Wivu wa Baba na Mama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wivu wa Baba na Mama!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PakaJimmy, Mar 20, 2012.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wakubwa,

  Nilishasikia toka zamani kidogo kuwa kawaida Baba ndani ya nyumba anapata wivu kidogo inapofikia wakati wa kumuoza bintiye, hali kadhalika Mama anakuwa na aina fulani ya kijicho pale Kijana wake wa kiume anapotangaza kuanzisha uchumba na binti wa mtu kwa nia kumuoa!...

  Huenda wengine tumeshaona Live pale binti anapoleta habari nyumbani kuwa amepata Mchumba, Mama anaweza kuipokea taarifa hiyo kwa vigelegele, lakini Baba itamchukua muda kidogo, na wakati mwingine ataanzisha sababu sababu, na hata kufikia baadaye kumkataa kijana muoaji!

  Binafsi sasa hivi nina'handle 'ushenga' ambao una mvutano mkali sana kati ya Baba na Bintiye, ambapo baba anaonyesha wazi kutokumkubali kijana muoaji bila sababu za msingi, na anasema kuwa "huyo mwanaume atakuja kukuacha baadaye"...My hairs!
  Wanajamvi, naomba maoni yenu endapo jambo hili la wivu lina ukweli ama ni hisia tu!
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Huwa inatokea kwenye family ambazo hazina maadiri ya dini!
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  mmmh....shemeji....hii ndio naisikia leo....
  baba kwa binti.....mama kwa kijana......
  hainiingii ujue.....
   
 4. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ipo dada preta, hujachunguza tu kwa makini kwenye familia....Ni kweli kwamba kama Imani haijawajenga wanafamilia huangukia huku zaidi..
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmh hakunaga izo bwana pj?
  huyo mzee ana yake si unajua wanaume wa dotcom hata makindayao wanarusha?
  sket yeyote haikatizi kizazi hiki loh
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Upande wa baba

  Wanaume wanajuana wenyewe.... hasa kwa machafu yao! Wanajua nini wanafanya, wanajua ni jinsi gani kwa kiasi kikubwa wana manipulate wanawake.... Wanajua kwa kiasi kikubwa jinsi gani hua wana tabia za kishenzi. Baba anaposikia mtoto wake kapata mchumba hua anapata shock! (kwanza wengine wapo so naive hadi hudhani binti yake ni bikira bado hali binti tayari ni mkomavu na kama sio kutoa mimba angekua hata mama wa watoto hata wa 2-4); Anaanza mawazo ya yaani anaenda galagazwa kama ninavo galagaza wanawake wengine? yaani aende kuchezewa (hapa baba huona ni uchafu na kusahau kabisa kitu chaitwa mapenzi!) Humuuuuma sababu hapo ndio hukumbuka story zoote ambazo ziko disavantaged kwa wanawake alizo kua/anazo piga kijiweni, kwenye ma bar, na his fellow men ambazo huzungumza the way huwachezea wanawake..... na anatamani binti yake huyo arudi umri wa mia 10 kurudi chini when life was so simple na him (baba) ndio center ya maisha ya huyo mtoto.... The only true man for a long time.... na mabinti we love our fathers in a way it makes them feel so speacial as a man and a dad. Ndio maana wengine hadi huvuka mpaka na kulala na binti zao..... Sad.

  Uzuri wa akina baba.... Once he comes to terms kua bintie anaolewa na akaolewa.... Wengi eventually wanakua at peace na mwanaume alie oa binti yake....


  Kwa akina Mama

  Sijui ni kwa nini ila Mungu ameumba yule mtoto wa kiume kumpenda saana mamake wakati mdogo... Hili nimeona kwingi. Mara nying mtoto wa kike hana habari na mamake na hua karibu na babake na she does not care about the Mom. Ndio maana mara nyingi mabinti huwa hawapatani sana na mama zao hadi wawe wakubwa/wazae/waolewe na the like.... Mama anaposikia mtoto wake anaoa.... Anachanganikiwa kabisa! kama ni mchafu na mshirikina naona na akili upaa.... Anakumbuka yote yale alowafanyia watoto wa wanawake wenzie.... mauchafu alo walisha, Jinsi alivo weza kufaulu kumvuta mumewe kutojali familia yao ipasavo na jinsi alivo in control na mambo mengi ya msingi ya huyo mwanaume. Inamuuuma kwamba mtoto wangu wa kiume nimekua nae karibu kwa miaka yoooote hii (kama ni 27 onwards or whatever) anakuja binti ambae kamfahamu juzi tu ndio awe in control? Nimemsomesha mtoto wangu hadi kawa na maisha na uwezo sana hivo anakuja binti kua in control? Anaingiwa na hofu..... kua sasa ndio ampoteza mwanae.... na asipokua makini binti atamzidi kete kwa mwanae!

  Bahati mbaya kwa wanawake.... they do not come in term hata ndoa ifungwe..... Hili ndio hufanya vita kati ya mama mkwe na mkamwana kutokuja isha! Alafu bahati mbaya sana wanawake wengi wamekosa busara na hutaka shindana na wakwe zao badala ya kuwaelewa na kuwa ignore....

  Baba na Mama siku moja walikua young.... na walifanya mambo ambayo walisahau kabisa kutafakari na kufikiria kua What goes around comes back around.....

  Huo ndio mtazamo wangu....
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmh hakunaga izo bwana pj?
  huyo mzee ana yake si unajua wanaume wa dotcom hata makindayao wanarusha?
  sket yeyote haikatizi kizazi hiki loh
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Angalia father of the bride, utapata jibu.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  ADI,
  U r really expert in these matters!
  Actually hii kitu ni kweli kabisa na nimeigundua kwa huyu m'baba ambaye nimemsema hapo juu!...Hakika bintiye ni mzuri kweli na ameumbika haswa, nadhani akimwangalia anasikitika sana jinsi atakavyoshughulikiwa na jamaa, hadi anaona bora abaki nyumbani tu!
  Kwa akina mama mimi nimegundua kuwa zaidi ni masuala ya maslahi!..Wanakuwa na hofu kuwa hawatopata zawadi anymore toka kwa kijana wao, maana ana wa kumpa sasa!...

  ADI, thanx alot for excavating the depths of the matter!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Anyway, kwa vile sijui umri zenu!
  Lakini kama nilivyowaelezeni pale juu, nina mifano hai kabisa!
  Kama ungedhani Baba anamkataa kijana labda kwa vile hana uwezo , jibu ni Nooo!..Kwa case hiyo kijana ni mtumishi wa Kampuni kubwa tu, yuko njema in short, lakini Baba ana hisia mbaya kabisa kuhusu kumwachilia bintiye kumleta huyo jamaa pale kwake!~

   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  MjombaKaka,
  Hii si lazima!
  Dini si ishu kabisa, maana kwa ishu niliyoona, Mzee husika ni mtu wa dini sana, na hakosi kunako nyumba za Ibada, lakini anaposikia ishu ya binti kumleta jamaa, akili zinamruka!
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Asante for the acknowledgement PJ...

  na kwa kuongezea sio tu swala la maslahi kwa akina mama...
  hata tu maovu yao ya chini chini...
   
 13. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hata mi hii nimeshaiona. Kuna ndugu yangu mmoja bintiye alitaka kuolewa vikwazo alivyovitoa wote tulistaajabu.
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Huyo kijana aliyekuchagua uwe mshenga yawezekana ni sharo ndo maana baba amemshtukia
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mie huwa naona tu inakuwa huzuni kwa wazazi kuondokewa na mtoto wao..ila la wivu ndo nasikia shemeji,,
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  mie mgeni hapa Yerusalemu, acha nipate maujuzi tu...
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  No Thank you!
  Ni mtafutaji mbaya, na ana machungu na life!
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa, haya mambo yamewahi tokea kwa mtu wangu wa karibu kabisa.
  Baba wa binti alikataa kata kata kupokea uchumba kwa sababu zisizo na msingi.
  Baada ya jamaa kusubiri kama mwaka mzima, ikabidi amtoroshe binti na kumuoa kwa nguvu baadae ndo wakahalalisha.
  Nilivyoaccess ile situation sababu kubwa ilikuwa,
  1. Baba alikuwa kiwembe sana, alikuwa anareflect tabia yake kwa kijana aliyetaka kumuoa binti yake.
  Mwanamme akiwa mhuni sana, haamini kama kuna mwanamme mwingine dunuani mwaminifu au anayeweza kuishi na mke kwa furaha. (Anajaribu kumlindwa kwa kitu kisocho hatari)

  2. Baba wengine wana wivu usio na kichwa wala miguu kwa watoto wao, anataka kumlinda hadi siku anaingia kaburini bila sababu ya msingi.
  3. Dini ilikuwa tofauti
  4. Race, kijana alikuwa mwarabu na binti mswahili so ni kama hakuwa confortable na mwanae kwenda kule.
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Ni kitu cha ajabu sana!...We mkuu chukulia we una binti akamleta chalii nyumbani, vipi utakuwa Normal au mkuu utalianzisha?
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Kiukweli,

  Hata mie nna kawivu na tubinti twangu.

  Atakayekuja kuniletea posa kwa binti zangu anapaswa awe kamili. Nna mpango wa kumiliki AK47 muda si mrafu.
   
Loading...