Uchaguzi 2020 Watanzania, uongozi haujaribiwi. Chagua kwa ajili ya Uhuru na Amani ya Watanzania

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa.

Tumetafuta kura za kutosha na kwa tathimini ya haraka tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweza kuwafahamisha watanzania wengi nchini, kuhusu ilani yao pendwa na ahadi za kiongozi wao mpenzi. Na kutegemeana na matokeo ya tafiti ndogo zilizofanyika ni kwamba mgombea wetu na ilani ya chama chetu imefanikiwa kueleweka na kupokelewa vema, na hivyo upo uwezekano mkubwa wakupata idadi ya kura zaidi ya 90% ya wapiga kura watakaojitokeza.

Leo nimekuja kuendeleza kazi ile ya kutafuta kura ya ushindi wa kishindo kwa chama chetu pendwa na mgombea wetu mpendwa, chaguo la watanzania wazalendo.

Inafahamika kuwa historia ya binadamu haiwezi abadani kujitenga na historia ya amani, ya utulivu na ya uchumi. Binadamu amekuwa akitafuta amani, utulivu na uchumi tangu alipoanza kupata ufahamu kuhusu Dunia hii. Na kwa jinsi hiyo Binadamu huyu amejikuta akikutana na usaliti na utumwa wa namna zote katika akili na hali ya maisha. Waliofanikiwa katika utumwa walishindwa katika uaminifu, vivyo waliofanikiwa katika uaminifu waliushinda utumwa.

Afrika ni bara ambalo watu wake wamepitia historia ya kutisha na kuhuzunisha kwa karne nyingi, hata kabla ya kugawanywa kwake. Inasemekana biashara ya utumwa ndani ya Afrika ilianza katika karne ya 14 huko nyuma. Ni kwa sababu gani hasa..? Ukweli wa historia ya mwafrika kuingia utumwa ni kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya viongozi wa makabila makubwa, ndio kusema historia ya mwafrika imegubikwa na usaliti. Kundi moja kujiona ni bora zaidi kuliko wenzao, kwamba ni wao pekee wanastahili lakini sio wengine. Hivyo kupelekea kusalitiana. Utashangaa Makaburu kuweza kuitawala Afrika kusini baada ya miaka 100 tu tangu kuingia kwake miaka ya 1400's. Ambapo wakaburu wa kwanza kukanyaga ardhi ya Mzee Madiba Mandela inakadiriwa idadi ya wazee wastaafu wasiozidi 200! Lakini ndio hao waliweza kuwatawala zaidi ya waafrika 100k ya wazawa.

Hivyo kwa sababu ya usaliti, Afrika tulitawaliwa. Lakini kwa kuwa Binadamu ameendelea kutafuta amani na utulivu ni dhahiri kuwa ilitakiwa Uhuru uwepo kwa waafrika ili mwafrika aweze kupata amani na utulivu. Na kwa jinsi hiyo ni katika karne ya 19, waafrika walianza kujitafutia Uhuru wao na kwa kweli ilitakiwa kujenga umoja na kujengeana hali ya kuaminiana kwanza ili kufanikisha kuikomboa Afrika. Hivyo basi, umoja wa waafrika na uongozi wenye uaminifu uliwezesha Afrika kujikomboa na watu wake kuwa huru. Na sasa waafrika wanawajibika na ujenzi wa uchumi wa nchi zao.

Leo Tanzania kama sehemu ya Afrika inatudai uaminifu wetu sisi waafrika watanzania katika kuhakikisha tunayaendeleza yale ambayo Afrika iliyahitaji kwa muda mrefu hata kuweza kujikomboa. Nao ni umoja wa waafrika, ndio kusema kuwa Tanzania, inatudai umoja wetu sisi watanzania.

Sasa tutawezaje kuilipa Tanzania? Kipindi tunaelekea uchaguzi mkuu, wajibu wetu ni kupiga kura kwenda kumchagua kiongozi ambaye atakuwa na misuli imara isiyotetereka katika kuwaunganisha watu pasi na kuwagawa katika misingi ya udini, ukabila wala hali zao kiuchumi. Kiongozi ambaye wajibu wake ni kwa Tanzania na Afrika, kiongozi ambaye kipaumbele chake ni kuendeleza na kukuza siasa zenye kufuata tamaduni za mwafrika na Afrika. Tukachague chama ambacho kinaamini katika ujamaa na kujitegemea kwamba usawa ndani ya jamii ndio msingi wa haki sawa kwa wananchi wote na hivyo huzaa matunda ya amani na utulivu na uaminifu baina ya Watanzania.

Siasa haiwezi kujitenga na Tanzania, na watanzania hawawezi kujitenga na siasa. Hivyo wajibu wetu ni kuwapima wanasiasa na kutambua ni wanasiasa gani wenye malengo ya kudumisha umoja, amani na utulivu wa Afrika! Kushindwa kutambua jambo hilo, ni kuiweka nchi katika hatari ya kurudi kule ilipotoka. Hivyo basi siasa haijaribiwa bali hutekelezwa kwa umakini na uangalifu mkubwa. Kwa miaka mitano sasa, wapo wanasiasa ambao kwa haiba zao, uwezo wao wa misuli, uzalendo wao kwa nchi umefunuliwa kwetu.

Tarehe 28/10/2020 siku ya jumatano, ni siku ambayo inaenda kutoa uelekeo wa Tanzania kwa miaka mitano na zaidi mbeleni. Ewe Mtanzania napenda nikukumbushe kuwa hakuna dalali ambaye aliwahi kumuacha salama mwenye mali. Yeye anasukumwa na faida zake binafsi na sio za mwenye mali. Dalali yeyote atakayeweza kuingia ikulu pale, ni hakika yangu watanzania hawatakuwa salama, Tanzania ni ya watanzania. Chagua mtanzania mzalendo mwenye kuiona Tanzania katika mioyo ya watanzania, na sio mwenye kuiona Tanzania katika mikataba ya madini iliyopo tu. Hiyo ni ishara ya udalali wa wazi kabisa. Amka asubuhi kisha fanya uamuzi wa kwenda kumchagua Rais wa nchi mzalendo na mwenye maamuzi magumu na mwenye kuamini katika misimamo yenye tija kwa ajili ya watanzania, hana msukumo wa uoga bali ni ukweli wa kitafiti, fahari ya Tanzania, kiongozi mfano wa kuigwa na Marais wa mataifa hata ya Ulaya na Asia, si mwingine ni Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI. Leo hii mataifa wanashangaa ni jinsi gani ajabu alivyoweza kidhibiti covid-19 bila lockdown?! Walipogundua kuwa ni maombi, sasa na wao wanaitisha maombi ndani ya nchi zao.

#chaguaMagufuli2020
#chaguaCCM2020
#Magufuli5Tena

Sauti ya Mdodomia
20/10/2020.


IMG-20201020-WA0006.jpg
 
Wazungu wa Marekani walisema hivyohivyo wakati wa Obama. Uraisi haujaribiwi. Eti nweusi kutawala ni kujaribu kana kwamba Uraisi ni kwa weupe tu. Akishinda wa Chadema ni kujaribu uraisi kana kwamba umewekwa kwa ajili ya ccm tu. Acheni hizo!!! Tukimchagua Jiwe akionekana kuburuza Watz, tunabadilisha.

Lissu ndiye hitaji kubwa la Wtz kwa sasa atakayeirudisha nchi katika misingi ya utawala wa sheria badala ya huu wa kiimla. Leo jiwe akiwa Same aliagiza ziletwe milioni 100 kukarabati Zahanati. Aibu. Hivi Uraisi sio taasisi? Hivi hakuna mfumo on place wa kufanya hivyo? Tumechoka na ujinga. Kura zote kwa Lissu.
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa...
Amani gani yakuteka watu watukuwekwa kwenye viroba kutufilisi wavuvi hiyo unaita amani hii amani bandia hatutaki amani bandia tunataka mtu ayahemu mawazo na malizetu
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa...
Jiwe alikuwa hajawahi kuwa hata kiranja wa darasa, hata wa chekechea, leo eti ni Rais......
Tunawataka Ben, Azory, Mawazo, Akwilina and many others...... hatusikii lolote katu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom