Wizara ya Afya Inavyowaua!

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Linapokuwa suala la dawa za ARV ambazo hutolewa bila malipo kwa walengwa, kinakuja kichekesho. Kwanza wafamasia wanasema kuna uwezekano mkubwa watumiaji wanatumia dawa hizi chini ya dozi wanayotakiwa na hivyo kukamilisha safari ya kuviofanya HIV kuwa sugu dhidi ya dawa hizi. hapa wagonjwa watalazimika kutumia dawa zinazoitwa second line drug ambazo nazo ni aghali mno, ambapo kampuni zinazotengeneza zinadai kuuza kwa zaidi ya $1000 kwa dozi ya mwaka. hapa tena inalengwa Richmond nyingine maana hata waziri wao hapigi Kelele. Cha kushangaza ufisadi ndani ya wizara hii kuhusu manunuzi haujavaliwa njuga.

Kingine ni kuwa ovedose walengwa na hivyo kuharakisha vifo vyao badala ya kuvirefusha.

Kiini cha yote haya ni Dawa zinazotolewa na MSD ambazo hufika vituoni zikiwa na sawa na kuwa zimekwisha muda wake wa matumizi. na pia Tabia ya MSD ya kutawanya dawa ambazo, badala ya kuwa kidongo kimoja chenye uzito unaotakiwa, wao sijui kwa rushwa ama misingi gani, wanasambaza dawa amba zina ujazo mdogo mdogo na hazipo pamoja, hivyo ngoma inakuja kwenye mahesabu ya kutafuta dozi kulingana na uzito, ambayo yanahitaji mfamisia, ambao kimsingi hawapo katika hospitali nyingi za JK, na badala yake zinapigwa hesabu kingumbalu gumbulu na kwa kubahatisha.

Aanaweza kufuatilia hili na afuatilie, kwa manufaa ya watz, jamani wenzetu wanakufa.

End
 
Mgoyangi umekuja na tuhuma nzito sana dhidi ya Wizara ya Afya; tuhuma ambazo implication yake ni mbaya sana.

a. Kuna ushahidi gani kuwa dosage inakuwa manipulated. Nikikumbuka pharmacology 101 kati ya vitu unavyojifunza mapema ni suala zima la umuhimu wa kujua potency ya dawa, muda inayochukua kukaa mwilini, na kiasi gani inahitajika kufikia ile effects inayohitajika. Ndio maana watu wanaambiwa usikatishe Dose ya dawa yoyote hata kama unajisikia vizuri; hakikisha umaliza ile dose. Sasa, kama manesi au wauguzi wanamanipulate dosage ya madawa siyo tu wanaweza kusababisha hicho kinachoitwa drug resistance lakini wanahatarisha juhudi za kutafuta tiba inayofaa. Sasa ni kweli haya unayoyasema?

b. Pili suala zima la kuongeza dosage nalo hilo siwezi kulishangaa sana. Kwenye hadithi yangu ya "Mama Ngaiza" ambayo ilitokana na matukio ya kweli kwenye hospitali ya Bugando; nilishuhudia mwenyewe kwa macho yangu jinsi nurse mmoja alivyojipa uwezo wa kuharakisha kifo cha mgonjwa "Jumanne" kwa vile tu hali yake ilikuwa mbaya. Alichokifanya ni kuongeza kutiririka kwa maji ya chupa yale na hivyo to poison his body with water..! Thank Heaven nilikuwa najua mambo haya kidogo na nikamchallenge na sijawahi kuona mtu mwenye sura ya hatia kama dada yule.

Sasa wengine wanafanya hivi kwa sababu wanafikiri wanatenda jambo jema. Kila dawa ni sumu na ndiyo sababu dawa zote hutolewa kwenye kiwango kinachohitajika na zinapewa maelezo ya jinsi ya kutumia. Ndiyo maana enzi za Chloroquine ulitakiwa utumia combination ya 4 4 2 na ile ya Aspirin kwa famous dosage ya "viwili kutwa mara tatu" kwa siku tatu. Hata hivyo anayeamua kunywa Chloroquine 40 kwa mkupuo huyo hatibu Malaria tena!! The same thing applies to the now forbidded "fansida"...

Sasa ni taratibu gani zilizopo zinazosimamia wauguzi kutoa madawa? Je tatizo la ukosefu wa wafamasia linaweza kutatuliwa vipi hasa ukizingatia kuwa bado HIV/AIDS bado ni tatizo?
 
Ebana eehh wewe umesomea kila kitu eehh...hadi pharmacology...duh we kweli kiboko
 
Kwa mtazamo wangu, mtoa mada ana hoja mbili, ya kwanza ni kutokuwepo uhakika wa UBORA wa ARVs, na pili ukosefu wa wafamasia wa kutosha, naomba nichangie kama ifuatavyo.
1.Tatizo la UBORA wa ARV.
Kwa maoni yangu, ni vigumu sana kutoa kauli ya kuthibitisha kwamba ARVs hazina ubora unaotakiwa kwa maneno tu. Tunahitaji ushahidi wa kisayansi wa aina mbili, ya kwanza ni Ushahidi wa maabara, huu utatuonyesha kwamba ARVs zinazotumika hazikidhi viwango vya ubora, na njia ya kupata ushahidi huu ni kupata data (kama zipo) toka mamlaka husika ambayo ndio hushughulika na mambo ya ubora wa dawa kwa kupitia kitengo chake cha Quality Assurance. Kwa kawaida Dawa yoyote inapoingizwa nchini lazima iwe registered, na ili iwe registered lazima itimize vigezo vyote vya ubora (siwezi kuvitaja hapa kwani ni shule nyingine). Na kama ikitimiza inaingia sokoni, na ikishaingia sokoni kuna ufuatiliaji mwingine unaitwa Post-market surveillance, kwa maana ya kufuatilia ubora wake ikiwa sokoni, huu ni muhimu sana kwani utaonyesha kama dawa iliyoikuwa registered ina'maintain' ubora wake. Tunahitaji kupata hizi data za hii post-market surveillance hasa kwa ARVs zinazotuhumiwa kukosa ubora ili kuthibitisha au kukanusha UBORA wa hizo ARVs. Mwenye uwezo wa kupata hizo data atupe au afuatilie kwani zitatusaidia kupata picha halisi.
2.Njia nyingine ambayo si nzuri au sio ya uhakika sana ya kupima ubora wa dawa ni pale ambapo mgojwa au wagojwa wanaotumia dawa hiyo hawapati nafuu inayotarajiwa katika muda fulani, yaani kama ni mgojwa anayetumia ARVs kwa kufuata maelekezo sahihi, tunategemea kuwa atakuwa na improvement clinically, yaani kuongezeka uzito, kupungua kwa magonjwa nyemelezi n.k. Kingine ni kuongezeka kwa chembechembe za kinga (CD4) na kupungua kwa virus mwilini. Kama haya hayatokei KWA WAGONJWA WENGI, sababu mojawapo inaweza kuwa ni ukosefu wa ubora wa dawa.Tunahitaji data kwa hili pia, ila hii inaweza kuwa research ya Phd.
CHA MSINGI ni kuwaomba TFDA na mamlaka husika wahakikishe ubora wa dawa unakuwepo kwa kufanya chunguzi za kisayansi na KUUELIMISHA umma dalili mbalimbali za dawa zisizokuwa na Ubora

UKOSEFU WA WAFAMASIA
Kweli ni wachache na wengi wako mijini, na kwa uchunguzi wangu naona hata hao wa diploma hawatoshi, kuna vyuo sidhani kama vinazidi viwili nchini kote. Pamoja na uchache wao sijaona kama wana ORGANISATION yao na kama ipo sijaisikia. Ninaamini wanaweza kutumia elimu yao kuufahamisha umma na kushauri kuhusu mambo haya muhimu.
Wafamasia wafikirie jinsi ya kuungana na fungua shule zaidi, na serikali isaidie katika hili.Kuna vyuo vingi vya AMO, nurses, lakini vya wafamasia ni vichahce mno, AU HAWAHITAJIKI? Inawezekana kazi zao huweza kufanywa na Nurses, na inawezekana umuhimu wao hauonekani Sijui kama hilo ni la kweli!!!!Mimi siamini!!!
Ninaamini kwa elimu walioipata hawa (Four Years) wanaweza kufanya zaidi ya wanavyofanya sasa kwani wengi wapo kwenye madirisha ya kutolea dawa tu,kazi ambayo pia hufanywa na technicians na wenye certificate. Naiomba Wizara ikae na hawa jamaa ili waone ni jinsi gani wanaweza kutumiwa kikamilifu kwenye shughuli za afya kwani kwenye nchi nyingine Pharmacists hufanya zaidi ya haya yanayofanywa hapa Bongoland.

Peace be with You.
 
Leo nilijiona niko busy na sina muda wa kujibu mada yoyote lakini hii imenigusa, hasa kwa kuwa wanaoumia ni wanyonge wasiojua wafanyeje kujitoa katika hatari iliyotajwa. Lingine ni matumizi mabaya ya rasilimali zetu.

Kuna jamaa zangu niliosoma nao sekondari walikuwa "vipanga" hasa kwenye masomo ya sayansi, wakafanikiwa kwenda chuo kikuu Muhimbili kusomea udaktari, wengine ufamasia. Na wote hakika hali zao ni nzuri kiuchumi hata leo. Wale madaktari wananung'unika sana kuwa wanalipwa kidogo nk, lakini ukiwaangalia hali zao ni bora kuliko wafanyakazi wengi wa serikali, kwani katika hao ninaozungumzia, wote wana nyumba zao walizojenga, usafiri wa kuridhisha na watoto wao wanasoma shule za maana. Wale wafamasia sasa, ndio zaidi wana hela balaa, na wengi wako kwenye private pharmacies mijini. Sasa ukiulizia kazi wanayofanya utashangaa sana, maana hadi leo najiuliza kulikuwa na sababu gani ya kumsomesha mtu mwenye kichwa kizuri kama kile kwa miaka minne university, tena wengine hadi level ya masters, halafu wanaishia kufanya kazi kwenye pharmacy ya mhindi (kuuza dawa, frankly! kupokea hela na kutoa chenji! kusimama pale kusubiri "wateja"! anasoma cheti kimeandikwa dawa gani, anatoa dawa kwenye shelfu, anaweka kwenye kibahasha, anampa mteja anapokea hela na kurudisha chenji, vivyo kama wanavyofanya tu wauzao vibiriti na mishumaa!) Sasa jamani hii mbona manesi wenye elimu ndogo zaidi wanafanya huko mawodini na kwenye mahospitali ya kijijini, hivyo ndio hicho tu wanachosoma wenzetu hawa? Yaani msomi na madigrii yote hayo anafanya tu kama shopkeeper? Imenifikirisha na kuniumiza sana. Nimemkuta majuzi jamaa yangu mmoja ana masters ya pharmacy kasomea Australia, na B.Pharm kasomea Muhimbili, yuko anauza dawa kwenye pharmacy fulani bongo, sasa najiuliza inakuwaje wataalamu wakubwa kama hawa tunawaacha wafanye kazi rahisi rahisi lakini zile kazi ngumu (kama hizi sasa za udhibiti wa madawa nk, nadhani kuna mikoa mingi tu haina wafamasia wa kiwango cha masters) tunawaachia wasiosoma ama wenye elimu pungufu? Imekaaje hii? Mwenye elimu kubwa yuko dukani kwa mhindi, mwenye elimu ndogo ndio yuko wilayani anadhibiti masuala ya dawa, na je mambo yakiharibika ni haki kumlaumu kweli wakati ujuzi wake ni kidogo? Hivi tukikusanya hawa wasomi wetu wenye fani za famasia, kemia nk hatuwezi kuwa na viwanda vyetu vya dawa? Sisi mabingwa wetu wanauza dawa kwenye maduka ya wahindi, wakati huko India mabingwa wao ndio wanaotengeneza hizo dawa tunazouziwa sisi!

Ushauri wangu kwa hiyo wizara ya afya, watumie vizuri wataalamu walio nao. Huu wimbo wa kuwa hakuna wataalamu mtu hawezi kunidanganya, wapo kibao hawajatumika tu vizuri. Sina data za kitakwimu lakini ninazo za uzoefu wa maisha nilizosema, na ukitafuta watu kama mimi wengi watakupa uzoefu wao ambao naamini hauna tofauti na wa kwangu. Wataalamu wenye elimu kubwa kama hawa wanapaswa kupewa kazi zenye changamoto zinazoendana na utaalamu wao, na si kuwaacha tu wanazagaa mitaani humo na kuajiriwa u-shopkeeper na watu wasiosoma, ati kisa hela iko! Jamani tunauana bila sababu namna hii! Haya bana!
 
Labda mimi niwachambulie kidogo matatizo ya MSD na ARV

1. Kwanza nakubaliana kabisa na mtoa mada kwamba Wizara ya Afya inahusika na Kuua watu(indirectly). Hapa kwetu Tanzania Dawa husambazwa na MSD nchi nzima. Matatizo ni mengi kama ifuatavyo

a) Urasimu uliopo katika Manunuzi ya Dawa hizo kutoka zinakotoka na Vikao vya Tenda hapa nchini vinasababisha muda kuwa mrefu wa dawa kuagizwa kutoka Nje ya Nchi

b) Zikifika hapa bandarini, kutokana na TICTS kuwa wazembe na uchakavu wa Vifaa, Clearance ya Dawa hapo port huchukua muda mrefu, siku hizi utakuta Meli inakaa mpaka siku 30 kule pwani bila kupakua mizigo,this is due to unnecessary congestion caused by TICTS na Karamagi wake.

c) Wakipakua Mzigo kutoka Bandarini(wakibahatika) usafirishwaji wake kutoka central store kwenda Zonal store mpaka huko kwenye mawilaya ambako ndugu zetu wengi walala hoi wagonjwa ndipo waliko ni wa michosho hakuna usafiri wa uhakika.Magari yao yameoza yalinunuliwa miaka ya 80 mpaka leo, utakuta mchuma unatumia week 3 mpaka 4 kufika Mwanza, jee kagera itakuwaje?

d) Uwezo mdogo wa watendaji wetu kuanzia ngazi ya Taifa hadi mawilayani ni mdogo sana hasa katika kupanga, hapa namaanisha Planning skills, hasa kuestimate ARV need ya Taifa letu iwiane na mahitaji.

e)Mfumo duni wa Taarifa za wagonjwa kutoka katika vituo vya afya mpaka Taifani ni kasheshe. Hapa namaanisha Health Management Information systems pamoja na Monitoring and Evaluation Report hazitumwi kwa wakati makao makuu. Hii inatokana na watendaji wengi Mawilayani hawana elimu ya kutosha katika maswala haya ya takwimu na utoaji wa taarifa muhimu.

2. Utegemezi kwa Wafadhili, hii ni kutokana na manunuzi ya dawa hizi kwa kiasi kikubwa tunategemeea mabwana zetu wazungu watakavyojisikia, maana kuna taarifa kuwa kuna kipindi Global Fund walichelewa kutoa pesa zao hapa ilikuwa kasheshe kwani kwenye stock dawa ziliisha na pesa hatukunazo, Mafisadi washaaiba . Kumbuka mgonjwa akianza dose hatakiwi kuacha .hii Mzee ni life time medication, if it happen one has to terminate the dose, Chances for developing Resistance are very high. na hicho ndio kifo chenyewe.

3.Weak health system and infrastructure, jamani bado wafamasia, madaktari hawatoshi, majengo mabovu,Maabara zipo hoi, ili mgonjwa aanze dawa kuna maandalizi jamani lazima upime damu kucheck CD4 counts, Liver Function test maana madawa ni makali, Renal test vyote hivi ni vipimo muhimu sana kwa mtu kuanza Dawa. Hospitali nyingi Wilayani hivi vipimo ni hadithi watanzania wenzangu.

4. Bado Serikali haijajicomit vizuri kisawa sawa kuondoa tatizo hili, hawa CCM hawajajua vipaumbele vyetu bado, acha wafichane majina siku zao zinahesabika shime ndugu zangu shime tumuondoe nyani huyu.

NAWAKILISHA!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ndorobo,

MSD kuna matatizo mengi sana sana, thanks for analyzing that. Mwaka jana baada ya bunge kukaa, nilipata habari kuwa wabunge walivaa njuga kuhusiana na suala zima la MSD na utendaji wake wa kazi; kufikia mahali walikuwa wakitoa pendekezo MSD ifunjwe(or so). In short; Wizara husika iliomba isijunjwe kwanza, waliomba wapewe muda kwamba watateua tume ambayo ingefuatilia malalamiko, upotevu madawa, na pesa na uongozi wa sasa. Walisema wangewakilisha ripoti yao wakati bunge litapokaa tena Februari ya 2008. Sasa Februari imeshapita, unajua/umesikia anything about it or anyone for that matter?
 
Linapokuwa suala la dawa za ARV ambazo hutolewa bila malipo kwa walengwa, kinakuja kichekesho. Kwanza wafamasia wanasema kuna uwezekano mkubwa watumiaji wanatumia dawa hizi chini ya dozi wanayotakiwa na hivyo kukamilisha safari ya kuviofanya HIV kuwa sugu dhidi ya dawa hizi.
Mgoyangi ahsante kwa observation yako,
kwa kiasi fulani napingana na wewe.
1. Dawa za ARV zinatolewa bila malipo kutokana na kuwa 'subsdized', na hizi dawa hazitolewi kama za TB -kwa mtindo wa 'DOTS', mgonjwa anapewa dawa akatumie nyumbani mwenyewe chini ya uangalizi wa jamaa zake (treatment partner), hivyo anaweza akameza tofauti na alivyoelekezwa au asimeze kabisa kulingana na utashi wake.
2. Moja ya sababu inayosababisha resistance ni drug adherance, kwa kiasi kikubwa inatokana na matumizi ya siyosahihi ya dawa, iwe overdose, underdose, misdose etc. Wagonjwa pamoja na watoa huduma kwa namna moja au nyingine wanachangi katika hili.

hapa wagonjwa watalazimika kutumia dawa zinazoitwa second line drug ambazo nazo ni aghali mno, ambapo kampuni zinazotengeneza zinadai kuuza kwa zaidi ya $1000 kwa dozi ya mwaka. hapa tena inalengwa Richmond nyingine maana hata waziri wao hapigi Kelele.
Actually hizi dawa zimeshaanza kutumika tayari, na zinapatikana bila malipo pia.

Cha kushangaza ufisadi ndani ya wizara hii kuhusu manunuzi haujavaliwa njuga.

Kiini cha yote haya ni Dawa zinazotolewa na MSD ambazo
1. hufika vituoni zikiwa na sawa na kuwa zimekwisha muda wake wa matumizi.
2. na pia Tabia ya MSD ya kutawanya dawa ambazo, badala ya kuwa kidongo kimoja chenye uzito unaotakiwa,
3. wao sijui kwa rushwa ama misingi gani,

Manunuzi ya serikali yanataratibu zake, na ukumbuke pia dawa si kama bidhaa nyingine. zina mambo mengi zaidi ili 'kuachieve required pharmacological/therapeutic outcomes'.

Recently kulikuwa na crisis ya ARVs, serikali imefanya manunuzi wa dhalula kufidia hili pengo.

Si dhani kama MSD peke yake wanapaswa kulaumiwa kwa hili la ARVs,
watendaji wetu(mahospitali/vituo vya afya etc) wanawajibika zaidi kubeba lawama.
Kwanza takwimu mahospitalini kwetu ziko chini sana, nafikiri ukiuliza kwa mwezi wanatumia dawa kiasi gani na projection ya wagonjwa wapya kila mwezi ni wangapi, wengi hawajui.
Kama hujui haya utawezaje kustock dawa za kuwatosha wagonjwa wako?

wanasambaza dawa amba zina ujazo mdogo mdogo na hazipo pamoja, hivyo ngoma inakuja kwenye mahesabu ya kutafuta dozi kulingana na uzito, ambayo yanahitaji mfamisia, ambao kimsingi hawapo katika hospitali nyingi za JK, na badala yake zinapigwa hesabu kingumbalu gumbulu na kwa kubahatisha

Kuwepo na dawa kwa kulingana na uzito (kama Alu-new firstline for malaria tretment) ni vema, lakini inategemeana na mambo mengi (pharmaceutical industry).
Mimi naridhika na 'current formulations' zinakidhi mahitaji ya walengwa katika umri mbalimbali.

Kuhusu idadi ya wafamasia, ni kweli wako kidogo kwa ujumla .
Serikali ilisimamisha ajira na hii iliathiri sector ya afya,

Sidhani kama ni rahisi mtu alishajiimalisha 'kwa muhindi kuwa sales person/kutoa change' na akaanze upya kuwa mfamasia Namtumbo tena kwa TGS F.3 na probation ya mwaka mmoja.
 
Ndorobo,

MSD kuna matatizo mengi sana sana, thanks for analyzing that. Mwaka jana baada ya bunge kukaa, nilipata habari kuwa wabunge walivaa njuga kuhusiana na suala zima la MSD na utendaji wake wa kazi; kufikia mahali walikuwa wakitoa pendekezo MSD ifunjwe(or so). In short; Wizara husika iliomba isijunjwe kwanza, waliomba wapewe muda kwamba watateua tume ambayo ingefuatilia malalamiko, upotevu madawa, na pesa na uongozi wa sasa. Walisema wangewakilisha ripoti yao wakati bunge litapokaa tena Februari ya 2008. Sasa Februari imeshapita, unajua/umesikia anything about it or anyone for that matter?

Pamoja na kuwa saa nyingine MSD huwa wananibore hasa kwa sisi ambao tuko mbali na bandari ya salama, lakini bado nawatetea kwa kiasi fulani.
Wanafurahia MSD ivunjwe ili wanunue dawa nje (private) ili wapate 10%.

Soma hii report kama utakuwa na muda

[media]http://www.who.int/hiv/amds/en/tanzania.pdf[/media]
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom