mwanamabadiliko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 843
- 1,363
Wizara ya Nishati umeshindwa kutatua kero za kuunga umeme kwa wananchi na badala yake imezidisha ugumu wa kupata huduma ya umeme hasa kwa wateja Wanahitaji nguzo 1,2,3,4,5,6,7,8,9, Hadi kumi.
Wizara ilitoa sharti gumu kwa TANESCO inayojiendesha kihasara kupunguza gharama za umeme wa nguzo na kufanya zote ziwe 27,000/= yaani mtu atalipia nguzo moja 27000 badala ya 177000/= nguzo mbili atalipia 27000/= badala ya 385000 na hata mtu akitaka nguzo 10 atalipia 27000/=
Maelekezo hayo ni hatua nzuri kwa machoni kwa wengi lakini kiukweli watu Wana zaidi ya mwaka mmoja hawajaungiwa umeme na wamelipia nguzo 27000. Kiuhalisia TANESCO hawana bajeti ya kulipia hizo nguzo, hivyo wananchi wengi kukosa umeme.
Ukitaka kulipia gharama halisi tanesco hawataki wanaogopa kufukuzwa kazi lakini hapo hapo mteja hapati huduma.
TANESCO wanadai walilazimishwa na serikali kuwalipisha watu 27000, Ila wao hawakuridhia, hivyo kwao ni sawa wananchi kuendelea kukosa umeme. Naamini serikali itatatua shida hii na kuacha kuitwika tanesco mizigo na lawama