Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Rais Samia amesema amri ya kuchoma vifaranga 6400 vilivyoingizwa kutoka Kenya miaka mitano iliyopita ilikuwa sio sawa.

Rais Samia kasema hawakushulikia vizuri uingizaji ule wa vifaranga maana pia vifaranga vinavyo haki ya kuishi.

Rais Samia alizungumza haya wakati akiongea na mawakili wa ukanda ya Afrika Mashariki.

"Afrika Mashariki tuna soko la pamoja ambalo linatusaidia kufanya biashara zetu, tunakubaliana kwenye mambo ya customs na taxation lakini we had a lot of NTB's na ni tariff barriers ambazo mnajitahidi kuzifanyia kazi kuziondosha.

Ni kitu kidogo tu, ni mmoja kutoka kwenda kwa mwingine. Wakati mimi sikuingia, biashara yetu na Kenya ilikuwa ngumu sana, ngumu sana. Fika vifaranga mipakani pale, makaratasi hayasomi vizuri, vimetoka wapi haisemi vizuri, kunapita vifungu vya sheria as if sheria is everything. No no no sheria hairuhusu, solution hata hatuogopi dhambi, choma hivyo vifaranga.

Tumejisahau, vifaranga pia ni viumbe vya Mungu, walikuwa na life tukachoma"

Alisema Rais Samia

pic-vifaranga.jpg
 
Kuvichoma ilikuwa ukatili ilitakiwa wazuie visiingie nchini virudishwe viliko toka au viwekwe quarantine vipewe chanjo zote, vikaguliwe vigezo vya kuingiza vitu kama vile kama sheria inavyotaka kisha wapigwe faini walio ingiza bila kufuata sheria.
Kuchoma ilikuwa ukatili, pia siamini ama a,mri ilitoka kwa mkuu wa nchi. Kama ndivyo mkuu alikosea.
 
Wataalamu waliovichoma ndio tatizo!
 
Rais Samia amesema amri ya kuchoma vifaranga 6400 vilivyoingizwa kutoka Kenya miaka mitano iliyopita ilikuwa sio sawa.

Rais Samia kasema hawakushulikia vizuri uingizaji ule wa vifaranga maana pia vifaranga vinavyo haki ya kuishi.

Kuhusu biashara na Kenya, Rais Samia kasema mpaka karibuni ilikuwa ngumu, vikwazo vingi na kuchoma vifaranga ilifanya mambo yawe mabaya.

Rais Samia alizubgumza haya wakati akiongea na mawakili wa ukanda ya Afrika Mashariki.

View attachment 2427229
CC National Anthem
Mambo ya jiwe haya
 
Huyu mama asiongee haya, maana alikuwa ni sehemu ya utawala uliopita na alifurahi na hata sasa anafanya muendelezo wa yaliyopita na anaharibu zaidi kaweka magenge ya wezi.. Kujadili kilichopita na kukwepa matatizo yaliyopo ni janja janja yake ingine.. Nchi ime mshindwa
Siangalii sana kuongea, Hebu angalia mateso waliyoyapata wale vifaranga..!! Kwanini hawakuwarudisha walikotoka?
 
Back
Top Bottom