Uchomaji wa vifaranga wa Kenya ulikuwa sahihi kwa usalama, tuache siasa

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,731
Wabongo wengi ni mbumbumbu sana na Bahati mbaya hadi mkuu wetu anaingizwa mkenge sana kwenye huu ujinga wa Watanzania wengine.

Swala la kuchoma Vifaranga/Ndege/wanyama/mimea inayo ingizwa nchini bila vibali ni swala la kiusalama zaidi na kulinda afya za raia.Uteketezaji haufanywi Tanzania pekeee bali ni Dunia nzima huwa wanafanya hivyo, nenda Zimbawe haipiti miezi miwili bila kuteketeza vifaranga vya magendo kutoka South Africa, Kuna nchi huchoma moto Ng'ombe za magendo achilia mbali vifaranga.

Sababu kubwa ni kwamba haijulikani hao vifaranga wametoka wapi hasa,Usalama wao nani anaujua? vipi kama waliletwa kutoka nchi yenye mafua ya ndege? na wanataka kuingizwa kinyemela ili kuleta magonjwa nchini? nani alikuwa na uhakika kwamba hao vifaranga ni salama make hawana makaratasi yoyote.

FAO wenyewe wana sisitiza hili, WHO pia wanasisistiza hili, na uteketezaji hufanywa hadi kwa mimea ambayo imeingizwa nchini bila kuwa na documents zozote kuna mimea inaweza leta balaa kwa mimea yetu hasa mazao.

Sasa kwa sababu tunashikiwa akili tunazania ile ilikiwa ni Amri ya Magufuri kuchoma wakati ni sheria ipo na inasema hivyo kwamba wateketezwe bila kujalisha wanatokea nchi gani.Mama naye inaonekana ni mweupe sana kwenye mamb mengi sana na sasa na walamba asali wanatumia hio nafasi kumdanganya kila kitu.

Nchi kama Zambia, Zimbabwe, Botswana na Namibia swala la kuteketeza ndege hasa vifaranga wa magendo kutoka South Africa ni la kawaida sana tena kule sio box 5 bali ni unakuta vifaramga 10, 000+ wanapigwa moto, sasa je uhusiano wa hizo nchi na South Africa umeharibika kwa sababu hio?

Wakenya ni wajanja wajanja sana wanajua ni makosa kuingiza ndege/wanyama nchi nyingine bila vibali ila sasa wanatumia umbumbu wa Watanzania ionekane kwamba Tanzania ilifanya makosa kumbe ni sahihi kabisa.

Na na shangaa Wizara ya mifugo wanashindwa kumpa ukweli Mama kwamba ile ilikuwa sahihi na ni sheria zinasema hivyo sio swala la mtu mmoja.

Mnajua mafua ya ndege? Vipi wale vigaranga wangekuwa wana mafua ya ndege?
 
Waeweke karantini, kiumbe chochote kina haki ya kuishi nacho husikia maumivu kama uyasikiayo wewe, usitetee ukatiri dhidi ya viumbe.

Hivi karibuni kuna mcheza mpira huko uingereza alionekana akimpiga teke paka wake nyumbani kwake, kilichompata kilimgharimu na kumpa fundisho.
 
UMEAMBIWA NI TAKWA LA KISHERIA...
PUNGUZENI HISIA!!...

BISHA KWA HOJA BASI..
Dah
 
Tusiwe biased, tuongozwe na Kweli na HAKI.

Kiongozi yeyote akifanya baya asemwe na akifanya zuri apongezwe.

Magu alifanya Mengi MAZURI, kuchomwa vifaranga hakufanya vizuri ingawa wakenya Wana HILA sana.

Hata msiba wa magu ulipokuwa Unaendelea, Citizen TV ilikuwa live pia ikitangaza kuwa aliyefariki ni Governor wa county ya Jericho.

Unaeza ona tuna Jirani wa aina Gani, so sa100 kurudisha uhusiano awe makini.
 
Waeweke karantini, kiumbe chochote kina haki ya kuishi nacho husikia maumivu kama uyasikiayo wewe, usitetee ukatiri dhidi ya viumbe.
Hivi karibuni kuna mcheza mpira huko uingereza alionekana akimpiga teke paka wake nyumbani kwake, kilichompata kilimgharimu na kumpa fundisho.
Unakula nyama?samaki?
 
Sasa kipindi hiki kuna uchumi upi?
We unaelewaje uchumi labda tuanzie hapo. Unaposikia uchumi ni kitu kinakujia kichwani ambacho hukioni kw serikali hii. Au huelwi chochote kuhusu uchumi Mana watanzania wengi ni mbumbumbu hamna kitu kichwani
 
Huna unachojua wewe mramba mata. Kle!

Uchumi upi? Huu wa kukopa til. 20 ndani ya mwaka 1?
 
Back
Top Bottom