Wito wangu kwa Vijana: Usiishi Kama mwenyeji

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
"USIISHI KAMA MWENYEJI"

Anaandika Robert Heriel,
Mwanafalsafa.

Moja ya makosa makuu tunayoyakosea Vijana wa Zama za leo tuendapo Mijini au nchi za mbali, ughaibuni kutafuta maisha mazuri Kwa. Ajili yetu na familia zetu ni pamoja na "kuishi Kama wenyeji" mara tuu tufikapo ugenini, Mijini.

Hilo ni kosa kubwa sana ambalo wengi limewagharimu.

Leo Taikon atatumia muda wake kuwakumbusha na kuwaasa vijana ili mambo yao yasiende Mrama.

Vijana wengi hutafuta fursa za kwenda Mijini au nchi za nje kutafuta maisha mazuri zaidi. Kwenda mjini ni bahati kubwa, hasa majiji makubwa Kama vile Dar, Mwanza, Arusha na miji mingine mikubwa inayokua Kwa Kasi. Hata hivyo kwenda nchi za nje hasa bars Ulaya na Nchi za Scandinavia Kwa wengi huonekana Kama bahati ya dhahabu kutokana na uchumi na fursa zilizopo katika nchi hizo.

Vijana wengi wanapofika mjini wanakuwa na Ari ya kufanikiwa, wanajituma wakihangaika Kwa Hali na Mali juhudi na bidii zikiwa vifuani mwao.
Bahati mbaya ni kuwa Vijana hufanya kosa la kiufundi ambalo huwapelekea kushindwa katika vita vyao.

Unapofika nchi au miji ya ugenini unapaswa uishi Kama Mgeni, hiyo ni kanuni ya mafanikio, na hata Kama utajichanganya lazima uwe na tahadhari kubwa mazingira yasije yakakuathiri ukashindwa kutimiza malengo yako.

Huwaga nawaambia Vijana kuwa kwenye maisha hasa ya utafutaji "usipende kuzingatiwa" usipende sifa, wala usipende kutukuzwa, ishi maisha yako, Usiishi Kwa kuiga watu wengine ufikapo mjini.
Usitake kuonekana nawe umo, au nawe ni mjanja.

Watu Kama kina Taikon hatuoni shida kudharaulika, kubezwa, kuonekana washamba, hiyo ni kawaida yetu hasa tunapokuwa tunataka malengo yetu yafanikiwe.

Usipende kuheshimiwa, wewe fanya mambo yako heshima huwa inakujaga yenyewe tuu, automatically.

Vijana wengi wafikapo Mijini hujikuta wakihangaika kutaka kuendana na Kasi ya mambo ya mjini ili wasionekane washamba au watu waliopitwa na wakati. Mara nyingi nawaambiaga kutaka kuheshimiwa Kwa nguvu ni Dalili ya kujiona Duni, kutojiamini na kutojikubali. Na hii hupelekea wengi kujikuta katika ugumu wa maisha, hujikuta wakihangaika lakini mambo Yao yakizidi kuwachachia, wengine hujikuta katika matatizo Kwa kujiingiza katika biashara hatari za haramu ili tuu wajipatie Fedha zinazoenda na mambo wanayoyahangaikia.

Siku zote anzia chini, kisha panda polepole Kwa uhakika, zingatia sheria na na kanuni zote za nchi na dini yako. Mwendokasi unaua, sio barabarani tuu hata kwenye Maisha. Usipende wala usiendekeze mwendokasi katika kujipatia maendeleo na mafanikio, wengi hujikuta katika Ajali mbaya wakiyaharibu maisha yao na kuleta huzuni Kwa wazazi na ndugu zao.

Ukifika mjini hakikisha unatafuta makazi mazuri nafuu ya kuishi kulingana na kipato chako. Ikiwezekana Kama unaweza kumudu kulipia Kodi ya elfu 50 basi tafuta chumba cha elfu 40.
Usipende sifa za kijinga.

Usiishi Kama wenyeji uliowakuta,
Hata Kama wao wanaendana na Fasheni, wewe vaa nguo zao mbili tatu Kwa mwaka mzima huku ukisevu na kuhakikisha unafanya kilichokupeleka.

Mjini haujaja kuvaa vizuri
Mjini haujaja kufanya STAREHE na kukesha Bar,
Mjini haujaja kutumikishwa na watu mashuhuri Kwa kwenda kila tamasha unalolisikia kwenye matangazo ya Redioni, television au mabango ya barabarani.
Mjini haujaja kutumikishwa na kushinda makanisani hasa haya yamanabii na mitume.
Mjini haujaja kukimbizana na wanawake wadangaji wa mjini ambao watakupa mikosi na kukuharibia maisha.

Mjini haujaja ili kuçhapwa na kulalwa na waume za watu au Vijana wakikugeuza jamvi la wageni, huku ukiharibu maisha yako na watoto wako utakaowazaa Kwa uchi huohuo watakaipitia watoto wako ukawajaza mikosi ya wahuni

Mjini haujaja ili uhangaishwe na mawigi au maurembo ambayo kila siku kunakuwa na mtindo mpya.

Mjini haujaja ili uhangaishwe na kukariri nyimbo za wasaniii na kuhangaika na kuangalia tamthilia za kikorea na kituruki.

Mjini haujaja ili ujaribu kila kilevi na madawa ya STAREHE ambayo wengi hujikuta katika shimo la madawa ya kulevya ambayo yameharibu Maisha Yao.

Mjini haukuja ili uwaridhishe wanawake kingono mpaka ukajiingiza katika matumizi ya dawa za kusisimua na kubusti nguvu za kiume na kuweka ganzi Kwa kutumia Mkongo Kama sio mundende ganzi mujarabu.

Mjini haukuja ili ujitese Saluni Kwa kupaka kokoto kichwani kila siku na mitindo ya nywele ya Kula namna, nywele zionekane nyeusi tii ilhali wewe bado ni kijana hata miaka arobaini huijui na Mvi hauna

Mjini haukuja ili ujitese huko kwenye Gym Kwa ajili ya kutanua vifua na kukata matumbo na mikono, mpaka kufikia Kula powder.

Usiishi Kama mwenyeji,

Nataka nikuambie kuwa mjini umekuja kuhangaika Kwa ajili ya kukomboa maisha yako na wazazi wako jijini. Kusaidia ndugu zako walioko kijijini kuwapa connection za kazi za huku mjini.
Na Kama upo nchi za nje lazima ujue kuwa upo Kwa ajili yako, Familia yako na Nchi yako

Kuishi Kama mwenyeji kutakufanya upoteze Focus.
Na ukishapoteza focus hakuna cha maana utafanya, utaishi na kushindwa akili hata na wanyama wa porini.

Baada ya kupata unachokitaka ndio unaweza kuishi Kama mwenyeji.

Angalia baadhi ya jamii Kama wahindi, Waha, na sasa Wakinga, pengine na wapemba, na Kwa zamani wachagga hawa walikuwa wakifika ugenini wanafanya kilichowaleta.
Na wengi hupata kilichowaleta na kusingiziwa tuhuma za Uchawi na ushirikina utadhani makabila mengine sio wachawi na washirikina.

Mwisho: Usiuamini MUDA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Je mimi nilie zaliwa magomeni. Niishi vipi
Fasihi imetumika,ishu ni kwamba kesho inatia hofu kuliko leo.

Mfasihi anaharibu kuangalia case ya Prof J na wasanii.wengine kwamba pamoja na majina yao wamekwama kwenye ishu ya matibabu.

Inakuaje watu wakubwa kama Hawa waombe kuchangiwa? Waliishi kama wenyeji.
 
Safi mkuu pia na siku ingine tuletee mipango ya kuishi mjini kwa waliowenyeji yaani kuzaliwa mjini na kuachiwa mali za urithi...maana hao wageni wakishazoea mazingira wanakua wenyeji na kuvikuta vitu vilivyotafutwa na wazazi...
 
Safi mkuu pia na siku ingine tuletee mipango ya kuishi mjini kwa waliowenyeji yaani kuzaliwa mjini na kuachiwa mali za urithi...maana hao wageni wakishazoea mazingira wanakua wenyeji na kuvikuta vitu vilivyotafutwa na wazazi...


🙏🙏🙏🙏

Tupo pamoja Mkuu
 
Kwa sisi tunaojitambua tumekuelewa na tunakuomba uzidi kutushushia nondo,ila kwa tuvijana tule twa bendera hufuata upepo hatuwezi kukuelewa,tunajua kama unatupangia maisha

Hiyi mada umenikumbusha kitu kuna jamaa yangu mmoja hivi aliuvamia mjii akawa anadai hapa town nikipata gari kali la kutembelea nitakuwa nimefanikiwa lengo langu,basi kwa kuwa nilikuwa namtumia kwenye dili zangu nikamwambia ukikaza mwaka ujao na kufanyia mpango ni kweli jamaa alikaza,muda ulipo fika nikamchukulia zile Corolla Zilizo kama taxi alifurahi sana,asee kilicho mpata,najutia kwa nini nilimtimiZia matakwa yake kwa muda mfupi,sio siri Mkuu vijana wengi hatujitambui.tunapekekwa kama upepo, mkuu na kufuatilia sana ungekuwa utube ningepiga tiki kwenye kengere ili unapotoa mada niwe wa kwanza big up kwa kazi nzuri
 
Kwa sisi tunaojitambua tumekuelewa na tunakuomba uzidi kutushushia nondo,ila kwa tuvijana tule twa bendera hufuata upepo hatuwezi kukuelewa,tunajua kama unatupangia maisha,
Hiyi mada umenikumbusha kitu kuna jamaa yangu mmoja hivi aliuvamia mjii akawa anadai hapa town nikipata gari kali la kutembelea nitakuwa nimefanikiwa lengo langu,basi kwa kuwa nilikuwa namtumia kwenye dili zangu nikamwambia ukikaza mwaka ujao na kufanyia mpango ni kweli jamaa alikaza,muda ulipo fika nikamchukulia zile Corolla Zilizo kama taxi alifurahi sana,asee kilicho mpata,najutia kwa nini nilimtimiZia matakwa yake kwa muda mfupi,sio siri Mkuu vijana wengi hatujitambui.tunapekekwa kama upepo, mkuu na kufuatilia sana ungekuwa utube ningepiga tiki kwenye kengere ili unapotoa mada niwe wa kwanza big up kwa kazi nzuri


Mkuu Nashukuru Sana.

Nimekuelewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom