makubi. Nina shauku sana kujua utekelezaji wake.. kwa uchache nakumbuka CT scans kwa Hospitali zote za rufaa za mikoa, MRI hospitali za Kanda , Mtwara, Mbeya, Chato. Pamoja na mambo méngine mengi sana. Alisisitiza mwisho wa utekelezaji ni June 2022... Ninasubiria mrejesho kwa hamu sana.. Wizara ya Afya Tanzania
 
Kwa nini unasema wasimuangushe Rais? Sema wasiangushe nchi.

Back
Top Bottom