Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,231
WIVU
Envy is the art of counting the other fellow’s blessings instead of your own.” – Harold Coffin
Wivu ni sanaa ya kuhesabu baraka za wengine badala ya kuhesabu baraka zako. Na wivu unapokuzidi una kufumba macho unakua huoni dunia ipasavyo. Ili ufanikiwe toa wivu katika moyo wako. Alafu anza kupambana uwe bora zaidi ya jana. Usijilinganishe na wengine hapana. Ila jitaidi upate 5 kama jana ulikua na mbili.
Epuka kuwa na wivu, hauwezi kukusaidia bali unakurudisha nyuma. Wivu unapokuzidi unakua huoni mbele. Unakua huwazi mazuri na unakata tamaa na kujiona huna lolote katika maisha yako. Ila ukipenda kitu kwa mtu jaribu kumfuata na ongea nae. Akuwezeshe akikutosa tafuta njia Ingine ila usiweke wivu na chuki.
Wivu unakufanya ujilinganishe na wengine na hatimaye uone wewe huwezi. Wivu daima una kurudisha nyuma. Amini kuwa Mungu kawapa binadamu wote baraka sawa. Ukiona mtu kakuzidi jitaidi kutafuta njia yako. Kuna wengine watakula kwa shule, biashara na kipaji. Tafuta njia yako.
Wivu utakukatisha tamaa na kuona wewe haufai.
Wivu unaweza kukufanya ukawa mchawi na mshirikina. Punguza wivu utatua mzigo mzito sana maishani mwako. Kuna watu wanaangaika kuwashusha wenzao hata kwa imani ya kishirikina yote hiyo ni sababu ya wivu.
Hapa duniani kila mtu anazo baraka zake. Wivu wa chuki utakurudisha nyuma. Huwezi pinga kudra za Mungu kwa watu wake. Kila mtu analo fungu lake. Huwezi kuziba ukiziba hapa Mungu atafungua pale.
Jiamini Na Mtangulize Mungu.