Uchaguzi 2020 Wito kwa Watanzania wenzangu tukiwemo sisi WanaJF, Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi chagua chama cha ukweli kwa maendeleo ya kweli

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,602
Wanabodi

Watu wameisha zoea ukitolewa wito, then wito huo uwe umetolewa na kiongozi fulani, mtu ukiwa nobody, huwezi kutoa wito.

Mimi ni nobody, lakini hapa natoa wito kwa Watanzania wenzangu tukiwemo sisi wana Jf, kwanza hiyo Tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi, twende tukapige kura kuwachagua viongozi tunaowataka, na vyama tunavyo vitataka, ila chonde chonde, tusifanye makosa!, chagua chama cha ukweli chenye uwezo wa kuleta maendeleo ya kweli!.



Kwenye kupiga kura, ukichagua chama ambacho sicho, ambacho sio chama cha ushindi, unakuwa umepoteza kura yako!.
Tukapige kura lakini tusipoteze kura zetu!.

Paskali
 
Kaka paskali una akili Sana kwenye soka hii tunaiita both teams to score au double chance Ingawa Ni mmoja kati ya wafia chama Cha kijani ila umeenda kinyume na mwenyekiti wako anaewapangia wapiga kura yupi wamchague Tena kwa vitisho.

Hongera Sana kwa kuwakumbusha watu wamchague wanaemtaka. Pia hongera kwa kujaribu kuua ndege wawili kwa jiwe moja kwani hujasema Ni chama gani hivyo una uwezo wa kusema uliwapigia kampeni chadema baada ya ushindi wao 28 October.
 
Hakuna chama kilichoandikwa usoni kuwa ni chama cha ushindi. Halafu upuuzi wa eti msichague chama fulani kwa kuwa mtapoteza kura zenu kwani hakitashinda ulishakufa na kina Mkapa. Nashangaa wewe umebakia duniani kuubeba upuuzi huo na mbaya zaidi unatuletea waelewa.

Huo uliobeba kichwani kwako ni upuuzi uliopitiliza kwa kizazi hiki. Hovyo kabisa!
 
Chama chochote kinaweza kuleta maendeleo kwasababu ndio kinakusanya kodi, na kuleta maendeleo kwa wananchi sio hiari ni amri kwasababu unakusanya kodi zao.

Hatutachagua mgombea anaepeleka maendeleo kule walipo mchagua, huyo ana upendeleo hatufai Watanzania.
 
Kaka paskali una akili Sana kwenye soka hii tunaiita both teams to score au double chance Ingawa Ni mmoja kati ya wafia chama cha kijani ila umeenda kinyume na mwenyekiti wako anaewapangia wapiga kura yupi wamchague Tena kwa vitisho.
Jamaa unatakiwa usome kati ya mstari, kwamba unatakiwa uchague chama cha ushindi.
 
Back
Top Bottom