Wizara ya Afya kutumia Tsh. Trilioni 1.3 kwa mwaka 2024/25. Tsh. Bilioni 632.2 ni matumizi ya kawaida

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,890
12,144
Wizara ya Afya imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. Trilioni 1.31 itakayotumika kwa mwaka 2024/25 ambapo Tsh. Bilioni 632.26 (48%) ya Bajeti zitaenda katika Matumizi ya Kawaida ikiwemo Mishahara na Matumizi Mengineyo

Pia, Wizara itatumia Tsh. Bilioni 679.57 (52%) ya Bajeti katika Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya Fedha hizo, Tsh. Bilioni 416.25 ni Fedha za Ndani na Tsh. Bilioni 263.31 ni Misaada na Ufadhili (Fedha za Nje).


BAADHI YA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTIKI NCHINI YAMEFIKIA USUGU WA 56.1%
Ufuatiliaji wa matumizi ya Dawa za Antibiotiki ngazi ya Hospitali kwa kutumia WHO Point Prevalence Survey umeonyesha matumizi ya Dawa hizo kwa Wagonjwa waliolazwa ni wastani wa 62.7% hadi 87% wakati kiwango cha Shirika la Afya Dunia (WHO) kinaeleza isizidi 30% ya matumizi ya Antibiotiki kwa Wagonjwa wanaoenda kutibiwa.

Utafiti huo umefanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wanaohusika na usugu wa Dawa pia utafiti umehusish baadhi ya Dawa za Antibiotiki kuona kama zinaweza kutibu vimelea (Antibiotic Susceptibility Testing).

Tathmini kupitia mfumo huo imeonesha kuna matumizi makubwa ya Dawa za Antibiotiki Nchini na baadhi zimefikia usugu wa 56.1%.

Waziri Ummy Mwalimu amesema Wizara imejipanga kupambana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya matumizi holela ya dawa kwa kutoa elimu kwa Wananchi kwa kuja na kampeni itakayozinduliwa Mei 25, 2024 yenye kauli mbiu ya “HOLELA HOLELA ITAKUKOSTI”.


Wajawazito 43,323 walibainika kuwa na maambukizi ya VVU (Julai 2023 - Machi 2024)
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha jumla ya Vituo 7,830 sawa na 96% ya Vituo 8,164 vinavyotoa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto viliweza kutoa huduma za kuzuia Maambukizi ya VVU na Kaswende kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Jumla ya Wajawazito 1,453,235 sawa na 97.4% ya Wajawazito 1,492,931 waliohudhuria Kliniki walipimwa VVU katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 ikilinganishwa na Wajawazito 1,627,685 sawa na 98.9% ya Wajawazito 1,645,417 waliopimwa katika kipindi kama hicho Mwaka 2022/23.

Wajawazito 43,323 sawa na 2.98% ya Wajawazito wote walibainika kuwa na maambukizi ya VVU kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024 ikilinganishwa na Wajawazito 47,475 sawa na 2.85% waliobainika kuwa na maambukizi ya VVU kwa kipindi kama hicho Mwaka 2022/23.
 

Attachments

  • BUDGET%20SPEECH%20-%20FINAL%20AFYA%202024-25.pdf
    2.7 MB · Views: 2
Kwamba machawa walioandaa speech hawajui kama kwa sasa ni Waziri wa Nishati
Screenshot_20240513-154315.jpg
 
Back
Top Bottom