Uchaguzi 2020 Wito kwa Watanzania wenzangu tukiwemo sisi WanaJF, Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi chagua chama cha ukweli kwa maendeleo ya kweli

Hatuchagui chama cha ;

1. Kutubagua kikabila na kikanda

2. Kukandamizia uhuru, haki na demokrasia

3. Kubambikia kesi wakosoaji, kuwateka, kuwatesa na kuwauwa

4. Kutoboresha maslahi ya watumishi wa umma

5. Kutolipa hela za korosho

6. Kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa vijijini kwao

Watanzania sio wajinga wanaelewa
 
Kama unavyoenda kupoteza kura yako kwa kumchagua mzee wako. Sisi tunaomchagua Lissu kura zetu azipotea kwa Hali yoyote Ile.
 
Naunga mkono hoja msipoteze kura zenu kwa kuwapigia waropokaji mpigieni kura za ndio JPM ili aendelee kuleta maendeleo.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
Ndugu yangu Pascal, awali kauli yako ilikuwa inachukuliwa kwa uzito hapa JF na heshima kubwa.

Lakini sasa hivi umekuwa kama Lyatonga Mrema na thamani yake ndani ya siasa.

Umepatwa na nini mkongwe?
 
Kwanza Uhuru, haki halafu ndipo maendeleo, Maendeleo hayana maana bila haki na uhuru.

America ni nchi yenye maendeleo makubwa katika kila nyanja lakini maendeleo hayo yanafaida gani kwa 40 million African Americans wanaobaguliwa na kuwindwa kama swala na watu weupe ili wauwawe??, they can't "breath" despite all the developments achieved by their country -- kwao hayo maendeleo ya maana gani katika hali hiyo???.

Sasa, jifunze unaposema maendeleo ni lazima kwanza utaje HAKI na UHURU wa watu.
 
Rais ametupuuza wananchi kwa miaka 5.

Na bado anaaidi.

Na hivi sasa ameanza kuahidi kupeleka maendeleo majimbo ya ccm pekee.

Haki ya raia kumchagua kiongozi wake nayo anaitaka.

Lazima aoneshwe hana haki ya kuwachagulia watu kile wanachokitaka
 
Back
Top Bottom