Inasikitisha sanaNajaribu kuviwazia vilivyokua vinaomba ndani ya boksi
Wale wabunge tulioambiwa wako kwenye list ya risasi waliisha hadi waingilie uhuru wa kuku!!!
Nathani Kama wamefanya kwa mujibu wa Sheria, hakuna haja ya kujificha bali kuweka wazi ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kukiuka taratibu za kuingingiza vifaranga nchini, mbona didhaa nyingine fake kama vle TV na vipodozi huteketezwa hadharani ?
naonawangechoma kwa siri..
Itathibitkaje ikiwa umeambiwa hawakupimwaWizara iko sahihi ,Kuhusu bidhaa zisizo na ubora kama zimethibitika na mamlaka husika zinapigwa chini, mbona tunachoma vifaa fake vingi kutoka nje? ni mara ngapi vitu vimepatikana airport au bandari tena macontainer yanakamatwa na yanachomwa moto? je huwa tuna ugomvi na hizo nchi ambazo watanzania wamenunua bidhaa hizo? tatizo tumekubali kujenga undugu usio na tija na nchi jirani hivyo kupelekea kushindwa kusema hapana hata kwa mambo yasio na msingi, tukipata chickenpox ndo tutajua ni kwa nini serikali inakataza hao vifaranga.
Kikubwa ambacho kitaleta stability kati yetu na nchi zote za jirani, ni serikali ya Tanzania kuanza kutenga maeneo maalum kwa ajiri ya kuchungia mifugo hasa kwa wananchi wanaoishi maeno ya mipakani au karibu na mipakani.
Wizara ya mifugo na uvuvi imetetea uamuzi wa kuchoma vifaranga kwani ni utaratibu unaotambulika kimataifa na kwa mujibu wa sheria namba 17 ya sheria ya wanyama ya mwaka 2003 imechukua uamuzi huo wa kuteketeza vifaranga hivyo 6400 ili kuepusha kusambaza mafua ya ndege.
Msimamo huo umetolewa na katibu mkuu wa wizara, amesema hatua hio imefikiwa kuzuia kuenea ugonjwa wa aina yoyote wa kuku kuingia kwenye kuku wa nchini na kuzuia uingizaji holela wa vifaranga bila kupitia utaratibu na sheria zilizopo.
Amesema hasara ambayo ingeletwa na vifaranga 6400 kama wangeingia kwa namna waliyoingia na kuleta madhara yangekuwa makubwa zaidi kuliko yanayoonekana kwa kuteketeza vifaranga 6400.
Alipoulizwa kama hakukuwa na namna nyingine ya kuviaribu zaidi ya kuviteketeza hadharani, amesema havikuchomwa hadharani na amesema waliosambaza hizo picha walikuwa na lengo tofauti, amesema vitu vinavyofanyika nje ya hadhara maana yake havitakiwi kuonekana kwenye hadhara na mtu akikiuka ndio analeta madhara kama yaliyotokea.
Amesema utaratibu wa kuwachoma umetumika pia na mataifa mengine akitolea mfano Ulaya kilipotokea kichaa cha Ng'ombe lakini amesema sio kitendo cha kumuonyesha kila mtu ndivyo walivyofanyiwa.
Kuhusu kuwapima, amesema hawawezi kupima vifaranga ambavyo tangu awali walishatoa katazo visiingie nchini.