Mgoyangi
Senior Member
- Feb 6, 2008
- 184
- 9
Linapokuwa suala la dawa za ARV ambazo hutolewa bila malipo kwa walengwa, kinakuja kichekesho. Kwanza wafamasia wanasema kuna uwezekano mkubwa watumiaji wanatumia dawa hizi chini ya dozi wanayotakiwa na hivyo kukamilisha safari ya kuviofanya HIV kuwa sugu dhidi ya dawa hizi. hapa wagonjwa watalazimika kutumia dawa zinazoitwa second line drug ambazo nazo ni aghali mno, ambapo kampuni zinazotengeneza zinadai kuuza kwa zaidi ya $1000 kwa dozi ya mwaka. hapa tena inalengwa Richmond nyingine maana hata waziri wao hapigi Kelele. Cha kushangaza ufisadi ndani ya wizara hii kuhusu manunuzi haujavaliwa njuga.
Kingine ni kuwa ovedose walengwa na hivyo kuharakisha vifo vyao badala ya kuvirefusha.
Kiini cha yote haya ni Dawa zinazotolewa na MSD ambazo hufika vituoni zikiwa na sawa na kuwa zimekwisha muda wake wa matumizi. na pia Tabia ya MSD ya kutawanya dawa ambazo, badala ya kuwa kidongo kimoja chenye uzito unaotakiwa, wao sijui kwa rushwa ama misingi gani, wanasambaza dawa amba zina ujazo mdogo mdogo na hazipo pamoja, hivyo ngoma inakuja kwenye mahesabu ya kutafuta dozi kulingana na uzito, ambayo yanahitaji mfamisia, ambao kimsingi hawapo katika hospitali nyingi za JK, na badala yake zinapigwa hesabu kingumbalu gumbulu na kwa kubahatisha.
Aanaweza kufuatilia hili na afuatilie, kwa manufaa ya watz, jamani wenzetu wanakufa.
End